Natamani wangetokea waandishi wa habari aidha wa radio au magazeti.
Wafatilie taarifa za huyu muenda kwa miguu kujua familia yake ikoje wanaomtegemea nyuma yake.....😔😔😔😔
Wakiamini baba/mume/kaka/shemeji/baba mdogo/mjomba.... atarejea leo jioni na chochote kwa ajili ya rizki ya familia.....
Walau kama ana mke au watoto basi tulioguswa tutoe mchango wa kufariji familia...😔😔😔
Na wakiweza onesha mahala familia yake ilipo kila atayeguswa na huyo mtembea kwa miguu basi kila mmoja atapeleka alichonacho kama huruma iliyotujia kwa lililompata binadamu mwenzetu.
Najua matukio ni mengi, hili sio la kwanza na sio la mwisho, huwezi changia yote ila binadamu huwa kila mmoja kwa namna yake huwa anaguswa mahala kutoa.
Kutoa ni moyo.😔😔😔