Msaada: Kibaka/bodaboda ameniibia simu yangu asubuhi hii

Msaada: Kibaka/bodaboda ameniibia simu yangu asubuhi hii

Mkuu, haraka sana wasiliana na mtandao uliokua unautumia ili waweze kufunga hizo line zako. Niliwahi kuibiwa halafu wezi wakaanza kuwatumia message watu kwa simu yangu wakiomba hela kuwa nimepatwa na dharula. Hii ifanye haraka sana
hilo limefanyika tayari, na line zangu pia huwa zina PIN muda wote
 
Pole sana.

Mkasa huo ulishawahi nikuta Buguruni sokoni kabla ujenzi wa BRT haujaanza.

Nilikuwa namaliza kuongea na simu kabla ya kuvuka barabara jamaa wawili kwenye boda wakanikwapua.
Nashuru Mungu alikuwa upande wangu maana kulikuwa na daladala inakuja mbele ya bodaboda na wakaishia kuivaa daladala uso kwa uso.

Dereva wa boda aliumia sana ila yule mkwapuaji alipata michubuko tu. Simu yangu niliipata na pesa juu maana tulienda Buguruni polisi na nikaandikisha walinikwapua na pesa pia. Yule jamaa alikutwa na laki na 10. Niliambulia 80 elfu na askari alichukua 30.
 
Neenda Kwa Nabii au Mataalam,au kama unaiman ya kiislam nenda kwa sheikh
 
Potezea tuu, hakuna msaada wowote utakaopata zaidi ya kupoteza muda na fedha
 
Nilikuwa pale mnazi mmoja(Dar) nikawa narequest Bolt ili niwahi mzigoni, bodaboda akapita kama mshale akapokonya simu.

Inaonekana alishaona kuwa pale karibu hamna bodaboda mwingine amesimama muda ule ndio maana hata nikashindwa kumkimbiza, watu waliokuwa arround waliona ila hawakuwa na msaada zaidi ya kupiga kelele za mwizi ila ndio hivyo alikuwa speed.

Simu ni mpya, mwenye Idea nini cha kufanya tafadhali
Atakuwa adriz na hydroxo
 
Pole sana kwa hayo matatizo yaliyokukuta Tafuta nyuki awe mzima mtie katika kijichupa kisha funika nitafute mimi kwa wakati wako uje nae huyo nyuki nipate kumshughulikia ili aweze kuirudisha simu yako. Nyuki atakwenda kumtafuna na wenzake wengi watajenga mzinga kichwani mwake mpaka arudishe simu yako.
Ila Herbalist Dr MziziMkavu 😁😁😹
Hakuna kinachoshindikana kwako.
 
Iliwahi kunitokea kitu mwaka 2015 barabara ya kutokea Coco beach kuelekea Chole Road.

Nilikuwa nimeweka ear phone huku nikisikiliza wimbo kwenye simu nikiwa nimeishika mkononi.

Wakaja hao vishandu wawili(anayeendesha na aliyebebwa)

Aliyebebwa alishuka fast waliponikaribia kwa nyuma ili aje akwapue simu.

Alipojaribu kuikwapua akaikosa kidogo simu ikaniponyoka na kudonda chini mbele yangu. Nikataharuki na kuiokota chap(ikawa pona yangu) huku yeye akakimbilia kupanda Boda na kukimbia.

Nikajaribu kutafuta jiwe niwarushie ikawa too late.

Tangu siku hiyo nikawa makini sana nikiwa barabarani hasa mjini Daslam.
 
Pole sana kwa hayo matatizo yaliyokukuta Tafuta nyuki awe mzima mtie katika kijichupa kisha funika nitafute mimi kwa wakati wako uje nae huyo nyuki nipate kumshughulikia ili aweze kuirudisha simu yako. Nyuki atakwenda kumtafuna na wenzake wengi watajenga mzinga kichwani mwake mpaka arudishe simu yako.
Mzee wewe si upo abroad, atakutafutaje sasa[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Akili zako ndogo sana, kuingia Jamii Forum lazima simu? Au hujui kwamba kuna computer, umeshindwa kusoma hapo kwamba nilikuwa naenda kazini
Mbona unaomba ushauri kwakufoka? Au ndio yeye alipita nayo? Au kagusa kidonda kibichi
 
Pole sana mkuu!
Kuna stori nyingi kwamba smartphone ikiibiwa ni rahisi kuipata.
Ila uhalisia ni tofauti kidogo.

Kuna kimeo natumia hapa samsung j6 kama hautajali nikuazime, japo haikai na chaji ukinunua utanirudishia.
 
Pole sana mkuu!
Kuna stori nyingi kwamba smartphone ikiibiwa ni rahisi kuipata.
Ila uhalisia ni tofauti kidogo.

Kuna kimeo natumia hapa samsung j6 kama hautajali nikuazime, japo haikai na chaji ukinunua utanirudishia.
Thanks bro, imebidi nikope hela sehemu nivute nyingine maana simu inanisaidia sana kwa kazi zangu.
 
Malipo ni baada ya kazi..
Unatakiwa ulipe kwanza nusu na ukafanyiwa simu ikirudi usipo maliza pesa yako nyuki atakurudia wewe kukumaliza kama alivyomaliza mwizi.


View attachment 3063450
Ila Herbalist Dr MziziMkavu 😁😁😹
Hakuna kinachoshindikana kwako.
Hakuna kitu kinacho shindikana isipokuwa ni kifo alichokuandikia Mungu hakina kinga vilivyo bakia vyote vina dawa zake. Akitaka nimrudishe mwizi aliyeiba simu yake nitaweza ili mradi alipe gharama zangu nitakazo mwambia. nitamtumia mwizi nyuki wengi waende kumkamata mwizi na kumleta kwa mtu aliyeibiwa na kuipata simu yake. Na pia kuna Dawa ya kinga ya Sumu ukiwekewa katika chakula au kiti cha kukalia au katika maji hutoweza kuyanywa hayo maji na Chakula kitakukataa utanusurika na hiyo Sumu uliıyotegewa. Na kinga ya Risasi ukipigwa risasi haitoweza kukuingia mwilini mwako. Kinga ya majambazi wamekuzingira wanataka kukuchulia Pesa unapotea mbele ya macho yao kimaajabu na unajikuta upo sehemu salama. Hizo kinga zote zipo kwa anayehitaji ataniona Mimi Kwa Wakati wake.



COSTA KONGO DUA YA KUMKAMTA MWIZI AU KUMUHAMISHA MTU KATIKA NYUMBA KWA KUTUMIA NYUKI 1 KUMSOME...jpg
 
Back
Top Bottom