Mrejesho wa taarifa ya ajali iliyotokea Kisutu mnamo majira ya saa 05:45

Mrejesho wa taarifa ya ajali iliyotokea Kisutu mnamo majira ya saa 05:45

Eneo la tukio washafanya repair duka linaendelea na shughuli

Wahindi wengi waoga sana wa kesi, hapo wakijakuulizwa qanakataa kabisa kama duka/fremu yao iligongwa..... (iwapo eneo limekodishwa na muhindi).

Wengine bila uoga anahela zake hataki kadhia anafanya marekebisho na maisha yanaendelea kama kawaida.

Maana kikawaida insurance ya magari kipengele cha 3rd party ilitakiwa kilipe fidia kwa waliojeruhiwa na kuharibiwa mali.
 
Natamani wangetokea waandishi wa habari aidha wa radio au magazeti.

Wafatilie taarifa za huyu muenda kwa miguu kujua familia yake ikoje wanaomtegemea nyuma yake.....😔😔😔😔
Wakiamini baba/mume/kaka/shemeji/baba mdogo/mjomba.... atarejea leo jioni na chochote kwa ajili ya rizki ya familia.....

Walau kama ana mke au watoto basi tulioguswa tutoe mchango wa kufariji familia...😔😔😔

Na wakiweza onesha mahala familia yake ilipo kila atayeguswa na huyo mtembea kwa miguu basi kila mmoja atapeleka alichonacho kama huruma iliyotujia kwa lililompata binadamu mwenzetu.

Najua matukio ni mengi, hili sio la kwanza na sio la mwisho, huwezi changia yote ila binadamu huwa kila mmoja kwa namna yake huwa anaguswa mahala kutoa.

Kutoa ni moyo.😔😔😔
Sahihi uyu bwana atakayepata taarifa zake azilete hapa jf.
 
Sahihi uyu bwana atakayepata taarifa zake azilete hapa jf.
Taarifa
JamiiForums-462031551.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naiweka hapa muone wenyewe...

MREJESHO WA TAARIFA YA AJALI ILIYOTOKEA KISUTU MNAMO MAJIRA YA SAA 05:45

Mnamo majira ya saa 06:58 niliweza kufika Eneo la tukio nilikuta ajali imetokea gari ya mwendokasi yenye usajili wa
Plate No: T 122 DGW
JINA: SHABANI NGAUGIA
Ilipata ajali Eneo la Kisutu mbele kidogo ya mataa ilikuwa inatoka Kivukoni kwenda Kimara.

Chanzo cha ajali dereva wa mwendokasi alikuwa anatoka Kivukoni kwenda Kimara alifika mataa wakati anavuka kuna gari ndogo aina ya RVA4 yenye namba ya usajili T 978 DHZ ilikuwa ikitokea posta mpya ikielekea Kivukoni ilikuwa inapita pasipo kuangalia dereva wa mwendokasi alimuona akawa anamkwepa ndipo alipoenda kugonga flame za maduka na kuleta itirafu nje ya maduka.

Ndani ya gari ya mwendokasi kulikuwa na abiria wanafunzi na wananchi wamepata majaraha madogo madogo walipelekwa Muhimbili kwa check up ila dereva wa mwendokasi ameumia sana sehem ya mguuni yupo Muhimbili akiendelea na matibabu.

Wakati ajali imetokea gari aina ya RVA4 iliyosababisha ajali ilikuwa inakimbia kuelekea Kisutu kufika mbele ikapata ajali ikagonga ukuta wa shelli ya puma Kisutu na kuaribika. Waliokuwa ndani ya gari hiyo ndogo waliumia na kupelekwa hospital dereva wa gari ndogo alivyofika hospital alikimbia akabaki Majeruhi mmoja ambae ni mwanamke.

Katika ajali hii iliyotokea akuna vifo vilivyotokea isipokuwa kuna Majeruhi na wote wako Muhimbili kwa matibabu ila dereva wa mwendokasi na watu wanne wanahali sio nzuri sana.

Reported by
Overall Incharge
Shani Mussa.
&
Zonal Incharge
Amina Juma.
Mkuu kuripoti matukio Kuna mfumo wake. Labda mhusika haufahamu.
 
Back
Top Bottom