Mrejesho wa taarifa ya ajali iliyotokea Kisutu mnamo majira ya saa 05:45

Mrejesho wa taarifa ya ajali iliyotokea Kisutu mnamo majira ya saa 05:45

Mbona kajitahidi sana. Hawa ndugu zetu si inasemekana ni Fa Fa Fa...kwa hiyo nampa hongera kajitahidi.
Nadhani PDF itatoka,kwa wale walioomba Polisi,itajulikana ni FaFaFa au nini?
Jamaa mbona kawasilisha vizuri tu,polisi mnawachukulia poa kwasababu wanaishi ndani ya jamii na wanashughulika na mambo ya ndani ya nchi,hivyo wananchi wengi kujifanya wanawajua saana,nakuwazia majeshi yasiyoshuguulika na mambo ya ndani,ni perfect sana na wanaoajiriwa kule ni divisione one tu na kama wamepitia vyuo wamepata first classes.
 
Ila naangalia uhalali wa pedestrian kupona ni ngumu, taarifa ya polisi ni batili
Mkuu Mungu ndio mweza wa yote. Sisi tulishawahi pata ajali pale karibu na mto Wami Busi ilivingirika kama mara tano hivi na ikawa nyang,anyang,a lakini tulipona wote isipokuwa wanawake wawili walitenguka kiuno na mkono tu lakini ukiiona Busi iliisha kabisa. Mungu ndio mpangaji wa yote.
 
Yule mtu Kama kafa,inabidi daktari adhibitishe,yaani taarifa itoke kwa daktari,lakini baadhi ya wananchi wanaamini polisi ndiyo kilakitu,hasa akiwa na ufaulu wa AAA,atatoa taarifa zote.
 
Kila taaluma ina uwasilishaji wake ulitaka aandike kama bar vicha anatoa tamko

USSR
Kama unatetea uandishi wa Shanni inasikitisha sana. Mkuu ni kweli kila taaluma ina uwasilishaji wake lakini taaluma ya upolisi kama moja ya matawi ya taaluma ya sheria haina uwasilishaji wa hovyo hivi.

Mfano, alipoelezea chanzo cha ajali kazunguuka bila sababu kabisa angeweza kusema hivi;

CHANZO CHA AJALI
''Ni uzembe wa dereva wa gari aina ya RAV4 namba T ...... iliyokuwa ikitokea .... kuelekea .... ''

Sio kuleta stori zisizo na maana, ndio maana Mahakamani tunawapiga sana Jamhuri sababu ya ubovu wa uandikwaji wa maelezo polisi.

Hakuna gari inaitwa gari ya mwendokasi, mwendokasi ni kitu gani hicho? angesema tu;

''gari inayomilikiwa na UDART namba T ....... maarufu mwendokasi, inayofanya safari zake ....... na ......''

Yasije yakawa ndio maelezo yatakayotumika Mahakamani, atalia mtu
 
Back
Top Bottom