Msaada: Familia inahangaika namna gani watawasadia watoto wawili wa nje wa marehemu

Hakuna biashara ya familia.
Baba kaacha nyumba tuu aliyojenga na mkewe na duka la madawa ya binadamu ila nimesikia ni la mkewe maana mkewe kasoma madawa
Hilo duka ndo chanzo cha kipato, na hilo duka si la mkewe ni la familia
 
Familia ya nani???

Wewe mkeo akiwa na shemeji yako akiwa na duka limesajiliwa kwa jina lake utasema ni la familia mpk wewe unamgao hapo??
 
Nadhani kauli ni marehemu kaacha duka la dawa! na siyo marehemu kampa mkewe duka la dawa
 
Habari wa JF,

Kuna msiba wa ndugu mmoja jirani hapa. Sasa siku ya msiba walikuja watoto 2 wana umri wa miaka 5 na mama yao wanafanana sana na watoto mapacha wa kiume aliyozaa na mkewe wake ambao wana umri wa miaka 6. Ina maana jamaa alizaa nje watoto wamefanana na Baba yao ukiwaona ni kama watoto 2 wa ndani ya ndoa aliyezaa na mkewe.

Mkewe marehemu hajui nini cha kufanya hapo msiba ushaisha mpaka sasa. Familia wanajua hao watoto wanahitajika kutuzwa na kuishi. Marehemu kaacha nyumba moja aliyokuwa anaishi na mkewe na gari moja Toyota ICT na duka la madawa ya binadamu aliyokuwa anasimia mkewe, pesa za benk sijajua.

Sasa familia imeingia na kiwewe kuhusu hawa watoto 2 wa nje maana ni watoto wa ndugu yao kabisa. Kuna mtu mmoja amesema kama mama wa hao watoto anatafuta kusaidiwa malezi ya watoto aende ustawi wa jamii au akafungue shauri mahakamani, sasa inawezekana hio kweli.

Vipi kuhusu hapo watoto nani awapokee na ni nani awahudumie? Mke wa marehemu yeye ana kazi yake japo ni ya kawaida. Msaada jamani.
Ndiyo shida ya kuzaa nje ya ndoa.
 
Hapa hutapata unachokitaka maana hapa kuna wazaa na wanaume za watu,kuna wanaume Malaya kuna wanawake na familia zao kiufupi hamtoelewana.

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Nashkuru kuzaliwa Muislamu.

Yani in islamic perspective ni suala dogo sana hilo.

Watoto wa nje ya ndoa hawarithi kitu labda baba yao awape yy mwenyewe akiwa hai.

Uzinzi haujawahi kumuacha mtu Salama.
Ujinga ujinga tu wa mapokeo
 
Wamama nao waangalie maana wakishabaki peke yao uwezo wa kutunza Mali unakuwa robo.
 
Habari wa JF,

Kuna msiba wa ndugu mmoja jirani hapa. Sasa siku ya msiba walikuja watoto 2 wana umri wa miaka 5 na mama yao wanafanana sana na watoto mapacha wa kiume aliyozaa na mkewe wake ambao wana umri wa miaka 6. Ina maana jamaa alizaa nje watoto wamefanana na Baba yao ukiwaona ni kama watoto 2 wa ndani ya ndoa aliyezaa na mkewe.

Mkewe marehemu hajui nini cha kufanya hapo msiba ushaisha mpaka sasa. Familia wanajua hao watoto wanahitajika kutuzwa na kuishi. Marehemu kaacha nyumba moja aliyokuwa anaishi na mkewe na gari moja Toyota ICT na duka la madawa ya binadamu aliyokuwa anasimia mkewe, pesa za benk sijajua.

Sasa familia imeingia na kiwewe kuhusu hawa watoto 2 wa nje maana ni watoto wa ndugu yao kabisa. Kuna mtu mmoja amesema kama mama wa hao watoto anatafuta kusaidiwa malezi ya watoto aende ustawi wa jamii au akafungue shauri mahakamani, sasa inawezekana hio kweli.

Vipi kuhusu hapo watoto nani awapokee na ni nani awahudumie? Mke wa marehemu yeye ana kazi yake japo ni ya kawaida. Msaada jamani.
Mbona hakuna cha kurithi mkuu
 
Back
Top Bottom