Mrejesho wa thread ya “Hapa kuna mapenzi kweli au napotezewa muda?”

Huyu wangu alikuwa anabadilika badilika nikawa simuelewi ndiyo maana nilichelewa kujua
Pole sana mama muhimu Kama utabahatika kuingia Tena kwenye mahusiano usiruhusu Hali ya past relationship background ichukue nafasi kwenye present relationship utazidi kuumia zaidi maana sio wanaume wote watakuwa Kama ex wako Kama mnavyoaminishwa wanaume wote ni sawa, jitahidi ufunge ukurasa wanyuma wote na uingie kwenye mahusiano mapya ukiwa mpya.
 
Asante sana mkuu, nitajitahidi kujipa muda kwanza wa kuheal
 
Kati ya viumbe wagumu kukubali kuachwa ni wanawake.
Mwamba alishakuonesha signs ila wewe ukawa kichwa ngumu na bado ukamtafuta tena ili mrudiane.

Mpaka anakwambia ana mtu wake alishaona wewe huachiki hivyo hiyo njia ngumu ya kukuuumiza aliyoitumia ni sahihi.
Si ajabu ukaingia kwenye mahusiano mapya huko mbele na jamaa akarudi kupasha kiporo.

Pole sana mkuu, next time jipende kwanza, kua na uhuru wa kipato, uliomba pesa mkaishia kuzagamuana na kurudi kwenye mahusiano.

Unaonekana ni binti mwenye akili na sasa unajitambua, karibu vingunguti kidarajani nikufunze jambo.
 
Asante sana mkuu, nimejifunza sana maana nikikaa nikikumbuka niliyokuwa nafanyiwa kweli nabaini hakukuwa na upendo, wacha nipumzike kwanza kwa sasa sitaki kukurupuka tena
 
UNASTAHILI KUACHWA KWA SABABU WEWE NI MBINAFSI. Yaani mmepata ajali wote halafu unakuja kumwambia "umenisababishia shida kubwa"?..... inasikitisha sana tabia za mwanamke kama wewe. Hufai kuwa mke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…