Mrejesho wa taarifa ya ajali iliyotokea Kisutu mnamo majira ya saa 05:45

Mrejesho wa taarifa ya ajali iliyotokea Kisutu mnamo majira ya saa 05:45

Naiweka hapa muone wenyewe...

MREJESHO WA TAARIFA YA AJALI ILIYOTOKEA KISUTU MNAMO MAJIRA YA SAA 05:45

Mnamo majira ya saa 06:58 niliweza kufika Eneo la tukio nilikuta ajali imetokea gari ya mwendokasi yenye usajili wa
Plate No: T 122 DGW
JINA: SHABANI NGAUGIA
Ilipata ajali Eneo la Kisutu mbele kidogo ya mataa ilikuwa inatoka Kivukoni kwenda Kimara.

Chanzo cha ajali dereva wa mwendokasi alikuwa anatoka Kivukoni kwenda Kimara alifika mataa wakati anavuka kuna gari ndogo aina ya RVA4 yenye namba ya usajili T 978 DHZ ilikuwa ikitokea posta mpya ikielekea Kivukoni ilikuwa inapita pasipo kuangalia dereva wa mwendokasi alimuona akawa anamkwepa ndipo alipoenda kugonga flame za maduka na kuleta itirafu nje ya maduka.

Ndani ya gari ya mwendokasi kulikuwa na abiria wanafunzi na wananchi wamepata majaraha madogo madogo walipelekwa Muhimbili kwa check up ila dereva wa mwendokasi ameumia sana sehem ya mguuni yupo Muhimbili akiendelea na matibabu.

Wakati ajali imetokea gari aina ya RVA4 iliyosababisha ajali ilikuwa inakimbia kuelekea Kisutu kufika mbele ikapata ajali ikagonga ukuta wa shelli ya puma Kisutu na kuaribika. Waliokuwa ndani ya gari hiyo ndogo waliumia na kupelekwa hospital dereva wa gari ndogo alivyofika hospital alikimbia akabaki Majeruhi mmoja ambae ni mwanamke.

Katika ajali hii iliyotokea akuna vifo vilivyotokea isipokuwa kuna Majeruhi na wote wako Muhimbili kwa matibabu ila dereva wa mwendokasi na watu wanne wanahali sio nzuri sana.

Reported by
Overall Incharge
Shani Mussa.
&
Zonal Incharge
Amina Juma.
Unaweza kushangaa wanakuandama wewe badala ya kumpeleka mafunzo mtu wao
 
Dereva wa mwendokasi kwanini akwepe Rav4 yenye watu wawili ilhali anajua Gari lake lina watu wengi zaidi tena wengine wakiwa taifa la kesho?! Busara ilikuwa ku-hit head-on Rav4 ili kuokoa majority
Pamoja na video kuwekwa bado unakaza fuvu
 
Kama unatetea uandishi wa Shanni inasikitisha sana. Mkuu ni kweli kila taaluma ina uwasilishaji wake lakini taaluma ya upolisi kama moja ya matawi ya taaluma ya sheria haina uwasilishaji wa hovyo hivi.

Mfano, alipoelezea chanzo cha ajali kazunguuka bila sababu kabisa angeweza kusema hivi;

CHANZO CHA AJALI
''Ni uzembe wa dereva wa gari aina ya RAV4 namba T___ iliyokuwa ikitokea _ kuelekea _ ''

Sio kuleta stori zisizo na maana, ndio maana Mahakamani tunawapiga sana Jamhuri sababu ya ubovu wa uandikwaji wa maelezo polisi.

Hakuna gari inaitwa gari ya mwendokasi, mwendokasi ni kitu gani hicho? angesema tu;

''gari inayomilikiwa na UDART namba _ mwendokasi inayofanya safari zake na ___''

Yasije yakawa ndio maelezo yatakayotumika Mahakamani, atalia mtu
Lazima itakua edited,bioashaka alikua yupo kwenye panic mode.
Nadhani hii ya kujiweka wazi,kila mmoja anakua na nafasi ya kukosoa,ndiyo inafanya polisi wawe na watu wanaojiona wangekua wao,wangefanya zaidi.
Majeshi mengine hayapati criticism hovyohovyo hivyo,mfano Magereza et al.
 
Yaani hapa nimerudia mara tatu nimetoka bila. RAV 4 ilikuwa inatokea posta ya zamani kwenda Kivukoni na mwendokasi kutoka Kivukoni kwenda Kimara halafu Rav 4 ikaelekea Kusutu, daah. Haya ni mataa yepi kwani?
😆😅🤣
Na ndiyo hawahawa wanapotosha kesi zza watu wengi tu huko vituoni zinakuwa kesi za kubambikiwa
 
Mbona ameripot kama mtu wa kawaid , asijua kanuni za barabara na kufafanua zaid

Hii ndio elimu bila viboko ndio kizaz hiki kinaanz chomoza
 
Huyu mwamba
Lazima itakua edited,bioashaka alikua yupo kwenye panic mode.
Nadhani hii ya kujiweka wazi,kila mmoja anakua na nafasi ya kukosoa,ndiyo inafanya polisi wawe na watu wanaojiona wangekua wao,wangefanya zaidi.
Majeshi mengine hayapati criticism hovyohovyo hivyo,mfano Magereza et al.
Magereza tume reserve tu zile product zao za ngozi mikono ya zile massenger bags zao sijui waliwaza nini kuzitengeneza walivyotengeneza 😂😂

Ila ni bora polisi wanavyoweka wazi hivi wakosolewe wajifunze. Hapa isisingiziwe panic sababu polisi wana mafunzo mazuri sana ya kukabili mazingira.

Hii sio mara ya kwanza, hata ukiona.michoro ya ramani za maeneo uhalifu mf. Mauaji yalipofanyika unaweza ukajiuliza hivi tupo serious au tunatania, huwezi ukaamini kabisa ni vitu vya kustaajabisha sana.
 
😆😅🤣
Na ndiyo hawahawa wanapotosha kesi zza watu wengi tu huko vituoni zinakuwa kesi za kubambikiwa
Kila nikikumbuka jiografia yangu niijuayo kuhusu posta na Kisutu na Kivukoni sipati majibu kabisa. Labda sikuhizi kumebadilika kiasi najiuliza haya mataa ni ya wapi? Zile barabara zina majina kwanini asingetumia majina ya barabara katika ripoti yake?
 
Back
Top Bottom