Kuna science ya asili, hii inakwenda kwa njia ya IMANI. Hapa tunaongelea nguvu (energy za kiroho au spiritual power. Unaweza ukadharau lakini hili lina nguvu kubwa kubwa sana. Mawazo au thoughts ni moja ya hizo nguvu, zikitekwa ndio hiyo shida mnaiona inaionesha mwilini..
Ili kuweza kuzikabili yabidi apatikane mmoja wenu au mtu mwingine mwienye nguvu kuliko alinazo kuzizima hizo, maana yeye hapo alipo ni mateka.
Sasa nini cha kufanya, haijalishi wewe ni mkristo, mhindu au mwislam nk. Yesu kristo ana nguvu juu ya hili na anatenda kupitia watu wake. Ninyi wenyewe mkiwa na imani mnaweza kumsaidia kupitia imani ya Yesu. Lakini kwa msaada wa haraka mpelekeni kwenye madhabahu za maombezi, kuna Suguye pale Matembele ya pili au Mwamposa pale Kawe wote wapo Dar es salaam. Haujataja mkoa ulipo, ila pia unaweza kuona watu wengine wenye nguvu (imani) ya kuombea hapo ulipo utapata matokeo.
Nashauri kwa Mwamposa Kawe Dar es salaam.
Lakini pia kama upo mbali na Dar es Salaam, mwekeni kwenye tv mfuatilie maombi pamoja na yeye, Arise and Shine Tv ni kila siku usiku saa 3.
Angalizo.
Uponyaji wa Yesu haulipiwi, ukiona mtoa huduma anakwambia lipia hata kama ni shilingi mia kabla au hata baada ya huduma hapo hakuna kitu kimbia.
Unaweza kutoa sadaka mwenyewe ili huduma iendelee kwa wengine na mtoa huduma na wasaidizi wake wapate mahitaji yao. Hii ni hiari na unavyojisikia