Pole sana.
Nafikiri ana tatizo ndiyo maana ana dalili hizo. Kama hana maradhi mengine yoyote yanayomsumbua basi afya yake ya akili haiko sawa.
Milembe hospital mliambiwa hana tatizo lolote lakini kwa hizo dalili (kupiga kelele, kushindwa kutafisiri vitu/kutoa majibu tofauti nk) kuna kitu hakiko sawa.
Kitaalamu kuna tatizo/ugonjwa unaoitwa Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia) ambapo mtu huwa na dalili za kuchanganyikiwa, hasira, kushindwa kutafisiri vitu au kutoa majibu tofauti na maswali, kuwa na sonona (depression) nk.
Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na:
-kuumia ubongo (traumatic brain injury)
-uvimbe kwenye ubongo (brain tumors)
-maambukizi kwenye mfuko wa neva
-magonjwa mengine ya ubongo kama Alzheimer's, Dementia nk
Ili kuweza kubaini tatizo hili, Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia) vipimo vifuatavyo hufanyika:
-CT scan brain au
-MRI brain
Pia wataalamu wa lugha (speech therapists) wana vipimo vyao maalumu vya kuwafanyia wagonjwa hao.
Kwa hiyo kwa dalili zake hizo kuna shida ambayo inaweza kuwa hiyo hapo juu [Wernicke's Aphasia (Receptive Aphasia)] au vingine. Haitoshi kusema kwamba yupo sawa.
Hivyo ni muhimu pengine mkampeleka hospital nyingine kubwa zaidi kama hakuwahi kwenda kwingine zaidi ya Milembe hospital.
Kila la kheri.