Habari.
Nina mtoto wa miezi miwili. Kuna changamoto aliyonayo ya kutolala karibia usiku mzima yaani analala kimagepu huku akiwa hayuko comfortable.
Na akiwa macho hatulii na mama yake pia akimuweka kitandani hataki kukaa peke yake anaanza kulia. Akimpatia pia nyonyo muda mwingine anakataa muda mwingine ananyonya.
Hali hii inatokea pia na mchana.
Msaada kudhibiti hii hali kama umeshawahi kuipitia na mwanao.
Pole kwa shida anayopata mtoto.
Tatizo linalomkabili dogo ni gesi iliyozidi tumboni ambayo anaimeza wakati wa kunyonya maziwa, sababu kubwa inayosababisha mtoto ameze gesi nyingi wakati wa kunyonya ni poor positioning ya mtoto wakati wa kunyonya kiasi cha kusababisha gesi nyingi kuweza kupita mdomoni kwa mtoto na kumsababishia Hali hiyo uliyoelezea.
Cha kufanya
1.Achana na wazo la kumpa gripwater,au sijui maji ya uvuguvugu au chochote kile mbali na maziwa ya mama,kwani utazidisha tuu tatizo na sio nzuri kwa afya ya mtoto mchanga ambae anatakiwa apewe maziwa ya mama tuu kwa muda wa miezi sita ya kwanza ya maisha yake.
2. Hakikisha mama wa mtoto anam position vizuri mtoto wakati anamnyonyesha. Position ya mtoto ikiwa vibaya husababisha gesi kuingia mdomoni kwa mtoto wakati ananyonya na kumsababishia gesi. Angalia video ifuatayo ambayo inaonyesha jinsi ya kumshikilia mtoto vizuri wakati wa kunyonyesha.
View: https://www.youtube.com/watch?v=or4OnMxihUg
3.Kila baada ya mtoto kunyonya na kushiba,mama yake amcheulishe mtoto kwa kumbeba na kuegemeza tumbo la mtoto kwenye bega lake (mama), huku akimgusa mgongoni gently,fungua video ifuatayo kuona jinsi ya kumcheulisha mtoto baada ya kunyonya. Hii husaidia mtoto kutoa gesi ambayo inaweza kuwa iliingia wakati wa kunyonya.
View: https://www.youtube.com/watch?v=m50PTFmmlxw
4. Amfanyie mtoto massage inaitwa "I love you tummy massage" akiona mtoto analia na kujinyonga nyonga na hayuko comfortable. Cheki vide chini hapa kuona namna ya kufanya
View: https://www.youtube.com/watch?v=nUNzi9PYBwc
View: https://www.youtube.com/watch?v=xfGtACWT9ng
Ukifanya kwa usahihi massage hiyo, kama mtoto alikuwa na gesi tumboni,basi utaona anajamba na ataacha kujinyonga na atalala kwa amani kabisa.
Financial Analyst