Gambo wewe hukumuelewa Dr. Samia, amekataza matusi ya aina zote! Hayo unayo hubiri kuwa Lema ana madeni, awapigie magoti wazungu etc, ni matusi!
Hizo ndizo siasa za kutukanana. Madeni ya Lema ni personal kama sura yake ilivyo personal! Ukisha sema Lema ana kichwa kama cha mbuzi, Lema anakojoa kitandani, Lema ana madeni etc yote hayo ni kumtusi Bwana Lema.
Maana hayo yote angekuwa nayo hayamzuii kutupigania sisi watanzania kupata haki zetu.
Na tusi jingine ulilosema ni kuwa Lema ni mjomba wako! Hiyo inalisaidia nini taifa letu? Awe mjomba asiwe mjomba wewe fanya kazi uliyotumwa kufanya. Na hili liwe onyo kwa viongozi wote, mkae chini mtafakari matusi aliyokataza Dr. Samia ni yapi/nini - nasema hivi maana mpaka sasa hamuelewi siasa Safi ni nini. Kurushiana vijembe, kejeli, ni matusi pia. Na asinge ishia hapo Dr. Samia - angeendelea na kusema atakaye msema vibaya Dr Magufuli (marehemu) ashughulikiwe. Ruto wa Kenya alitamka wazi kwamba siasa za Kumchamba Kenyatta zisitishwe mara moja na ikawa hivyo. Tanzania tunataka siasa za kutuletea maendeleo siyo za vijembe.