Msaada kuhusu kusoma kwa Njia ya Masafa (Distance Learning)

Msaada kuhusu kusoma kwa Njia ya Masafa (Distance Learning)

clinician

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
2,098
Reaction score
4,926
Wakuu, nipo huku Mtwara ndani ndani,natamani kujiendeleza kielimu ngazi ya degree kwa kozi za Afya.
Naomba mnielekeze chuo kizuri cha nje ya nchi ambacho kinatoa elimu kwa njia ya masafa na kinachotambulika na TCU.

Napokea pia ushauri wa kozi nzuri za Afya ambazo mtu anaweza kusoma kwa njia ya masafa. Kozi iwe nzuri tu sio lazima iwe na soko sababu kazi tayari ninayo.

Mie nilikuwa napendelea Kozi ya Nutrition. Elimu yangu ni Afisa tabibu.

NB: OUT sio option kwangu sababu GPA yangu hainiruhusu kusoma hapo kozi nayotaka. Na sielewi kwanini kozi ya Nutrition imewekewa GPA kubwa hivi.
 
Hiyo Nutrition umeshafatilia scale zao lakini? Ziko chini sanaa. Angalia uendelee kwenye muundo wako huo huo wa udaktari.
Na vyuo vya nje kwa kozi unayotaka wewe ada ni kubwa sana.
 
Hiyo Nutrition umeshafatilia scale zao lakini? Ziko chini sanaa. Angalia uendelee kwenye muundo wako huo huo wa udaktari.
Na vyuo vya nje kwa kozi unayotaka wewe ada ni kubwa sana.
Mshahara sio tatizo kaka,kikubwa nacholenga ni ujuzi,Unashauri nisome nini?
 
Back
Top Bottom