Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Wakuu,

Nilishawahi kuleta uzi wa kutojua kupika way back Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?
Jioni hii nimepika wali...nauangalia hapa naona aibu mimi...wali una mafuta huoo

Nilianza kujua kupika lakini sjui nimesahau ama ni vipi lakini kila nikipika naharibu 🙌

Nisaidieni tips za kujua kupika vizuri...

Aaliyyah
Mwachiluwi
Sis Carleen

Bro Evelyn Salt nisaidie braza
Pole dadaangu
Kuwa na amani kilakitu ni process utajua Carleen njoo huku
 
Yaan nawaza tu wanaume wa humu walivyo na mdomo mrefu,utakuwa ukiwakosea tu kwenye comments watakuwa wanakujibu "ndiyo maana hujui kupika wali"
Ungeomba msaada hata Twitter 🥴

Nishajuta kuweka uzi mbona 😂😂
Sema nawamudu hao mapimbi watakaonijia juu
 
Bibie Joanah Mimi nikikuoa hata kama hujui kupika sikupi talaka lakini wanaume wengine watakupa, ukishajua kunitengea kile kitu mtima wangu unapenda kwa ustadi wa hali ya juu inatosha.
 
Aiseee,baada ya hv karibun kurud jikon,nimeelewa ni kwanini wanawake wengi hawapendi kununua na kupika mchele mkuu kuu

Mchele mkuu kuu kama ulikuwa unakuwaga wa mwisho mwisho darasani kamwe hautaweza upika maisha yako yote
 
Nitajitahidi kupika nikiweza manake muda wa kupika mixer uvivu 🙌
Sema kupika ukiwa mvivu inakua mtihani kumaster 😂😂😂... Na uombee uwe na mtu wa kukuoshea vyombo maana kupika ni jambo moja ila kuosha vyombo ni jambo lingine.
 
Back
Top Bottom