Msaada: Familia inahangaika namna gani watawasadia watoto wawili wa nje wa marehemu

Ndugu wa marehemu ndo "hamna akili"...yaani aende mahakama kudai nini?

Nyinyi watoto wawili mnashindwa kuchangishana mkawalea?

Hivi marehemu angekufa Hana kitu mngeshauri mama WA hao watoto aende wapi kudai nini??
 
Ndugu wa marehemu ndo "hamna akili"...yaani aende mahakama kudai nini?

Nyinyi watoto wawili mnashindwa kuchangishana mkawalea?

Hivi marehemu angekufa Hana kitu mngeshauri mama WA hao watoto aende wapi kudai nini??
We subiri. Hawa hawa, watamwambia ngoja usiondoke tuone itakavyokuwa, huku na wao wanamgegeda. Badae wamwambie we rudi tu tutatafutana. Mwanamke kama huyo japo nae ana ujinga wake, lakini ukatili atakaokuwa nao, atakaejichanganya kumgonga atajuta
 
Mmajuaje Mali ni za marehemu? What if ni Mali za mwanamke na zimeandikwa jina lake? Maana kama hazikua kwenye jina la huyo mwanaume hawapati chochote. Labda mafao ndo wanaweza kupata na iwe vyeti vya kuzaliwa vinaonesba jina la baba? Maana inawezekana mama hakutumia majina ya mwanaume kwenye vyeti vya kuzaliwa Kwa uoga
 
Yani mtu tayar anawatoto wawili nyumba 1 na biashara ndogo tu wanataka kumuongezea watu 3 tena kisa ujinga wa ndugu yao
Ndugu wa marehemu ndo "hamna akili"...yaani aende mahakama kudai nini?

Nyinyi watoto wawili mnashindwa kuchangishana mkawalea?

Hivi marehemu angekufa Hana kitu mngeshauri mama WA hao watoto aende wapi kudai nini??
 
Poleni mkuu. Haya mambo yanahitaji busara kuliko kukomoa/kutumia nguvu. Japo ni nadra sana wanasema pesa ni shetani. Wazee wa ukoo waitishe kikao liongelewe hilo swala kwa sababu ngazi ya kuanzia ndio hiyo. Muafaka utapatikana, watoto wapate haki zao za msingi. Mimi imewahi kunitokea, mama alifariki 2017, lakini walikuwa hawajafunga ndoa wala taratibu zozote kama ilivyo desturi, yaani, in short, wasomi walikutana mjini wakaendeleza maisha, ndio kuzaliwa mimi Marangu Village. Hahaha... Tuendelee sasa.

Kipindi tupo kwenye vikao vya ukoo, wajomba wakaleta noma kweli, yani wadogo zake maza (alikuwa first born) wakata wakamzike dada yao kwao kwa sababu hawamtambui baba yangu, kwa sababu hakuwahi kuenda kujitambulisha ukweni. So wakaweka ngumu sana, mzee nae akakomaa, akataka amzike mkewe, ilikuwa mbaya mbaya. Kufupisha story, mzee mimi alitumia trick, akanipanga nikawaombe wajomba ruksa ya kumzika mama yangu, nikafanya hivyo pamoja na mila nyingine zilifuata, nikamzika mama nyumbani sasa kwa mzee. Leo hii mzee hatupo naye, lakini nashukuru Mungu na najivunia, nawahudumia wajomba zangu kwa kiasi chake. Si mnajua tena maisha ya vijijini, bila kuwapa sapoti, hawasogei. Walinijali na mimi nikarudisha fadhila, so busara itumike kumaliza huo mgogoro mkuu. Kila la kheri, mkuu.
 
watoto wa nje ndoa wana haki sawaa na watoto waliozaliwa ndani ya ndoa
Hapa ndiyo utaona tofauti ya sheria za kidini na serikali, mtoto wa nje ana haki ya kurithi mali ya baba yake ili mradi tu ajulikane ni mtoto wa marehemu! Na siyo mpaka D.N.A kikao cha ndugu kikiridhia tu inatosha!

Lengo ni kuwalinda hawa watoto kwani hawana hatia yoyote!

Halafu mtu anakuambia sheria za kidini katunga Mungu!
 
Hao watoto wana haki ya kurithi ila mama yao ndio hatapewa kitu sana sana atakuwa msimamizi wa hiyo share yao mpaka wawe wakubwa.
 
Ndugu wa marehemu ukoo wa mume ndio wanaweza kuwasaidia hao watoto
Kawaida mirathi ikifunguliwa na wao wanapewa
Msimamizi wa Mirathi asije kusahau hilo mirathi itasumbua

Mahakama zinawatambua watoto.wa nje kwenye Mirathi
 
Watoto waishi na mama yao wahudumiwe wakiwa kwa mama yao ila hii tabia kwenye msiba mnapeleka watoto ili iweje sasa
Wanaenda kumuaga na kumsindikiza mzazi wao kwenye safari ya mwisho duniani. Why wasiende kwenye Msiba wa mzazi wao?

Huu ubinafsi umezidi sasa
 
Mlyambina J anakuambia hakuna bastard children ila kuna Bastard Parents...
 
Sheria za dini ndio zinatambua watoto wote..... Ikiwa ndoa imefungwa hata mke azae nje mtoto yule anatambulika maana ndoa imeshafungwa.

Kuna procedures kuwapa haki zao watoto wa nje kisheria kabisa.
 
Nashkuru kuzaliwa Muislamu

Yani in islamic perspective ni suala dogo sana hilo

Watoto wa nje ya ndoa hawarithi kitu labda baba yao awape yy mwenyewe akiwa hai

Uzinzi haujawahi kumuacha mtu Salama
Kwamba watoto wamejizaa?? Akili zako hazina akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…