Hakuna watoto wa nje ya ndoa mkuu kwa mujibu wa sheria za nchi. Watoto wote ni sawa
Watoto wote ni sawa. Kiubinadam lakini.
Wakati mwingine, hasa kwa wanaume japo na wanawake wamo tu. Bora useme mapemaaa, watu wakae wakijua. Japo mijanamke mingine ina roho mbaya ikiletewa mtoto wa nje inaweza mdhulu au wengine huwanyanyasa.
Lakini,we pia fikilia. Mwanamke anaejiita wako wa ndoa, kakupa sumu ili uondoke apumue, huenda ana kishikaji furani anataka kiwe kinagegeda. Hapo kufa kwako ataona raha. Hapo hapo unaanza msara wa mshua alikuwa na watoto 3 nje, na kila mtoto alikuwa na mama yake.
Haya, mawaza yanapanda kichwani. Kumbe alikua dunga dunga! Je, mimi si mtamu kumbe? Hapo anaanza kufichaficha mali, hapo wengine wanapanga afukuzwe zibaki wagawane, na madogo huenda wasipate haki yao.
Sawa,qanaume ni wazinzi. Ila, uzinzi wao unatokana na wanaojiita wake zao kwa asilimia kubwa.
Ni janga kama majanga mengine. Kuna wanawake wengine na wenyewe vilaza. Umezaa na mtu,mme wa mtu. Unapolenga kwamba akifa atarithi na yeye, mtoto huyo hajulikani, unategemea nini? Na ukitangulia? Si ndo anaenda kuwa chokolaa kabisa! Wa kike anajiuza? Pamoja na kwamba wapo walioshindikana, malezi, tabia, na mengine mengi,ila pia wapo ambao hawajui wametokea wapi. Hao si mzigo katika jamii? Haya,jiulize na wao wakizaa!
Kama mwanaume anataka umzalie,na wewe umelidhia,ongeeni muwekane sawa,hiyo mimba na mtoto watambulike.