Msaada: Mtoto kupoteza uwezo wa kuongea

Msaada: Mtoto kupoteza uwezo wa kuongea

Wako angalau.. Wangu next mwez wa 9 anatimiza 3yrs. Haongei kabisa. Nshampelema had hosp wakakata kile kilimi cha chini ya ulimi, lkn wapi. Anaongea maneno yasiyoeleweka.. Kusikia anasikia, ukimwita anakuja, katuni akisikia inaimba sebulen na tupo chumban anakurupuka anaenda sebulen. Means anasikia... Kuongea sasa..hasemi hata mma, mama au lolote.

Akitaka maji anakuletea kikombe.. Chooni anavua nguo then anakushika mkono, km kuchangamana apa home na kaa na watoto wawili wengine, achilia mbali majiran.. Ingawa huwa hachezi na wenzie.. Yy anacheza peke yake, na pembeniii.. Au anakaa ndani
Pole sn. Sio autism hio?
 
Natumai nyote mko vyema. Moja kwa moja kwenye mada, nina mtoto wa kiume ambaye mwezi wa sita mwaka huu ametimiza miaka miwili. Stages nyingine zote kama kukaa, kutambaa, kutembea, kuanza kuota meno etc. alizipitia kwa wakati. Akiwa na around mwaka mpaka mwaka na nusu alikuwa anaweza kusema mom, dady na kutaja vitu vichache. Lakini ghafla alipoteza uwezo wa kuongea. Kwa sasa anatoa tu sauti zisizo na mpangilio wowote wa lugha. Ninaomba kwa yeyote mwenye uzoefu, anayefahamu tatizo na tiba, anayemfahamu daktari au anayeweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, asaidie. Kwa nyumbani anaishi na kaka yake wa miaka 5, ambae anaongea vizuri tu. Tumemuanzisha pia daycare ili achangamane na watoto wenzake, amefanikiwa tu kuchangamka na kuongeza interaction, lakini suala la kuongea bado limekuwa changamoto. Msaada tafadhali
Kwa age hio usitie waswas sn. Ataongea huyo. Nishaona cases wengine wanafika 4 mpk 5 hawaongei na baade wanakaa sawa.

Ila sio vibaya kuongea na wataalam kwa uahauri zaidi
 
Ubarikiwe sana kwa kuweka neno la tumaini.
 
Wako angalau.. Wangu next mwez wa 9 anatimiza 3yrs. Haongei kabisa. Nshampelema had hosp wakakata kile kilimi cha chini ya ulimi, lkn wapi. Anaongea maneno yasiyoeleweka.. Kusikia anasikia, ukimwita anakuja, katuni akisikia inaimba sebulen na tupo chumban anakurupuka anaenda sebulen. Means anasikia... Kuongea sasa..hasemi hata mma, mama au lolote.

Akitaka maji anakuletea kikombe.. Chooni anavua nguo then anakushika mkono, km kuchangamana apa home na kaa na watoto wawili wengine, achilia mbali majiran.. Ingawa huwa hachezi na wenzie.. Yy anacheza peke yake, na pembeniii.. Au anakaa ndani
Kuna mchezo anapendelea kucheza mara kwa mara bila kuuchoka? Vipi yupo aggressive kwa wenzie hasa akichokozwa?
 
Mara nyingi watoto wa kiume huchelewa vitu vingi, ata kwenye ukuaji
 
Asante sana. Hospitali tumeshampeleka mara 2. Wamemchunguza, wanasema tuendelee kum-monitor. Hana tatizo la ukiziwi, ingawa mara nyingi akiitwa itamchukua relatively muda mrefu kurespond.
Upo mkoa gani? Kama upo Dar na imeenda Kwa wataalamu wa mfumo wa fahamu wa watoto Basi ni vyema kufuata Huo ushauri. Naonekana ni sahihi. Msitraumatize Kwa kumpeleka sehemu nyingi. Kila mlichofanya ni sahihi(kuhakikisha Hana tatizo la viuongo vya matamshi).... Hili hutokea na ni kitu Cha kuangalia na kuwa karibu na wataalamu husika. Pole
 
hana usonjii huyoo ni jambo la kawaidaa tu..
Nahisi haya mambo tuwaachie wataalamu. Hata mtaalam hawezi kujua kama. Kukaa. Kimya Kwa mtoto ni Kutokana na nini bila kufanya uchunguzi wa Ana Kwa Ana. Kukaa kimya Kwa mtoto inaweza kua sio tatizo au matoke ya mabadiliko, mshtukk, ukatili, taharuki, mabadiliko ya sehemu ya kuchanganua matamshi (wernicke /broca/Sylvia fissure), usonji, selective mutism, etc.....ila nakubali Ana nawe mama asipanick kwani viuongo vingine viko Sawa ila kuhusu ni nini na afanye nini, wataalamu wapo. Na hakuna mtaalam aliyekidhi taaluma yake anaye weza kutathmjni tatizo kupitia maelezo mafupi ya mtandao.
 
Hii inaitwa autism
Mpeleke kwa dr.kija mtaalam wa neuro yupo muhimbili
Inaweza isiwe autism ikawa kitu kingine...... Nakubali Ana nawe Dr. Kija ataweza kuwa msaada mkubwa kutambua ni nini. Paediatric Neurologist atasaidia sanaa🙏🙏🙏🙏
 
Upo mkoa gani? Kama upo Dar na imeenda Kwa wataalamu wa mfumo wa fahamu wa watoto Basi ni vyema kufuata Huo ushauri. Naonekana ni sahihi. Msitraumatize Kwa kumpeleka sehemu nyingi. Kila mlichofanya ni sahihi(kuhakikisha Hana tatizo la viuongo vya matamshi).... Hili hutokea na ni kitu Cha kuangalia na kuwa karibu na wataalamu husika. Pole
Asante sana mkuu.
 
Pole sana, usisahau wazee ni muhimu sana au Kwa mwamposa sio kawaida hilo jambo
Natumai nyote mko vyema. Moja kwa moja kwenye mada, nina mtoto wa kiume ambaye mwezi wa sita mwaka huu ametimiza miaka miwili. Stages nyingine zote kama kukaa, kutambaa, kutembea, kuanza kuota meno etc. alizipitia kwa wakati. Akiwa na around mwaka mpaka mwaka na nusu alikuwa anaweza kusema mom, dady na kutaja vitu vichache. Lakini ghafla alipoteza uwezo wa kuongea. Kwa sasa anatoa tu sauti zisizo na mpangilio wowote wa lugha. Ninaomba kwa yeyote mwenye uzoefu, anayefahamu tatizo na tiba, anayemfahamu daktari au anayeweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, asaidie. Kwa nyumbani anaishi na kaka yake wa miaka 5, ambae anaongea vizuri tu. Tumemuanzisha pia daycare ili achangamane na watoto wenzake, amefanikiwa tu kuchangamka na kuongeza interaction, lakini suala la kuongea bado limekuwa changamoto. Msaada tafadhali
Inaweza kuwa Autism au ni Speech delay, Huwa nafanya therapy kwa watoto wenye changamoto kama hizo ila muhimu ni kufanya Diagnosis kujua Nini shida. Unaweza kwenda Muhimbili kwa Dr. Kija
 
Natumai nyote mko vyema. Moja kwa moja kwenye mada, nina mtoto wa kiume ambaye mwezi wa sita mwaka huu ametimiza miaka miwili. Stages nyingine zote kama kukaa, kutambaa, kutembea, kuanza kuota meno etc. alizipitia kwa wakati. Akiwa na around mwaka mpaka mwaka na nusu alikuwa anaweza kusema mom, dady na kutaja vitu vichache. Lakini ghafla alipoteza uwezo wa kuongea. Kwa sasa anatoa tu sauti zisizo na mpangilio wowote wa lugha. Ninaomba kwa yeyote mwenye uzoefu, anayefahamu tatizo na tiba, anayemfahamu daktari au anayeweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine, asaidie. Kwa nyumbani anaishi na kaka yake wa miaka 5, ambae anaongea vizuri tu. Tumemuanzisha pia daycare ili achangamane na watoto wenzake, amefanikiwa tu kuchangamka na kuongeza interaction, lakini suala la kuongea bado limekuwa changamoto. Msaada tafadhali

Jaribuni pia kumkazania lugha moja, msimchanganyie lugha, kiswahili, kingereza mara mother tongue language kwa huo umri mdogo, inamchanganya mtoto na atashindwa kujiamini kuwa ashike ipi. By the way kwa umri huo bado mdogo, Mungu atamsaidia ataongea tu wakati wake ukifika wa kuongea.
 
Nahisi haya mambo tuwaachie wataalamu. Hata mtaalam hawezi kujua kama. Kukaa. Kimya Kwa mtoto ni Kutokana na nini bila kufanya uchunguzi wa Ana Kwa Ana. Kukaa kimya Kwa mtoto inaweza kua sio tatizo au matoke ya mabadiliko, mshtukk, ukatili, taharuki, mabadiliko ya sehemu ya kuchanganua matamshi (wernicke /broca/Sylvia fissure), usonji, selective mutism, etc.....ila nakubali Ana nawe mama asipanick kwani viuongo vingine viko Sawa ila kuhusu ni nini na afanye nini, wataalamu wapo. Na hakuna mtaalam aliyekidhi taaluma yake anaye weza kutathmjni tatizo kupitia maelezo mafupi ya mtandao.
yani akianza hizo cliniz za usonji sijui matakataka gani ni kumchosha tu mtotoo...mwisho wa siku atafikiri kwend hadi kwa mgangaaa ni suala la kusubirii muda utaamua mtoto kushindwa kuongea vizuri sio ugonjwaaa ni wenge tu la mzazi
 
Jaribuni pia kumkazania lugha moja, msimchanganyie lugha, kiswahili, kingereza mara mother tongue language kwa huo umri mdogo, inamchanganya mtoto na atashindwa kujiamini kuwa ashike ipi. By the way kwa umri huo bado mdogo, Mungu atamsaidia ataongea tu wakati wake ukifika wa kuongea.
Asante kwa ushauri mkuu. Tunaendelea nae mdogo mdogo. We pray and hope the best for him
 
Jaribuni pia kumkazania lugha moja, msimchanganyie lugha, kiswahili, kingereza mara mother tongue language kwa huo umri mdogo, inamchanganya mtoto na atashindwa kujiamini kuwa ashike ipi. By the way kwa umri huo bado mdogo, Mungu atamsaidia ataongea tu wakati wake ukifika wa kuongea.
Mtu anafundishwa kihindi,kimeru,kichina,kiswahili, kingereza sasa siatazimia
 
Back
Top Bottom