Comments nyingi ni nzuri,
Bt umenikumbusha historia ya maisha yangu ya utoto,
Nilipokuwa na umri wa miaka 11 hv, tuliishia nyumba Moja ya kupanga, na mwenye nyumba wetu alikuwa wa Dini Ile, baba wa mama mwenye nyumba alikuwa sangoma, nyumba tuliyopanga sie alikuwa akiishi mwenye nyumba, alipohamia nyumba mpya mtaa wa pili, sie tulipangishwa nyumba hiyo.
Mdogo wangu wa mwisho akiwa na umri kama huo wa mwanao, alikuwa usiku halali, ni kulia usiku kucha, tumia dawa za gesi wapi, mchana analala vizuri tu,
Baada ya siku kadhaa kupita, my dad baada ya tafakuri ya kina, akapata wazo la kuifanyia Ujasusi nyumba ile, alianzia chini hakuona chochote, alipopanda juu ya Dari na kupiga search ya maana, alishuka Toka darini akiwa na kijimfuko cheusi kilichokuwa kimefungwa, baada ya kukifungua,ndani ya mfuko huo kulionekana vitu ambavyo sitavitaja hapa.
Mzee alivichukua na akavipiga moto.
Kuanzia siku Ile, dogo alilala Ule USINGIZI wa mtoto mchanga anatakiwa kulala.
Good morning!!