Mrisho Gambo: Vyeti Feki walipwe, Serikali ilikurupuka!

Mrisho Gambo: Vyeti Feki walipwe, Serikali ilikurupuka!

Angeondoa wafanyakazi hewa na sio wa vyeti.wa vyeti wengi walisoma zamani za uhaba wa shule.
 
Unaweza forge cheti taaluma huwezi foji.
Unaweza endesha gari au kuwa daktari kwa cheti tu pasipo kukaa darasani
Wao hiyo taaluma waliipata wapi?
Yaan daktari anaweza kua na taaluma ya udaktari bila kua na cheti?
 
Mbona Majeshini akugusa akuondoa hao wa vyeti na Kazi zinafanyika tu.
Aliwakomoa watu lengo kumridhisha bashite baada ya kunangwa hana vyeti.
 
Nchi ya wajinga hii hadi raha, kwamba mna hamasisha watu wasiende shule bali wakafoji vyeti wapate ajira, sio tu ajira tunaenda kutengeneza taifa la watu mbumbu, hivi tuna furahia ujinga huu kweli?
Upinzani nchi hii ni kapu la mwendawazimu yaani wanaweza hata kubisha kua hawavuti oxygen kisa tu wasionekane wapo sawa na chama tawala.
 
Walipewa.unamfukuza vipi professor aliyekaa darasa na akahitimu vizuri kisa tu eti cheti cha form jina limekosewa au sio lake.
Alifikaje kwenye uprofessa kama jina la kwenye cheti cha form four sio lake?
 
Wao hiyo taaluma waliipata wapi?
Yaan daktari anaweza kua na taaluma ya udaktari bila kua na cheti?
Udaktari ,ualimu ni taaluma kama alikaa darasani hata kama cheti sio chake.Cheti si chake bali taaluma ni yake.Thus walienda sekta binafsi wengine botswana,kenya,ulaya nk zingine wanafanya Kazi nzuri tu hadi wengine wakashukuru kupigwa chura.Ukuona madereva vyeti walivyosababisha Sana ajali tumepoteza watumishi wengi kwenye ajali sababu ya madereva vyeti.
 
Kazi nzuri sana Gambo, hayo ndiyo mambo tunayotaka kusikia.

Wenye vyeti feki pamoja na makosa yao lakini kazi walifanya, jasho lao limo mle kwa hiyo on humanitarian grounds ni vizuri serikali iwafikirie!
 
Alifikaje kwenye uprofessa kama jina la kwenye cheti cha form four sio lake?
Zamani shule za sekondari zilikuwa chache kupata kuchaguliwa wapo watu walirudia hata mara 7 na sio hawakuwa na akili bali nafasi chache wapo waliopata nafasi lakini wazazi hawana uwezo wa kuwalipia,au amefariki ,ndugu mwenye kiu ya elimu alitumia jina lake kusonga ngazi zingine za elimu.Thus taaluma ni yake u profesa ni wake lkn jina sio lake.
 
Pole mwendazake kumbe alikuwa hana rafiki ...ila uoga nao unakasumba tena unauzandiki
 
Back
Top Bottom