Mrisho Gambo amvaa Lema, amtaka alipe madeni yake kwanza

Mrisho Gambo amvaa Lema, amtaka alipe madeni yake kwanza

Sasa Madeni ni kitu gani? Rais Samia tu kakopa Trillion 30 in less than 2 years.
Naona haujui hata maana ya deni la Taifa kama wewe ulikopa benki ya nje ya nchi upo kwenye hizo T30 , fikra zako zote hizo T30 kakopa mama samia, kwenye hizo wapo Mo, Rostam, Rwega etc . Kuuliza sio ujinga
 
Mrisho kashaanza kuharisha kabla hata lema hajapanda ndege Canada 2025 tutaona kivumbi
 
Kuna clip Moja inazunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha Mbunge wa Arusha mjini, Kwa tiketi ya CCM, Mrisho Gambo, alimkashifu Sana Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Godbless Lema, kuwa alikuwa mtu tapeli, ambaye hata alipokwenda salon ya kunyoa, alikuwa akiwakopa na kiondoka bila kulipa chochote!

Akaendelea Mbunge huyo kueleza kuwa Mbunge huyo wa zamani wa Arusha mjini, alikuwa pia akila chakula Kwa mama ntilie, bila kulipa!

Akazidi kuelezea Mbunge huyo Gambo kuwa hata sababu zinazotolewa na Mbunge huyo wa zamani kukimbia nchi, Kwa madai ya usalama wake, ni ya uzushi na ukweli aliodai yeye ni kuwa Mbunge huyo aliikimbia nchi, kukimbia madeni anayodaiwa sehemiu mbalimbali nchini.

Tunafahamu kuwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, wakati anaonfoa zuio hilo batili la kutofanya mikutano ya hadhara Kwa vyama vya kisiasa, alitoa tahadhari Kwa viongozi wa vyama hivyo, kufanya siasa za kistarabu na Wala siyo za matusi Wala kuchafuana.

Ninachouliza, je tahadhari hiyo aliitoa Kwa viongozi wa vyama vya upinzani pekee na kuwaacha viongozi wake wa CCM waweze kujiropokea watakavyo, kama alivyofanya Mbunge Mrisho Gambo?

Je ikitomea Lema naye ayakaporejea nchini, aamue kujibu mapigo, si ndiyo hapo patakapochimbika?

Ingekuwa vyema chama chake Cha CCM, kikumuita Mbunge huyo Mrisho Gambo, kwa kuwa ustarabu wetu wa nchi yetu, hayo maneno hayakustahili kutamkwa na mtu mwenye heshima kama yake ya ubunge, badala yake maneno hayo yalipaswa kutamkwa na vijana wa vijiweni.

Kwa nn ashindwe wakat huyo ni direct opponent , yaan hamna mtu mwingine gambo anatakiwa apambane naye from the scratch Zaid ya Lema...!!
 
Kuna clip Moja inazunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha Mbunge wa Arusha mjini, Kwa tiketi ya CCM, Mrosho Gambo, alimkashifu Sana Mbunge wa zamani wa jumbo hilo...
Lema alikuwa Mbunge na hivyo kuvaa kofia ya Mheshimiwa. Hivyo basi, kama hayo yaliyotamkwa si kweli, hata huko aliko anaweza kuchukua hatua. USIMSEMEE
 
Kuna clip Moja inazunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha Mbunge wa Arusha mjini, Kwa tiketi ya CCM, Mrosho Gambo, alimkashifu Sana Mbunge wa zamani wa jumbo hilo...
Akizidiwa atarudi kukanusha
 
GAMBO kachanganyikiwa Baba yake Magufuli hayupo tena anaogopa hana wa kumlinda kama Sabaya aliyowatendea Wana ARUSHA akiwa RC yanatisha ndio maana kaanza Visingizio Eti Wanataka Kumuua
 
Kwa nn ashindwe wakat huyo ni direct opponent , yaan hamna mtu mwingine gambo anatakiwa apambane naye from the scratch Zaid ya Lema...!!
Lakini siyo Kwa kutoa shutuma za uongo wa wazi kabisa, kuwa Lema alipokuwa akienda salon kunyoa nywele, au alipokuwa akienda Kwa mama lishe, kupata chakula, alikuwa halipi!

Kwa kuwa hizo ni tuhuma za uongo, inabidi Gambo ashughulikiwe na chama chake Cha CCM, Kwa kuwa hizo kampeni, ndiyo ambazo amezipinga vikali Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Kwa kuwa nchi yetu ni ya kistarabu na lengo letu ni kujenga umoja na mshikamano
 
Lakini siyo Kwa kutoa shutuma za uongo wa wazi kabisa, kuwa Lema alipokuwa akienda salon kunyoa nywele, au alipokuwa akienda Kwa mama lishe, kupata chakula, alikuwa halipi!
Mkuu naona tuachane nae tusije kupoteza muda na hayawani!
Tukumbuke kuwa huyu mtu hakufaa kuwa hapo alibebwa na yule dhulumati wa kura!
 
Kwamba Lema ni "guarantee kuwa ni mgombea wa ubunge Arusha kupitia Chadema"??

Yaani hata Wana chadema wengine hamuwapi nafasi ?.....

Na kwamba wewe mwana JF unashabikia hizi siasa za kumilikisha watu majimbo hata kama hawajapitishwa bado rasmi?
 
Ameanzisha ugomvi wa mawe akiwa kwenye nyumba ya vioo!!! Kwa jinsi lema alivyokuwa smart hatamjibu mapema anamsubiri kwenye Kona na siku maalumu
 
Tumdharau tu kwani ni mpuuzi kama wapuuzi wengine walivyo.
Huyo Gambo na wenzake akina Sabaya na Mnyeti, walikuwa wakifanya ubabe katika utawala wa awamu ya 5, chini ya Mwendazake.

Hivi Sasa keshajisahau kuwa utawala huu, chini ya Rais Samia, mambo mengi Anayabadilisha, Kwa hiyo hivi Sasa ameanza kuweweseka!😎
 
Kwamba Lema ni "guarantee kuwa ni mgombea wa ubunge Arusha kupitia Chadema"??

Yaani hata Wana chadema wengine hamuwapi nafasi ?.....

Na kwamba wewe mwana JF unashabikia hizi siasa za kumilikisha watu majimbo hata kama hawajapitishwa bado rasmi?
Kuna sehemu mtoa hoja kasema kuwa Lema kawa guranteed kuwa mgombea wa ubunge Arusha kupitia Chadema?
 
Kwamba Lema ni "guarantee kuwa ni mgombea wa ubunge Arusha kupitia Chadema"??

Yaani hata Wana chadema wengine hamuwapi nafasi ?.....

Na kwamba wewe mwana JF unashabikia hizi siasa za kumilikisha watu majimbo hata kama hawajapitishwa bado rasmi?
Kwanini usimuulize haya maswali yako Mrisho Gambo ?
 
Kuna clip Moja inazunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha Mbunge wa Arusha mjini, Kwa tiketi ya CCM, Mrosho Gambo, alimkashifu Sana Mbunge wa zamani wa jumbo hilo...
Mrisho Gambo alipewa ubunge wa bure na Magufuli , sasa amerukwa na akili baada ya kujua kwamba hana tena nafasi, maana siasa za kubebana zimezikwa pamoja na jiwe
 
Back
Top Bottom