Msaada: Miaka hii 43 nampataje mwenza ambaye hana mtoto

Nimepigwa mno na single mothers ambao niliamini baada ya 'kupigika' tungeyajenga vizuri sana kwa maana wameshayajua maisha, lakini wapi!

Wa kwanza kanipiga, visa havieleweki tu kila siku. Mwishowe tukaamua yaishe.

Wa pili kanipiga, mtoto akikohoa kidogo tu zinaanza safari za 'kwenda kumtibu'. Nikaona nachotaka kufia hapa ni nini?

Huyu wa tatu ndio jana kaniuliza kabisa, huku mdomo akiwa kaupeleka pembeni (ishara ya dharau), "Hivi wewe kwa akili zako unafikiri kabisa nitamsahau niliyezaa nae? Mfyuuuu!"

Nimeondoka nyumbani mpaka sasa sijarudi.

Wadau, wapi anapatikana asiyekuwa na mtoto katika umri huo nijiandae kula nae kikokotoo?

Nimekwama, tusaidiane.
Tulia kwanza ujipe muda halafu urudi baada ya miezi miwili tushauriane.Kwa sasa bado una wenge sana.Tuliza ball.
 
Ukituliza akili bila kuhemkwa unapata mbona. Muhimu tu umpe uhakika kiuchumi, maana umri huo wanaamini lazima ukae sawa kiuchumi.
 
Unakosaje mwanamke ? Au wewe huwa una matarajio makubwa kutoka kwa mwanamke unae msaka ?
 
Nyie si mnajifariji kwamba single mothers wamekata tamaa na huwa wanatafuta mwanaume yeyote tu mradi anapumua, haya sasa taratibu tu mtakuja kuelewa kwamba dunia inabadilika meza zinapinduka na huko tunakoelekea ndio kubaya zaidi, wanawake wamebadilika siyo wa enzi zile na hawajali tena lolote
Ila wadada wengi wenye wanakaa na watoto wao , hawana hadhi ya kuitwa single maza , kwa sababu unakuta baba wa mtoto anatuma pesa za matunzo na elimu ya mtoto ila una kuta mdada bado anajiita single maza[emoji849]
 
Nimepigwa mno na single mothers ambao niliamini baada ya 'kupigika' tungeyajenga vizuri sana kwa maana wameshayajua maisha, lakini wapi!

Wa kwanza kanipiga, visa havieleweki tu kila siku. Mwishowe tukaamua yaishe.

Wa pili kanipiga, mtoto akikohoa kidogo tu zinaanza safari za 'kwenda kumtibu'. Nikaona nachotaka kufia hapa ni nini?

Huyu wa tatu ndio jana kaniuliza kabisa, huku mdomo akiwa kaupeleka pembeni (ishara ya dharau), "Hivi wewe kwa akili zako unafikiri kabisa nitamsahau niliyezaa nae? Mfyuuuu!"

Nimeondoka nyumbani mpaka sasa sijarudi.

Wadau, wapi anapatikana asiyekuwa na mtoto katika umri huo nijiandae kula nae kikokotoo?

Nimekwama, tusaidiane.
Wapo wengi Sana. Tafuta na uwe na pesa kiasi. Tafuta wa 25-30 yrs
 
Quick-Fluffy-Vitumbua-bp-1-1.jpg
 
Nyie si mnajifariji kwamba single mothers wamekata tamaa na huwa wanatafuta mwanaume yeyote tu mradi anapumua, haya sasa taratibu tu mtakuja kuelewa kwamba dunia inabadilika meza zinapinduka na huko tunakoelekea ndio kubaya zaidi, wanawake wamebadilika siyo wa enzi zile na hawajali tena lolote
Wengi bado ni tegemezi tu kwa hao waliowazalisha. Ndio maana hawaishi kupashana viporo ili huduma zirndelee. Mkuu dunia bado sana ipo mikononi mwa mwanaume, bado sana kupindua meza.
 
Back
Top Bottom