Msaada: Mama yangu anasumbuliwa na tatizo la akili ambalo hospitali halionekani

Msaada: Mama yangu anasumbuliwa na tatizo la akili ambalo hospitali halionekani

ni sahihi kabisa kwa miaka hii waathirika wengi wa HIV wanaotumia dawa hlf wakaamua kuziacha hizo dawa ndio wanakuwa na hizo dalili za kuvurugikiwa akili au ukichaa kupanda kichwani na mara nyingi ikifika hapo na akakosa matibabu sahihi ni lazma wanakata moto.
 
Pole sana.

Nafikiri ana tatizo ndiyo maana ana dalili hizo. Kama hana maradhi mengine yoyote yanayomsumbua basi afya yake ya akili haiko sawa.

Milembe hospital mliambiwa hana tatizo lolote lakini kwa hizo dalili (kupiga kelele, kushindwa kutafisiri vitu/kutoa majibu tofauti nk) kuna kitu hakiko sawa.

Kitaalamu kuna tatizo/ugonjwa unaoitwa Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia) ambapo mtu huwa na dalili za kuchanganyikiwa, hasira, kushindwa kutafisiri vitu au kutoa majibu tofauti na maswali, kuwa na sonona (depression) nk.

Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na:
-kuumia ubongo (traumatic brain injury)

-uvimbe kwenye ubongo (brain tumors)

-maambukizi kwenye mfuko wa neva

-magonjwa mengine ya ubongo kama Alzheimer's, Dementia nk

Ili kuweza kubaini tatizo hili, Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia) vipimo vifuatavyo hufanyika:
-CT scan brain au
-MRI brain
Pia wataalamu wa lugha (speech therapists) wana vipimo vyao maalumu vya kuwafanyia wagonjwa hao.

Kwa hiyo kwa dalili zake hizo kuna shida ambayo inaweza kuwa hiyo hapo juu [Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia)] au vingine. Haitoshi kusema kwamba yupo sawa.

Hivyo ni muhimu pengine mkampeleka hospital nyingine kubwa zaidi kama hakuwahi kwenda kwingine zaidi ya Milembe hospital.

Kila la kheri.
Nitumie namba zako kwa msaada zaidi
 
ni sahihi kabisa kwa miaka hii waathirika wengi wa HIV wanaotumia dawa hlf wakaamua kuziacha hizo dawa ndio wanakuwa na hizo dalili za kuvurugikiwa akili au ukichaa kupanda kichwani na mara nyingi ikifika hapo na akakosa matibabu sahihi ni lazma wanakata moto.
Shida inakuwa nini hasa?
 
wadogo zangu pamoja na mama wa kufikia
mkuu hapa umesema huyo ni mama wa kufikia. km hutajali unaweza kuelezea mama yako halisi yuko wapi au aliondoka kwenu katika mazingira gani? kama aliondoka kwa kinyongo inaweza kuwa ndo chanzo cha hayo yanayotokea.
 
Salamu kwenu wakubwa zangu.🙏

Wakuu nina changamoto ya kifamilia, kiafya zaidi na ninaomba msaada kutoka kwenu.

Mimi ni mwanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu ninaishi na mzee (baba), wadogo zangu pamoja na mama wa kufikia. Situation ipo hivi ndani ya siku za hivi karibuni since last year katika familia yangu mama yangu wa kufikia huwa anashindwa kutafsiri vitu vizuri. Kwa mfano; ukimuuliza kitu fulani anajibu kengine, anazunguka nyumba nzima usiku kucha (halali), hali vizuri na sometimes huwa anapiga makelele kiufupi ni kama ana ukichaa fulani hivi

Tulifanikisha kumpeleka hadi hospitali ya ukichaa (Milembe) lakini wakasema hana tatizo lolote la akili. Binafsi nimegundua imani potofu na kumbukumbu zinamtesa sana. Kuna muda anakuwa sawa kuna muda hawi sawa especially asipopata kulala na ni mbishi mno ukimwambia kitu hakuelewi ifikapo usiku halali kutwa anazunguka tu hadi panakucha na ikitokea tukawa hatupo (school or market statue) huwa anatoroka nyumbani

Kitu kinachotisha zaidi kuna muda mwili wake unakakamaa na akiwa hivyo basi huwa haongei kabisa wala halali kiufupi anakuwa kama zezeta na ikitokea akiongea basi huwa anapiga kelele mpaka majirani wanamsikia.

Kwa hofu huwa tunamfunga na kamba ili asifanye lolote baya. Tumejaribu kumpeleka hospitali lakini haisaidii
Misikiti pamoja na hata Makanisa haisaidii pia .

Pia nimuathirika wa VVU. Samahanini lakini ila kuna wakati tunashindwa kuendesha masomo yetu vizuri mimi pamoja na wadogo zangu.

Naombeni msaada kwenu
Wasalam .
Poleni sana. Hapo kwa hospital kusema ''hana tatizo la kiakili'' badilisha iwe ''walishindwa kugundua ana tatizo gani''. Hii ni kwa sababu unaweza kuzunguka hopsital hata tatu, ya nne ndiyo wakagundua tatizo lako. Msikubali kutumia waganga wa kienyeji, mtafilisika. Hata hawa mitume wa kisasa muwe macho nao. Mpelekeni hospital kubwa kama Muhimbili aonane wa mabingwa.
 
Hizi homa za hivi ni changamoto kwelikweli anaweza kumaliza hospitali juu ya hospitali akatoka kapa. ni vyema kujaribu maeneo mbalimbali hata izo tiba mbadala kama wakuu wanavyoshauri hapa hauwezi kujua ataponea wapi.

kuna sehemu apo juu nimeshuhudia kuna jamaa yetu alipata wazimu km huyo tulianza naye huko mahospitalini lakini alikuja kuponea kwenye tiba mbadala. huwa tunazichukulia poa lakn zinafanya kazi almradi tu wasiwe ni hawa matapeli waliojaa mijini. masangoma OG wengi wapo vijijini ndanindani uko na styms ni ngumu kuwapata maana wengi wa ivo hawapendi kujulikana.
 
Fanya utafiti wa mambo haya!
1.Ukoo wake kuna watu wana matatizo kama hayo.
2.Asiwe aliaachika kwa mme wake kisha akaolewa na baba yako
3.Anateseka huenda ni kwa sababu ya maagano ya babu zake waliyofunga na mizimu.
Kuwa na HIV siyo sababu ya kuwa hivyo! Wapo ambao ni HIV case lakini wanapewa councelling na kutumia dawa wanaendelea na maisha.
 
Hizi homa za hivi ni changamoto kwelikweli anaweza kumaliza hospitali juu ya hospitali akatoka kapa. ni vyema kujaribu maeneo mbalimbali hata izo tiba mbadala kama wakuu wanavyoshauri hapa hauwezi kujua ataponea wapi.

kuna sehemu apo juu nimeshuhudia kuna jamaa yetu alipata wazimu km huyo tulianza naye huko mahospitalini lakini alikuja kuponea kwenye tiba mbadala. huwa tunazichukulia poa lakn zinafanya kazi almradi tu wasiwe ni hawa matapeli waliojaa mijini. masangoma OG wengi wapo vijijini ndanindani uko na styms ni ngumu kuwapata maana wengi wa ivo hawapendi kujulikana.
Hospital kwanza. Narudia tena, hospital kwanza. Ile miaka ya nyuma ya kudhani kuna kulogwa inafikia ukingoni na karibu kila kitu kina maelezo ya kisayansi. Sikatai kuwa kuna dawa za kienyeji lakini unapopatwa na tatizo la kiafya hospital ndiyo sehemu ya kimbilio. Bahati nzuri sana tunaweza ku copy and paste kutoka majuu ambako wameshapitia hizi changamoto na kuzipatia ufumbuzi.
 
mkuu hapa umesema huyo ni mama wa kufikia. km hutajali unaweza kuelezea mama yako halisi yuko wapi au aliondoka kwenu katika mazingira gani? kama aliondoka kwa kinyongo inaweza kuwa ndo chanzo cha hayo yanayotokea
Hapo kwenye situation ya bimkubwa sidhani ila nakumbuka baada ya bimkubwa kugundua mwamba (mzee)amezalisha mwanamke mwengine ndipo akamamua kubeba vitu vyake na kusepa
Ila uzuri tupo mkoa mmoja japo huwa napenda sana kukaa kwa mzee
So one time huwa naenda kwa maza na kurudi n.k
So back to then nimekuwa nikikaa kwa bi wakufikia since 2012 of course ndio tulitesana na nini agh just was past only ila kwakusema kwamba alikuwa anambaya na mimi maybe huenda but simhukumu kwa chochote ila nadhani kuna ubaya aliwahi kunipangia kufanya si anajua me ndo mtoto wa kiume wa mzee..
Ni story ndefu mkuu nikiseme niwaambie hapa nitashusha simulizi
 
Hospital kwanza. Narudia tena, hospital kwanza. Ile miaka ya nyuma ya kudhani kuna kulogwa inafikia ukingoni na karibu kila kitu kina maelezo ya kisayansi. Sikatai kuwa kuna dawa za kienyeji lakini unapopatwa na tatizo la kiafya hospital ndiyo sehemu ya kimbilio. Bahati nzuri sana tunaweza ku copy and paste kutoka majuu ambako wameshapitia hizi changamoto na kuzipatia ufumbuzi.
Shukuran pia na ww mkuu
 
Ugonjwa wa akili haupimwi kwnye Maabara ila kwa observation za behaviors and experiences then unalinganisha na norms kufikia conclusions so ni kumuona psychiatrist au psychologist na team zao na itachukua muda kuconclude na certification so hizo deviations from normal zinakupa sababu sasa ya kutafuta huduma zaidi kabla haijawa mbaya sana
 
Back
Top Bottom