Msaada: Mama yangu anasumbuliwa na tatizo la akili ambalo hospitali halionekani

THE JAGGERS

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2023
Posts
545
Reaction score
410
Salamu kwenu wakubwa zangu.🙏

Wakuu nina changamoto ya kifamilia, kiafya zaidi na ninaomba msaada kutoka kwenu.

Mimi ni mwanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu ninaishi na mzee (baba), wadogo zangu pamoja na mama wa kufikia. Situation ipo hivi ndani ya siku za hivi karibuni since last year katika familia yangu mama yangu wa kufikia huwa anashindwa kutafsiri vitu vizuri. Kwa mfano; ukimuuliza kitu fulani anajibu kengine, anazunguka nyumba nzima usiku kucha (halali), hali vizuri na sometimes huwa anapiga makelele kiufupi ni kama ana ukichaa fulani hivi

Tulifanikisha kumpeleka hadi hospitali ya ukichaa (Milembe) lakini wakasema hana tatizo lolote la akili. Binafsi nimegundua imani potofu na kumbukumbu zinamtesa sana. Kuna muda anakuwa sawa kuna muda hawi sawa especially asipopata kulala na ni mbishi mno ukimwambia kitu hakuelewi ifikapo usiku halali kutwa anazunguka tu hadi panakucha na ikitokea tukawa hatupo (school or market statue) huwa anatoroka nyumbani

Kitu kinachotisha zaidi kuna muda mwili wake unakakamaa na akiwa hivyo basi huwa haongei kabisa wala halali kiufupi anakuwa kama zezeta na ikitokea akiongea basi huwa anapiga kelele mpaka majirani wanamsikia.

Kwa hofu huwa tunamfunga na kamba ili asifanye lolote baya. Tumejaribu kumpeleka hospitali lakini haisaidii
Misikiti pamoja na hata Makanisa haisaidii pia .

Pia nimuathirika wa VVU. Samahanini lakini ila kuna wakati tunashindwa kuendesha masomo yetu vizuri mimi pamoja na wadogo zangu.

Naombeni msaada kwenu
Wasalam .
 
Salamu kwenu wakubwa zangu.🙏
Wakuu nina changamoto ya kifamilia kiafya zaidi na ninaomba msaada kutoka kwenu.
Mimi ni mwanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu ninaishi na mzee(baba), wadogo zangu pamoja na mama wa kufikia. Situation ipo ivi ndani ya siku za hivi karibuni since last year katika familia yangu mama yangu wa kufikia huwa anashindwa kutafsiri vitu vizuri kwa mfano,
ukimuuliza kitu flaani anajibu kengine ,
anazunguka nyumba nzima usiku kucha (halali), hali vizuri na sometimes huwa anapiga makelele kiufupi ni kama anaukichaa flaani ivi japo tulifanikisha kumpeleka hadi hospitali ya ukichaa (milembe) lakini wakasema hana tatizo lolote la akili binafsi nimegundua imani potofu na kumbukumbu zinamtesa sana. Kuna muda anakuwa sawa kuna muda hawi sawa especially asipopata kulala na ni mbishi mno ukimwambia kitu hakuelewi ifikapo usiku halali kutwa anazunguka tu hadi panakucha na ikitokea tukawa hatupo (school or market statue) huwa anatoroka nyumbani
Kitu kinachotisha🥺 zaidi kuna muda mwili wake unakakamaa na akiwa ivyo basi huwa haongei kabisa wala halali kiufupi anakuwa kama zezeta na ikitokea akiongea basi huwa anapiga kelele mpaka majirani wanamsikia.
Kwa hofu huwa tunamfunga na kamba ili asifanye lolote baya.
Tumejaribu kumpeleka hospitali lakini haisaidii
misikiti pamoja na hata makanisa haisaidii pia .

samahanini lakini ila kunawakati tunashindwa kuendesha masomo yetu vizuri mimi pamoja na wadogo zangu.
Naombeni msaada kwenu
Wasalam .

Pole sana.

Hongera kwa kumjali na kumtunza mama yako licha ya changamoto alizonazo, ni baraka kufanya hivyo,, mvumilie na msichoke kumsaidia kwa kadiri ya uwezo wenu.

Umesema mmempeleka hospitali na nyumba za inabada lakini hakupa ahueni, napenda kujua kama alifanyiwa vipimo hospitalini (vipimo vya aina gani na pengine vilionesha kitu gani?). Vipi umri wake ukoje?
 
Shukuran mkuu kwa umri anamiaka 34 tu pili kwa vipimo vyake daktari alitoa wazo la kumpima fungus kwenye ubongo lakini hawakuona fungal yoyote mkuu
 
Salamu kwenu wakubwa zangu.🙏
Wakuu nina changamoto ya kifamilia kiafya zaidi na ninaomba msaada kutoka kwenu.
Mimi ni mwanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu ninaishi na mzee(baba), wadogo zangu pamoja na mama wa kufikia. Situation ipo ivi ndani ya siku za hivi karibuni since last year katika familia yangu mama yangu wa kufikia huwa anashindwa kutafsiri vitu vizuri kwa mfano,
ukimuuliza kitu flaani anajibu kengine ,
anazunguka nyumba nzima usiku kucha (halali), hali vizuri na sometimes huwa anapiga makelele kiufupi ni kama anaukichaa flaani ivi japo tulifanikisha kumpeleka hadi hospitali ya ukichaa (milembe) lakini wakasema hana tatizo lolote la akili binafsi nimegundua imani potofu na kumbukumbu zinamtesa sana. Kuna muda anakuwa sawa kuna muda hawi sawa especially asipopata kulala na ni mbishi mno ukimwambia kitu hakuelewi ifikapo usiku halali kutwa anazunguka tu hadi panakucha na ikitokea tukawa hatupo (school or market statue) huwa anatoroka nyumbani
Kitu kinachotisha🥺 zaidi kuna muda mwili wake unakakamaa na akiwa ivyo basi huwa haongei kabisa wala halali kiufupi anakuwa kama zezeta na ikitokea akiongea basi huwa anapiga kelele mpaka majirani wanamsikia.
Kwa hofu huwa tunamfunga na kamba ili asifanye lolote baya.
Tumejaribu kumpeleka hospitali lakini haisaidii
misikiti pamoja na hata makanisa haisaidii pia .

samahanini lakini ila kunawakati tunashindwa kuendesha masomo yetu vizuri mimi pamoja na wadogo zangu.
Naombeni msaada kwenu
Wasalam .
Poleni
 
Kuna science ya asili, hii inakwenda kwa njia ya IMANI. Hapa tunaongelea nguvu (energy za kiroho au spiritual power. Unaweza ukadharau lakini hili lina nguvu kubwa kubwa sana. Mawazo au thoughts ni moja ya hizo nguvu, zikitekwa ndio hiyo shida mnaiona inaionesha mwilini..

Ili kuweza kuzikabili yabidi apatikane mmoja wenu au mtu mwingine mwienye nguvu kuliko alinazo kuzizima hizo, maana yeye hapo alipo ni mateka.

Sasa nini cha kufanya, haijalishi wewe ni mkristo, mhindu au mwislam nk. Yesu kristo ana nguvu juu ya hili na anatenda kupitia watu wake. Ninyi wenyewe mkiwa na imani mnaweza kumsaidia kupitia imani ya Yesu. Lakini kwa msaada wa haraka mpelekeni kwenye madhabahu za maombezi, kuna Suguye pale Matembele ya pili au Mwamposa pale Kawe wote wapo Dar es salaam. Haujataja mkoa ulipo, ila pia unaweza kuona watu wengine wenye nguvu (imani) ya kuombea hapo ulipo utapata matokeo.

Nashauri kwa Mwamposa Kawe Dar es salaam.

Lakini pia kama upo mbali na Dar es Salaam, mwekeni kwenye tv mfuatilie maombi pamoja na yeye, Arise and Shine Tv ni kila siku usiku saa 3.

Angalizo.
Uponyaji wa Yesu haulipiwi, ukiona mtoa huduma anakwambia lipia hata kama ni shilingi mia kabla au hata baada ya huduma hapo hakuna kitu kimbia.

Unaweza kutoa sadaka mwenyewe ili huduma iendelee kwa wengine na mtoa huduma na wasaidizi wake wapate mahitaji yao. Hii ni hiari na unavyojisikia
 
Kuna science ya asili, hii inakwenda kwa njia ya IMANI. Hapa tunaongelea nguvu (energy za kiroho au spiritual power. Unaweza ukadharau lakini hili lina nguvu kubwa kubwa sana. Mawazo au thoughts ni moja ya hizo nguvu, zikitekwa ndio hiyo shida mnaiona inaionesha mwilini..

Ili kuweza kuzikabili yabidi apatikane mmoja wenu au mtu mwingine mwienye nguvu kuliko alinazo kuzizima hizo, maana yeye hapo alipo ni mateka.

Sasa nini cha kufanya, haijalishi wewe ni mkristo, mhindu au mwislam nk. Yesu kristo ana nguvu juu ya hili na anatenda kupitia watu wake. Ninyi wenyewe mkiwa na imani mnaweza kumsaidia kupitia imani ya Yesu. Lakini kwa msaada wa haraka mpelekeni kwenye madhabahu za maombezi, kuna Suguye pale Matembele ya pili au Mwamposa pale Kawe wote wapo Dar es salaam. Haujataja mkoa ulipo, ila pia unaweza kuona watu wengine wenye nguvu (imani) ya kuombea hapo ulipo utapata matokeo.

Nashauri kwa Mwamposa Kawe Dar es salaam.

Lakini pia kama upo mbali na Dar es Salaam, mwekeni kwenye tv mfuatilie maombi pamoja na yeye, Arise and Shine Tv ni kila siku usiku saa 3.

Angalizo.
Uponyaji wa Yesu haulipiwi, ukiona mtoa huduma anakwambia lipia hata kama ni shilingi mia kabla hata baada ya huduma hapo hakuna kitu kimbia.

Unaweza kutoa sadaka mwenyewe ili huduma iendelee na kwa wengine na mtoa huduma na wadaidizi wake wapate mahitaji yao. Hii ni hiari na unavyojisikia
Shukuran mkuu kunakitu sikukinotice kweny maelezo yangu
 
Pole sana.

Nafikiri ana tatizo ndiyo maana ana dalili hizo. Kama hana maradhi mengine yoyote yanayomsumbua basi afya yake ya akili haiko sawa.

Milembe hospital mliambiwa hana tatizo lolote lakini kwa hizo dalili (kupiga kelele, kushindwa kutafisiri vitu/kutoa majibu tofauti nk) kuna kitu hakiko sawa.

Kitaalamu kuna tatizo/ugonjwa unaoitwa Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia) ambapo mtu huwa na dalili za kuchanganyikiwa, hasira, kushindwa kutafisiri vitu au kutoa majibu tofauti na maswali, kuwa na sonona (depression) nk.

Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na:
-kuumia ubongo (traumatic brain injury)

-uvimbe kwenye ubongo (brain tumors)

-maambukizi kwenye mfuko wa neva

-magonjwa mengine ya ubongo kama Alzheimer's, Dementia nk

Ili kuweza kubaini tatizo hili, Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia) vipimo vifuatavyo hufanyika:
-CT scan brain au
-MRI brain
Pia wataalamu wa lugha (speech therapists) wana vipimo vyao maalumu vya kuwafanyia wagonjwa hao.

Kwa hiyo kwa dalili zake hizo kuna shida ambayo inaweza kuwa hiyo hapo juu [Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia)] au vingine. Haitoshi kusema kwamba yupo sawa.

Hivyo ni muhimu pengine mkampeleka hospital nyingine kubwa zaidi kama hakuwahi kwenda kwingine zaidi ya Milembe hospital.

Kila la kheri.
 
M
Salamu kwenu wakubwa zangu.🙏
Wakuu nina changamoto ya kifamilia kiafya zaidi na ninaomba msaada kutoka kwenu.
Mimi ni mwanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu ninaishi na mzee(baba), wadogo zangu pamoja na mama wa kufikia. Situation ipo ivi ndani ya siku za hivi karibuni since last year katika familia yangu mama yangu wa kufikia huwa anashindwa kutafsiri vitu vizuri kwa mfano,
ukimuuliza kitu flaani anajibu kengine ,
anazunguka nyumba nzima usiku kucha (halali), hali vizuri na sometimes huwa anapiga makelele kiufupi ni kama anaukichaa flaani ivi japo tulifanikisha kumpeleka hadi hospitali ya ukichaa (milembe) lakini wakasema hana tatizo lolote la akili binafsi nimegundua imani potofu na kumbukumbu zinamtesa sana. Kuna muda anakuwa sawa kuna muda hawi sawa especially asipopata kulala na ni mbishi mno ukimwambia kitu hakuelewi ifikapo usiku halali kutwa anazunguka tu hadi panakucha na ikitokea tukawa hatupo (school or market statue) huwa anatoroka nyumbani
Kitu kinachotisha🥺 zaidi kuna muda mwili wake unakakamaa na akiwa ivyo basi huwa haongei kabisa wala halali kiufupi anakuwa kama zezeta na ikitokea akiongea basi huwa anapiga kelele mpaka majirani wanamsikia.
Kwa hofu huwa tunamfunga na kamba ili asifanye lolote baya.
Tumejaribu kumpeleka hospitali lakini haisaidii
misikiti pamoja na hata makanisa haisaidii pia .

samahanini lakini ila kunawakati tunashindwa kuendesha masomo yetu vizuri mimi pamoja na wadogo zangu.
Naombeni msaada kwenu
Wasalam .
Mpelekeni kwenye maombi atakaa sawa,vinginevyo kama ana siri anaifahamu afunguke,huyo anaona vitu hivyo katika dimension nyingine
 
polleni sana naweza kumtibu nintajitolea kumtibu kwamakubaliano ambayo tutakubalia pande mbili.baada ya mgonjwa kupata nafuu nauhakika wa afya yake kwaidhini ya uubaji wake mtalipia gharama ambazo zitakua ndani yamakubaliano.
 
Back
Top Bottom