Msaada: Baba yangu mzazi ameuza nyumba yake na hataki kunipatia pesa japo kidogo

Hata ningekua mimi ndo babaako laki mbili ulio itafuta wewe umeenda kuipiga kiberiti eti unafurahia maisha je nikikupa hii nyingi ambayo hujaitafuta utaifanyia nini tena mzee aipanguse hiyo hela yote kabla ata hajafa aimalize yote akili yako ndogo sana hujui thamani ya pesa wewe. A kwa miaka 40 bado unajiita kijana tena upo nyumbani. Ningemjua mzee ningemwambia akutimue hapo nyumbani kabisa.
 
mimi ni kijana wa umri wa miaka 41
Kwa miaka hii kugonga 41, ni kumshukuru Mwenyezi Mungu! Angalau na wewe umekula kachumvi kidogo japo sio sana!
akiuza ntapata pesa na mimi ya kuanzia maisha,
WHAAAAAAAAAAT?! Kuanza maisha?
uwezi amini nilifurahi sana sana nilikuwa na bajeti yangu ya laki 2 na elfu 70 kwa furaha nzima iyo ela niliitumia kwa kufurahia maana nilijua kabisa nimesha kula maisha.
Hapo ulichukua uamuzi wa busara sana kama "kijana" wa miaka 41!
baba baada ya kupokea pesa ataki ata kunishirikisha kwa chochote,
Ulimchangia shilingi ngapi wakati anajenga?!
hajanipa ata sent kumi yake kwenye iyo ela
Ulitaka akupe pesa ya begi la shule au school fee?
, baada ya siku mbili kupita mzee akiwa kimya ikabidi nimuambie baba vipi kuhusu ela ya mauzo ya nyumba unioni mwanao na mimi nikaangalie maisha yangu mbele ya safari,
Ebo!! Ina maana ulikuwa unaishi hapo hapo nyumbani, au?
baba amenijibu tu kwa wepesi kabisa eti "SAWA NENDA KAANGALIE MAISHA TU, NAKUTAKIA KILA LENYE HERI"
Hakika baba yako ana roho mzuri sana. Ni lipi lililo jema kwa mzazi zaidi ya kumtakia heri mwanawe kijana wa miaka 41. Miaka 41 inakuwa umeshaingia phase two ya kuelekea kufa, kwahiyo heri kutoka kwa baba ni muhimu sana ili uweze kuishi angalau miaka mingine 20!
nikamuambia baba naendaje kuangalia maisha wakati ujanipa chochote, akaniambia kwani nadai nini kwake, kwa kweli ni kauli zilizo nivunja sana moyo na kunikatisha kabisa tamaa ya kuishi.
Unaona sasa! Kumbe jeuri! Yaani badala ya kumjibu unamdai nini, inaelekea ukapiga kimya!
Nani alikudanganya kwamba kuna sheria za kipuuzi kama hizo?! Cha babako ni chako siku akifa na sio wakati yupo! Kubwa jinga wewe.
 
We usimwambie hivi huyu kijana wa makamo anaonyesha ana msongo wa mawazo anaeza fanya tukio kweli huyu oooho
 
Ni mali ya baba yangu ila mimi ni mtoto wa wake kabisa kabisa wa kumzaa
Kuna watoto wa kuzaa wengine wa kutapikwa???😂
Nimecheka Sana hii mada, vijana miaka 40+, tutashikishwa ukuta, Kwa akili hii.

Everyday is Saturday..........................................😎
 
We usimwambie hivi huyu kijana wa makamo anaonyesha ana msongo wa mawazo anaeza fanya tukio kweli huyu oooho
🤣🤣🤣🤣🤣 Ila kweli. Dah sasa besty ukipata mtaji kama huu kule kwa muhindi sii utaweza mfilisi jamani
 
Nimecheka sana leo, Nyumba inajengwa bado upo nyumbani hadi inauzwa bado upo home na unataka mgao, Asante kwa kutufurahisha ....
 
Ndio maana baba yako hajakupa hela, Huna mausiano mazuri na pesa
 
hiyo ni nyumba yake, usimpangie, jenga na wewe yako uza hakuna atakayekupangia,
amekuzaa, amekulea hadi ukafika umri huo, amekusomesha kwa uzembe au jitihada zako umefikia kiwango hicho cha Elimu. Mshukuru
 
Na anahitaji sana maombi ya kukemea roho ya kumuua Baba yake, umeona anasema hasira aliyonayo hawezi kumwangalia Mzazi wake?
Huyo mzee naye siyo legelege, na hivyo anamngojea kwa hamu ambutulie mbali huko
 
Ni mali ya baba yangu ila mimi ni mtoto wa wake kabisa kabisa wa kumzaa
Kweli Bora umelileta Jambo hili hapa. Utapata ushauri na misemo ya kukuvunja nguvu na kukuinua pia. Mm nataka kukwambia kuwa Vijana wengi WA miaka hii hufikiria kuwa Mali za Baba au mama ni zao. Huwa hawajui kuwa Baba zao hawakupewa Mali na baba zao yaani Babu yako. Sasa ikiwa Mzee ameamua hakupi chochote basi usubiri urithi Tu maana hyo ndo Haki yako.
 
Yaani miaka 41 bado unamtegemea Mzee wako ndo akupe maisha hata ukipewa zote hizo ndani ya miezi 3 zimekwisha.Kama uliweza tafuna 270000 kwa siku tatu wakati huo ni mtaji tosha
Kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa mtoa mada. Wazazi tunatakiwa kuwajengea watoto wetu uwezo wa kujitegemea siku za baadaye kupitia elimu bora na pia kuwaelimisha kuhusu umiliki wa mali. Kwenye hii mada, baba na mtoto wake wote kwa pamoja wanahusika kwa hii sintofahamu.

Binafsi najitahidi kuwaambia vijana wangu kusoma kwa bidii kupitia mamilioni ya shilingi kwa mwaka kama ada zao za shule, kwa sababu hiyo elimu ndiyo urithi wao wa baadaye! Na kamwe wasizifikirie mali zangu ambazo nazitafuta kwa shida.

Ukimjaza mtoto aina hii ya maneno, na ukiwekeza kwenye kumpatia elimu bora! Kamwe hawezi kubweteka kama mtoa mada! Unless awe na kichwa kibovu. Inasikitisha katikaa umri wake huo, mtoa mada bado anaota kupata mgao wa mali kutoka kwa baba yake, na ambaye bado yuko hai.
 
Nenda kamshtaki mahakamani, kakuhujumu, mfungulie shtaka la uhujumu uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…