Natumai nyote mko vyema. Moja kwa moja kwenye mada, nina mtoto wa kiume ambaye mwezi wa sita mwaka huu ametimiza miaka miwili. Stages nyingine zote kama kukaa, kutambaa, kutembea, kuanza kuota meno etc. alizipitia kwa wakati. Akiwa na around mwaka mpaka mwaka na nusu alikuwa anaweza kusema mom, dady na kutaja vitu vichache. Lakini ghafla alipoteza uwezo wa kuongea. Kwa sasa anatoa tu sauti zisizo na mpangilio wowote wa lugha. Ninaomba kwa yeyote mwenye uzoefu, anayefahamu tatizo na tiba, anayemfahamu daktari au anayeweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, asaidie. Kwa nyumbani anaishi na kaka yake wa miaka 5, ambae anaongea vizuri tu. Tumemuanzisha pia daycare ili achangamane na watoto wenzake, amefanikiwa tu kuchangamka na kuongeza interaction, lakini suala la kuongea bado limekuwa changamoto. Msaada tafadhali
Habari!
Pole kwa yote mnayopitia kifamilia.
Ili kujua kama mtoto au mtu fulani hajaweza kufikia uwezo wake wa kuongea, ni vyema kuwa unafahamu kwa umri wake anatakiwa kuwa ana uwezo upi wa kutengeneza maneno. Wakati mwingine mtoto anaweza kuanza kwa spidi kubwa na kurejea kwenye hali yake tarajiwa au kinyume chake.
Tunazaliwa na uwezo tofauti, lakini mazingira pia huweza kuongezea au kupunguza uwezo husika.
Matatizo ya kutokuweza kutoa maneno kwa kiasi tarajiwa yakibeba maana au bila maana kulingana na umri, kunaweza kusababishwa na mambo haya:
1: Kutokuwa na uwezo wa kusikia
2: matatizo ya misuli ya ulimi
3: maendeleo dumavu ya ubongo
4: tatizo maalumu kwenye cerebral cortex.
5: matatizo ya kisaikolojia
6: mchango hasi au chanya wa mazingira yanayomzunguka mhusika.
7: madhira yaliyoanza tangu wakati wa ujauzito
Ili kuweza kujua kwa uhakika ni nini chanzo, tatizo halisi, kwa kiasi gani na nini kifanyike ni vyema zaidi kuhusisha SPEECH THERAPIST/mtaalamu maalumu wa tiba ya kuongea.
Hospitali kubwa hasa za rufaa vs Taifa (MNH) huwa na vitengo hivi. Nina uhakika pia kwa hospitali kama Agha Khan/Dar-es-salaam wana kitengo husika. Jaribu kufatilia kwa hospitali za ngazi hiyo hapo unaweza kuwapata wahusika na ukasaidika kupitia wataalamu hawa.
NB: Ufuatiliaji utaanza tangu ujauzito mpaka hapo alipofikia, pia jamii ya wahusika/wazazi ni vyema kupata taarifa zao.