Msaada: Miaka hii 43 nampataje mwenza ambaye hana mtoto

Msaada: Miaka hii 43 nampataje mwenza ambaye hana mtoto

Hiyo kazi ya kukutafutia binti mbichimbichi kama Abichams wape dada zako na shangazi zako, haraka sana watakuletea mwali
 
Nimepigwa mno na single mothers ambao niliamini baada ya 'kupigika' tungeyajenga vizuri sana kwa maana wameshayajua maisha, lakini wapi!

Wa kwanza kanipiga, visa havieleweki tu kila siku. Mwishowe tukaamua yaishe.

Wa pili kanipiga, mtoto akikohoa kidogo tu zinaanza safari za 'kwenda kumtibu'. Nikaona nachotaka kufia hapa ni nini?

Huyu wa tatu ndio jana kaniuliza kabisa, huku mdomo akiwa kaupeleka pembeni (ishara ya dharau), "Hivi wewe kwa akili zako unafikiri kabisa nitamsahau niliyezaa nae? Mfyuuuu!"

Nimeondoka nyumbani mpaka sasa sijarudi.

Wadau, wapi anapatikana asiyekuwa na mtoto katika umri huo nijiandae kula nae kikokotoo?

Nimekwama, tusaidiane.
We si Ulikuwa Officer Mwandamizi wa Kataa Ndoa?
 
Nyie si mnajifariji kwamba single mothers wamekata tamaa na huwa wanatafuta mwanaume yeyote tu mradi anapumua, haya sasa taratibu tu mtakuja kuelewa kwamba dunia inabadilika meza zinapinduka na huko tunakoelekea ndio kubaya zaidi, wanawake wamebadilika siyo wa enzi zile na hawajali tena lolote
 
Back
Top Bottom