Msaada: Dogo janja anaimbaga nini? Sijawahi kumuelewa

Msaada: Dogo janja anaimbaga nini? Sijawahi kumuelewa

Watanzania tunapenda kujipa magonjwa na visukari kwa kuhangaishwa na mambo yasiyokuwa na tija...!!!

Hii Ina wasanii kibao wanaoimba miziki ya aina mbali....maana yake ni wewe kufuatilia za unayempenda na kuachana na wengine ambao huvutiwi na nyimbo zao!!!!
 
Mi pia sijui anachokiimba ingawa nyimbo zake kama ngarenaro..tumetoka mbali na wayuwayu ndio nyimbo pendwa kwenye kitochi changu
 
Huyu mwanamuziki nimetokea kumfahamu pale alipofunga ndoa na binti mrembo Irene Uwoya, sasa nikaanza kusikiliza nyimbo zake.

Wajuvi wa mambo mnisaidie huyu huwa anaimba muziki wa aina gani?

Na hualikwa kwenye matamasha ama concert/show na watu wanalipa viingilio? Au anafanya hisani (bure).

Natanguliza shukrani.
Navyoona mimi ni kama umeandika hivi

UZI:
Msaada: Jay z anaimbaga nini? Sijawahi kumuelewa

Huyu mwanamuziki nimetokea kumfahamu pale alipofunga ndoa na binti mrembo Beyonce Knowles , sasa nikaanza kusikiliza nyimbo zake.

Wajuvi wa mambo mnisaidie huyu huwa anaimba muziki wa aina gani?

Na hualikwa kwenye matamasha ama concert/show na watu wanalipa viingilio? Au anafanya hisani (bure).


Yaani kitendo tu cha kutomjua hadi anaoa wewe si mshabiki wa bongo flavor utakuwa muimba kwaya kanisa la kisabato ,hata mimi masuperstaa wa nyimbo za kisabato simjui hata mmoja zaidi ya ile bendi ya Rwanda ila nawaheshimu na najua duniani siwezi jua kila kitu

USHAHIDI : Angalia comment nyingi zinakushangaa wewe
 
Naaam umemenisaidia kuelezea paragraph kumi kwa mstali mmoja ,ni sawa na mimi nimuhoji jamaa ''Hivi Rais wa Madagascar mbona simuelewi ?'' its simple hanihusu
Ni ukichaa kufafanisha Celebrity wa kimataifa na mpiga kelele mariooo
 
eti anaimba "Putururu" mi mwenyewe simuelewi kabisa basi tu wananchi wanamuonea huruma sababu ni mtoto ili asijiingize kwenye madawa and the likes
 
Hua anaimba......maujingaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!ujingaaaaa!!!!!!
 
HUU NI WIVU ULIOPITILIZA,
TAMBUA HII NDIO STYLE YAKE YA KUPATA PESA, CHA AJABU AKIKUOMBA HATA BUKU HUWEZI KUMPA... NA WEWE SIJUI HATA UNAANDIKAGA NINI
 
Ndugu sina chuki dhidi yake, ni katika kutaka kujua wanamuziki na muziki hapa nchini Tanzania. So far nauelewa zaidi Muziki wa Diamond, Harmonize, Ally Kiba, Ben Pol ILA BADO NAJILAZIMISHA kuwaelewa JUX, VANESSA, DOGO JANJA na ROMA.
Hata Roma humuelewi basi umelogwa wew
 
Ukiona humuelewi huenda ni tatizo lako kama ambavyo ulikua unashindwa kuelewa hesabu shuleni
 
Anafanya vizuri, ni uhater tu unakusumbua dada
 
Huyu dogo hakuja mwenyewe dsm, wanaojua mziki walimfuata kwao Ngarenaro wakamwambia twende bongo tukatengeneze pesa. Sasa wewe kama humuelewi basi ujue hakuletwa kwa ajili yako
 
Back
Top Bottom