Msaada: Baba yangu mzazi ameuza nyumba yake na hataki kunipatia pesa japo kidogo

Hiyo nyumba ni yake na mkewe period. Wewe kajenge yako uuze. Wewe hukusiki wala hukuchangia chochote alaa.
 
Mleta mada hupaswi kulalamika hata chembe.
Ninachoweza kukushauri kukupa connection uende Mombasa utapewa pesa unayotaka zaidi ya hiyo baba yako aliyopata baada ya kuuza nyumba yake.
 
pole sana mkuu nakushauri kubaliana na mawazo yake mzee cha msingi upambane ujitafutie cha kwako.

Hapo huenda hakuwa na maelewano mazuri na Mama yako na huenda na wewe unamsikiliza Mama kuliko yeye... lakini huu ni mtazamo wangu tuu.
 
Hiyo laki 2 uliyotumia ingetosha hata kukurudisha kijijini, fikiria miaka 20 mbeleni mwanao naye atataka umgawie mali je utampa nini? Stuka usingizini
 
Dah! Ukachoma zaidi ya 200k kufurahia pesa ambayo hauna uhakika nayo?

Sasa umpelekeka mzee mahakamani kwani unamdai kitu gani? Ingekua amefariki ungestahili mirathi.

Mie nilivyomaliza kidato cha sita nikaanza maisha sikuwahi kuomba hata kijiko kutoka kwa Mzee.

Usipobadili mtizamo kuhusu maisha, utalaumu watu sana mkuu
 
Nimecheka kinoma yani huyo mshua mimi kabisa miaka kadhaa mbele
 
nyumba ni yetu, maana nimezaliwa hapo hapo
Una share ngapi kwenye hiyo nyumba? Kuzaliwa humo hai-justify your ownership. Ninyi ndio hamkawii kuwauwa wazazi wenu kwa sababu ya mali zao; ref. lile jinga la Arusha lililomuua mama yake mzazi.
 
Kwani Sasa hivi mnaishi wapi na nyumba imeuzwa? Baba yako hajakupa hata cha udalali? Alikusomesha? Alisha Kupa mtaji? Kwenye urithi atakwambia subiri afe.Cha msingi ongea naye akikaza jaribu kuwashirikisha wazee wenzie.
 
unakaa hapo kwenu kama mfugo miaka 41 πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
nyumba ni yetu, maana nimezaliwa hapo hapo
Kwakuwa hukuchangia tofari wala bati hiyo nyumba ni ya baba yako.Una haki kupata share akikurithisha au kwa mujibu wa sheria Ila kwakuwa bado yuko hai,huwezi kumlazimisha.
 
Yaani wewe mzee alikubeba sana mpaka unamaliza form 6.
Mie Mzee mpaka namaliza Form IV jukumu lake lilikuwa ni Ada tu...
Mavazi na vikorokoro vingine utajijua mweneywe...
Baada ya Form nilijua nitaaendelea na Elimu na nililima ekari 6 za mahindi nikavuna gunia 50. Hela ya kukodi shamba iliyotokana na kupiga picha maana nilifanyaga vibarua wakati wa likizo nikanunua camera YASHICA Gunia hizo ndio nikasoma Diploma ya Ufundi Umeme. Hapo ada plus pesa ya Field nikajisomesha mpaka namaliza. Tayari nimekuwa fundi unataka nini tena. Nimejiendeleza... yaani haya maisha sometimes ukiona Mzee anakukataa ndio anakupa akili.
 
Hiyo nyumba baba yako alipewa na babu yako? Tafuta vya kwako na yeye Kaiza mali yake
 
Alitegemea nyumba ya urithi apige bei
 
Kitambo sana darasa la nne au tano kama sikosei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…