Msaada: Mama yangu kaolewa na kijana umri sawa na sisi wanae

Msaada: Mama yangu kaolewa na kijana umri sawa na sisi wanae

Pole sana pambana tengeneza maisha yako na uwasaidie wazazi wako wote,wewe simama kama mtoto usiingilie mambo ya wazazi ni laana mbaya sana.

Na kamwe usijaribu kuingilia mambo ya wazazi wala kuhoji mambo yake ya mahusiano,ni heshima mbaya sana.

Ukipata nafasi watumie wajomba,mababu zako na ndugu kwenda kuongea naye na kurekebisha palipoharibika,lakini wewe usithubutu kamwe hayo yapo nje ya uwezo wako.

Siku zote wapende wazazi wako usiwabague simamia nafasi yako kama mtoto,kwasababu hakuna mzazi anayekubali kuwa amekosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kama mamaaaa
Pole
Huenda anatumia bangi au kilevi fulani
 
Pole sana ndugu, life is living and living is pain, Yaani kwenye haya maisha unaweza kujiona una matatizo lkn mwenzako akikusimulia ya kwake unaona ya kwako yana nafuu.

Hebu fikiria mama mtu mzima anafanya vitu vya aibu kiasi hicho, hajali hata kuwa umri wa watoto umeshakuwa mkubwa na anawa aibisha watoto, Mungu atuhurumie kwa kweli...
 
ti mama yangu ameamua kuhama mji bila kumuaga mzee wangu,karudi kwao Mafinga Iringa na akaamua kuishi hapo kwao kwa muda usio eleweka.

Tukirudi nyuma,mama alishatuharibia sana mji kwani alifikia hatua ya kuuza mashamba ya familia bila kushirikisha mtu yeyote na akajiingiza kwenye madeni lukuki.

Hivi majuzi pia nilipokea ujumbe mfupi kutoka kwa ndugu wa karibu kuwa mama ameamua kwenda migodini na huko anafanya vitu vya ovyo sana na vya kutia aibu sana...yaani kama vile amekuwa ni binti mdogo.

Juzi pia nikapokea taarifa mbaya sna kupita zote kuwa ameolewa na kijana mdogo rika la kwetu sisi vijana wake na amefikia hatua ya kumpeleka kabsa pale nyumbani kwao....Ni almost 55's-60's anatembea na kijana wa 25s-40s,hii ni sahihi kweli?
Pole sana, lakini mwache dunia itamhukumu na kumwadhibu
 
Tatizo mdingi wako hampigi vizuri pipu mama yako,wacha aje kwetu tumpige pipu vzr
Kuwa na akiba ya maneno...kichaa anachekesha ikiwa hatoki kwenye familia yenu.....usiombe yakukute utatamani ata usingezaliwa
 
Pole sana!! Wazazi ni muhimu katika maisha yetu. Wana mchango mkubwa sana wakuchochea tabia fulani na muelekeo wetu katika maisha. Wewe bado ni mdogo kiumri, hivyo jifunze mengi kupitia hizo changamoto kutoka kwa mama, usiache kuongea naye, usiache kumshauri vizuri na kumuombea. Mengine yote ni juu yake kama binadamu. Huwezi fanya zaidi.

Lakini unaweza amua kuwa mtu sahihi kwake kwa kipindi chote cha changamoto hizo na Utabarikiwa kwa kumpenda, kumuheshimu na kumsaidia mzazi wako kwa kipindi ambacho ulipaswa kukimbia na kumpuuza. Usichukue maamuzi magumu, usiwaze sana. Kazi yako iwe, kumsikiliza anapokua na jambo, kumshauri ili kumpa muongozo sahihi, na kumuombea bila kukata tamaa.
 
Fanya mambo Yako Huyo ni mama Yako lakini ana haki ya kuishi maisha yake aliyo yachagua as long as hayavunji sheria za nchi kama hajitambui mpaka ktk umri huo alio nao hakuna Ambacho utaweza kukifanya kumbadilisha Tabia

Ishi maisha Yako Jenga future Yako
Hayo mengine achana nayo ,

Something will never change

Via 2pac shakur
 
1.Kalogwa katupiwa kitu ili awaibishe.
2. Mtu aingilie kati naashikilie biashara na apewe matumizi tu kama jacky.
3. Ni mama yenu aambiwe ukweli ila sana sana maombi yanahitajika anapepo langono na lakuwaibisha.
 
Nikirudi nyuma ktk Stori yako mama aliuza mashamba ya familia,na alikuwa na madeni mengi,nadhani hayo ambayo anayafanya sasa hivi huenda ni stress zinazo tokana na msongo wa mawazo.

Anyway yametokea ya kutokea na huna namna ya kuyabadilisha ingawa ni mazito kuyabeba ukiwa kama kijana wa kiume,kubwa ambalo naona ni la muhimu Sana ni wewe ujitahidi usiathirike na hayo yanayotokea mpaka kufikia kushindwa kutimiza ndoto zako,wazazi wameishi Maisha Yao basi na wewe jitahidi uishi Maisha yako,umetoa mfano mzur Baba amekupigia ukamwambia mwache mama kama alivyo nae akakusikiliza basi nawe uwe imara kama Baba yako.

Mwisho mama yako hata awe vipi ni mzazi wako,mpokelee Simu yake na msalimiane usimuwekee kinyongo,kitendo cha wewe kutotaka kuongea nae kitamkera na akinung'unika huenda kwako ikawa mtihani Sana,maana Hilo Linakuwa bifu lako na Mola wako na sio na mama yako.

Broo be strong,kuna a lot of things a head of you,kwahiyo SONGA MBELE na endelea kupambana
Ah wap....mama mpumbavu kama huyu hata akikupa laana haikupati hata kidogo
 
Fikiria Kusoma tu! Unachoweza kufanya akikupigia simu msikilize kama Mama ikiwezekana ndiyo muda wa kumweleza Masikitiko yako kwa hayo uliyosikia juu yake na hapo unaweza kumshauri arudi kwa Baba.Huwezi kujua yaliyomsibu huko mpaka akafikia hatua hiyo.
ZUNGUMZA NAYE KAMA MAMA,MAMA NI MAMA!
Usimfokee wala kumkaripia!!
 
Hii kitu inaumiza sana aisee.
Kama wazazi wako wanajiheshim basi shukuru Mungu tu.

Wengine waeza kuta dogo ana umri mkuhwa tu kama 16-20 lakini maza anaingiza wanaume tofauti tofauti ndani na kwa umri huo unajua fika nini kinaenda kufanyika huko ndani.

Pole sana mkuu, ila kua na mahusiano na kijana sio shida tatizo linaweza kua kama anatoka na hao vijana wengi wengi.
Na huo umri wa 26-40 mbona gape kubwa sana hapo kweny makadirio yako.
Mwanaume mwenye 35-40 ana muonekano wa kitu uzima kabisa kwa kibongo bongo.
 
Kuna mam mmoja vingunguti miaka ile alikua anatembea na marafiki wa mtoto wake wa kiume. Siku dogo alipogundua alimuambia mama yake.
Kuanzia leo nitaenda kusikojulikana na hutakaa unione Tena.
Mpaka Leo dogo hajaonekana
Kuna mijimama ina laana sana.
 
Akuna kitu nilikuwa na pinga kama hiki ila niliamua kuacha baada ya kuona kumbe nao wanateseka kukaa bila mwanaume
Mimi mama yangu ameolewa na kijana ambaye mimi nina mzidi umri na nina muita baba ndo chaguo la mama yangu
 
Back
Top Bottom