Msaada: Miaka hii 43 nampataje mwenza ambaye hana mtoto

Msaada: Miaka hii 43 nampataje mwenza ambaye hana mtoto

Nimepigwa mno na single mothers ambao niliamini baada ya 'kupigika' tungeyajenga vizuri sana kwa maana wameshayajua maisha, lakini wapi!

Wa kwanza kanipiga, visa havieleweki tu kila siku. Mwishowe tukaamua yaishe.

Wa pili kanipiga, mtoto akikohoa kidogo tu zinaanza safari za 'kwenda kumtibu'. Nikaona nachotaka kufia hapa ni nini?

Huyu wa tatu ndio jana kaniuliza kabisa, huku mdomo akiwa kaupeleka pembeni (ishara ya dharau), "Hivi wewe kwa akili zako unafikiri kabisa nitamsahau niliyezaa nae? Mfyuuuu!"

Nimeondoka nyumbani mpaka sasa sijarudi.

Wadau, wapi anapatikana asiyekuwa na mtoto katika umri huo nijiandae kula nae kikokotoo?

Nimekwama, tusaidiane.
mhn! ukivuka miaka 40 ni kazi kwelikweli ni bora ubahatishe haohao single mama vinginevyo hivi vitoto unahitaji kuwa kama rais wa Russia. ukibisha jiandae kusoma masomo ya kujitolea bila cheti (postgraduate in clinical officer specialized in sugar,pressure na vidonda vya tumbo) kwa kuwa hakuna dawa hutapata kuacha kuitumia na pia kuwa bingwa wa kuwashauri wengine.
 
Quick-Fluffy-Vitumbua-bp-1-1.jpg
Ndo matatizo ya kuzoea kudanganywa
 
kuna mtu ameishi kwa ndoa siku 43 au miezi 43 na ndoa ikavunjikaa

enda taratibu manake ushawatumia wengii ukawagwaya ukaona sio type yako.
 
Ulikuwa unafanya nini ulipokuwa kijana wa miaka 30-33?
swali nzuri sana ila unaweza usieleweke lakini mara nyingi kijana anahitaji kuoa kati ya miaka 27-32 ili anapofikisha miaka 35 ameanza kukomaa katika kupambana na changamoto familia.
 
Mtoto wa kike mzuri kama wewe inakuaje unakuwa na mawazo ya kijambazi hivyo?!!! Yaani kuna lipi hapo lililopitiliza hadi ionekane ni uongo?!!! Nimesema mtu alipaa km ndege?!!

Mie nimeunga mkono hoja ya Watu8 kwasababu hakuna namna naweza kumpinga...akisema ni chaii nakubaliana nae tu 🤣

Uzi wako ni chai lakini sio kivile
 
swali nzuri sana ila unaweza usieleweke lakini mara nyingi kijana anahitaji kuoa kati ya miaka 27-32 ili anapofikisha miaka 35 ameanza kukomaa katika kupambana na changamoto familia.

Ni kweli mkuu
Suala la mwanaume kuingia kwenye ndoa lipo mikononi mwake kwa asilimia nyingi...hasa kwa umri huo uliutaja

Hata mleta mada akiamua anapata na kuoa ndani ya mwaka huu
 
Back
Top Bottom