Msaada kuhusu mtoto kusumbua usiku kucha

Msaada kuhusu mtoto kusumbua usiku kucha

Gesi kuna wakati wamama huchoka sanaa aisee so unakuta anampa mtoto usiku nyonyo yeye analala mpaka mtoto ananyonya hewa tu.
1.nunua Grip water hii itamsaidia sana.
2.kama unahisi mambo ya uswahili usipewe dawa yoyote mkate tunywele kidogo kichwani mwake kisha hizo hizo nywele zake mfunge kichwani mwake.
3.Jitahidi kumbeba kwa kumweka begani kusaidia kutoa gesi.
Ahsante mkuu
 
Mwambie amfanyie tummy time
Anamweka kifuani pake alale hapo mpaka awe fofofo ndo amlaze kitandani
Kumbuka huyo kakaa tumboni miezi 9 na kule kuna joto tofauti na huku alipo sasa
So anapomueka kifuani anafeel safe then anatulia!
Ukitaka kujua kama ni gesi binya tumbo lake kama ni gumu sana mpe infacol kama si gumu usimpe dawa afanye tu hiyo tummy time utaona!
Nami ilimsaidia sana mwanangu now ana 10months
Ahsante mkuu
 
Duh mnanikumbusha kuna dogo nae alikua analia hivyo hivyo sasa huyu hata kunyonya hataki (Mtoto wa baba mdogo),kulala halali ucku kucha,ila mchana anauchapa vzr sn,bibi yake alisema mbadilisheni jina tu. Tangu limetekelezwa hilo hajawaji leta shida tena not sure why and what happened to previous name.
Inatokeaga hii
 
1. Hakikisha ananyonya na kushiba.
2. Mtoe gesi kwa kumbeba begani au mlaze kwenye mapaja kifudifudi baada ya kunyonya
3. Kwa vile hujui ni kiwango gani cha maziwa ananyonya kwenye ziwa. Ni vizuri nyakati za usiku umkamulie maziwa na umfanyie bottle feeding ambapo umnyweshe kulingana na umri wake.

4. Usimvalishe nguo za mpira au za joto hasa msimu wa joto.
5. Asikae na mikojo au kinyesi au uchafu. Kila akikojoa mbadilishe. Ikiwezekana usimvalishe Pampas kama anashinda nyumbani.

6. Kila baada ya siku moja aoge.

7. Mnyooshe viungo.
8. Angalau kwa siku umtoe nje akapigwe na upepo. Akilia.

9. Kabla hajanyonya maziwa hakikisha mamaake ameosha ziwa na maji masafi na kulifuta.
Ahsante mkuu
 
Pole kwa shida anayopata mtoto.

Tatizo linalomkabili dogo ni gesi iliyozidi tumboni ambayo anaimeza wakati wa kunyonya maziwa, sababu kubwa inayosababisha mtoto ameze gesi nyingi wakati wa kunyonya ni poor positioning ya mtoto wakati wa kunyonya kiasi cha kusababisha gesi nyingi kuweza kupita mdomoni kwa mtoto na kumsababishia Hali hiyo uliyoelezea.

Cha kufanya
1.Achana na wazo la kumpa gripwater,au sijui maji ya uvuguvugu au chochote kile mbali na maziwa ya mama,kwani utazidisha tuu tatizo na sio nzuri kwa afya ya mtoto mchanga ambae anatakiwa apewe maziwa ya mama tuu kwa muda wa miezi sita ya kwanza ya maisha yake.

2. Hakikisha mama wa mtoto anam position vizuri mtoto wakati anamnyonyesha. Position ya mtoto ikiwa vibaya husababisha gesi kuingia mdomoni kwa mtoto wakati ananyonya na kumsababishia gesi. Angalia video ifuatayo ambayo inaonyesha jinsi ya kumshikilia mtoto vizuri wakati wa kunyonyesha.

View: https://www.youtube.com/watch?v=or4OnMxihUg

3.Kila baada ya mtoto kunyonya na kushiba,mama yake amcheulishe mtoto kwa kumbeba na kuegemeza tumbo la mtoto kwenye bega lake (mama), huku akimgusa mgongoni gently,fungua video ifuatayo kuona jinsi ya kumcheulisha mtoto baada ya kunyonya. Hii husaidia mtoto kutoa gesi ambayo inaweza kuwa iliingia wakati wa kunyonya.

View: https://www.youtube.com/watch?v=m50PTFmmlxw

4. Amfanyie mtoto massage inaitwa "I love you tummy massage" akiona mtoto analia na kujinyonga nyonga na hayuko comfortable. Cheki vide chini hapa kuona namna ya kufanya

View: https://www.youtube.com/watch?v=nUNzi9PYBwc


View: https://www.youtube.com/watch?v=xfGtACWT9ng

Ukifanya kwa usahihi massage hiyo, kama mtoto alikuwa na gesi tumboni,basi utaona anajamba na ataacha kujinyonga na atalala kwa amani kabisa.
Financial Analyst

Ubarikiwe mara elfu
 
Mimi wa kwangu kashazidi huo umri anatembea yuko chekechea ila ikilala anastuka na kuanza kulia iwe mchana au usiku...ana mwaka na nusu +...
 
Mtoto huyo hashibi,maziwa ya mama hayamtoshi.Mpe maziwa ya ng'ombe au kopo.Utakuja kunishukuru.
Habari.

Nina mtoto wa miezi miwili. Kuna changamoto aliyonayo ya kutolala karibia usiku mzima yaani analala kimagepu huku akiwa hayuko comfortable.

Na akiwa macho hatulii na mama yake pia akimuweka kitandani hataki kukaa peke yake anaanza kulia. Akimpatia pia nyonyo muda mwingine anakataa muda mwingine ananyonya.

Hali hii inatokea pia na mchana.

Msaada kudhibiti hii hali kama umeshawahi kuipitia na mwanao.
 
Habari.

Nina mtoto wa miezi miwili. Kuna changamoto aliyonayo ya kutolala karibia usiku mzima yaani analala kimagepu huku akiwa hayuko comfortable.

Na akiwa macho hatulii na mama yake pia akimuweka kitandani hataki kukaa peke yake anaanza kulia. Akimpatia pia nyonyo muda mwingine anakataa muda mwingine ananyonya.

Hali hii inatokea pia na mchana.

Msaada kudhibiti hii hali kama umeshawahi kuipitia na mwanao.
Hongera kwakupata mtoto
 
Mtoto huyo hashibi,maziwa ya mama hayamtoshi.Mpe maziwa ya ng'ombe au kopo.Utakuja kunishukuru.

Kiafya haishauriwi kumpà mtoto aliyechini ya miezi sita kitu chochote isipokuwa maziwa ya Mamaake.

Anunue kikamulia maziwa(Breast pump) na mikopo vyake. Kisha amkamulie maziwa ya Mamaake. Kisha awe anampa.

Mtoto wa miezi miwili atahitaji 600ml to 800ml Kwa siku.
 
Habari.

Nina mtoto wa miezi miwili. Kuna changamoto aliyonayo ya kutolala karibia usiku mzima yaani analala kimagepu huku akiwa hayuko comfortable.

Na akiwa macho hatulii na mama yake pia akimuweka kitandani hataki kukaa peke yake anaanza kulia. Akimpatia pia nyonyo muda mwingine anakataa muda mwingine ananyonya.

Hali hii inatokea pia na mchana.

Msaada kudhibiti hii hali kama umeshawahi kuipitia na mwanao.
Kila baada ya kunyonyeshwa muweke begani umukimpapa mgongoni au kama kumpiga (Ile ya kubembeleza) ili atoe upepo (acheue). Hapo anaweza kutulia unapomlaza au kumuacha mwenyewe. Upepo tumboni huwasumbua Sana
 
Iliwahi nitokea mzee nikawa nalala sebuleni namuacha mama ake apambane na mtoto! Ila baadae nilimlipa mama ake kwa usumbufu alioupata pamoja na gharama za kunyonyesha mtoto kwa miaka 2!
 
Nenda pharmacy pia nunua gripwater

Ni dawa ya maji kwa watoto wachanga na ni normal tu kutumia ..inatoa ges


Afu kiasili kama unakaa na majan yale si tunaita milumbalumba japo ina majina mengi

Mama ake amchemshie japo vijiko viwili kwa siku atakua normal
 
Hakika nimejifunza mengi Sana kwenye huu Uzi.
Mbarikiwe Sana wore mliochangia.
 
Wewe nenda kacheze na watoto wenzio kule, huku kwa watu wazima. Mtoto wa miezi miwili hana ratiba ya chakula.
🤣🤣🤣🤣 kunyonya sio kula...? mkuu nina watoto watatu... na idadi hiyo ina kamilishwa na mapacha....!​
 
Back
Top Bottom