Kama unatetea uandishi wa Shanni inasikitisha sana. Mkuu ni kweli kila taaluma ina uwasilishaji wake lakini taaluma ya upolisi kama moja ya matawi ya taaluma ya sheria haina uwasilishaji wa hovyo hivi.
Mfano, alipoelezea chanzo cha ajali kazunguuka bila sababu kabisa angeweza kusema hivi;
CHANZO CHA AJALI
''Ni uzembe wa dereva wa gari aina ya RAV4 namba T___ iliyokuwa ikitokea
_ kuelekea _ ''
Sio kuleta stori zisizo na maana, ndio maana Mahakamani tunawapiga sana Jamhuri sababu ya ubovu wa uandikwaji wa maelezo polisi.
Hakuna gari inaitwa gari ya mwendokasi, mwendokasi ni kitu gani hicho? angesema tu;
''gari inayomilikiwa na UDART namba
_ mwendokasi inayofanya safari zake na ___''
Yasije yakawa ndio maelezo yatakayotumika Mahakamani, atalia mtu