Nikirudi nyuma ktk Stori yako mama aliuza mashamba ya familia,na alikuwa na madeni mengi,nadhani hayo ambayo anayafanya sasa hivi huenda ni stress zinazo tokana na msongo wa mawazo.
Anyway yametokea ya kutokea na huna namna ya kuyabadilisha ingawa ni mazito kuyabeba ukiwa kama kijana wa kiume,kubwa ambalo naona ni la muhimu Sana ni wewe ujitahidi usiathirike na hayo yanayotokea mpaka kufikia kushindwa kutimiza ndoto zako,wazazi wameishi Maisha Yao basi na wewe jitahidi uishi Maisha yako,umetoa mfano mzur Baba amekupigia ukamwambia mwache mama kama alivyo nae akakusikiliza basi nawe uwe imara kama Baba yako.
Mwisho mama yako hata awe vipi ni mzazi wako,mpokelee Simu yake na msalimiane usimuwekee kinyongo,kitendo cha wewe kutotaka kuongea nae kitamkera na akinung'unika huenda kwako ikawa mtihani Sana,maana Hilo Linakuwa bifu lako na Mola wako na sio na mama yako.
Broo be strong, kuna a lot of things a head of you,kwahiyo SONGA MBELE na endelea kupambana