Msaada: Kichwa kinawaka moto kwa mawazo, nakosa usingizi

Msaada: Kichwa kinawaka moto kwa mawazo, nakosa usingizi

Nimekuwa nikipitia changamoto ya kukosa usingizi, kutaka kujiua toka mwaka 2018 nikiwa chuo baada nikaanza kunywa madawa ya usingizi zaidi ya aina 15 bila kupona, nimeenda sehemu za maombezi pia ila bado haiponi.

Mwaka 2020 nilipata mchumba ambae nae mwaka huu kaenda JKT nimejikuta ninaishi kwa mawazo sana, maana huyu mwanamke nilikuwa nampenda sana.

Kiufupi kwa sasa nimekosa direction, maana pamoja na kusoma sina kazi, sipati usingizi na kuna roho ya kutaka kujiua inanisumbua kila siku.

Naombeni msaada.
Dawa ya kwanza ni kukubali kuwa huna kazi na umesoma, hiyo ni changamoto kila. Mahali na lisikufanye kujiona unagundu.

Weka Mkakati wa kufuatilia kazi labda kujiajiri au kuajiriwa. Ila kama kuajiriwa, kwanza tafuta PA kujitolea update uzoefu na connection.

Kwa ufupi ukikaa bure bila jambo la kukufanya busy lazima utajua... Bse the idle mind is the devil workshop.

Nakushauri hata zege kabebe ili ukirudi umechoka mwili nalala kwa uchovu... Kila la kheri
 
Jifunze kuji keep busy muda wote..shughulisha mwili...zunguka hapo nyumbani angalia kitu ambacho akija kaa sawa kiweke sawa... Soma vitabu,vijarida au hata humu ingia..pitia majukwaa yote soma kitacho kupa furaha.... Fanya mazoezi.... Anza nza na kazi yoyote utakayo ipata huku ukiendelea kujitafuta.

Mtangulize Mungu mbele.....
 
Aisee chanzo kikubwa ni nini maan umesema toka uko chuo tafuta chanzo cha hayo mashida iyo roho ya kujiua unajiendekeza tu
 
Nimekuwa nikipitia changamoto ya kukosa usingizi, kutaka kujiua toka mwaka 2018 nikiwa chuo baada nikaanza kunywa madawa ya usingizi zaidi ya aina 15 bila kupona, nimeenda sehemu za maombezi pia ila bado haiponi.

Mwaka 2020 nilipata mchumba ambae nae mwaka huu kaenda JKT nimejikuta ninaishi kwa mawazo sana, maana huyu mwanamke nilikuwa nampenda sana.

Kiufupi kwa sasa nimekosa direction, maana pamoja na kusoma sina kazi, sipati usingizi na kuna roho ya kutaka kujiua inanisumbua kila siku.

Naombeni msaada.

Najua unavyo jisikia maana mpenzi alikuwa ndo faraja yako na kaenda huko uliposema jikaze mtoto wa kiume, ufe kwa sababu gani??

Kukosa usingizi kwa sisi wanaume kawaida tu sio ugonjwa huo mzee!!!! Acha kunywa madawa utapotea,

Usichague kazi mkuu kazi yoyote fanya ili mradi unapata riziki ya kula

KAZI NI KIPIMO CHA UTU
 
Nimekuwa nikipitia changamoto ya kukosa usingizi, kutaka kujiua toka mwaka 2018 nikiwa chuo baada nikaanza kunywa madawa ya usingizi zaidi ya aina 15 bila kupona, nimeenda sehemu za maombezi pia ila bado haiponi.

Mwaka 2020 nilipata mchumba ambae nae mwaka huu kaenda JKT nimejikuta ninaishi kwa mawazo sana, maana huyu mwanamke nilikuwa nampenda sana.

Kiufupi kwa sasa nimekosa direction, maana pamoja na kusoma sina kazi, sipati usingizi na kuna roho ya kutaka kujiua inanisumbua kila siku.

Naombeni msaada.
Shida nn
Kukosa kazi,mwanamke kuondoka?
Sijaelewa
 
Hii hali iliwai kunipata,nikawa sasa naboea kunywa tu ili nilale wapi kukesha ilikua kawaida tu.
Hamna kitu kibaya usiku sasa sita hiyo,7,8,9,10,11,12 sa moja we umekodoa tu.
Hujalala huku kazi inakungoja.
Ilikua inakra sana.
Ila kwasasa nalala mpk nalala tena
 
Piga chuma a.k.a nondo.
Tena tengeneza zile local, nyanyua sana.
Hyo tetesterone itabuild up na kukufanya ulale kama mtoto.
Ikishindikana, katia ka ganja kidogo (hakikisha ni dry na sio mixer).
 
An idle mind is the devil's kingdom,find something to keep u busy,cheza hata football za kitaa,mambo ya kukaa pekeako pekeako ndo unavutia mapepo kukupa mawazo mabaya,jichanganye hata kwaya?,maombi ya asbuh na jion makanisan ,

Sent from my FRD-L19 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom