Msaada: Mtoto kupoteza uwezo wa kuongea

Mwamposa angekuwa na huo uwezo pasingekuwa na wagonjwa mahospitalini
Dah [emoji23][emoji119]!
Ila mm ninachofahamu ni kwamba, Imani huponya pia
Wapo watu hospitali hakuna wanachokipata ila wakienda kwa Wachungaji na Mashehe, wanapata faraja
Ndio maana hata madaktari wanatoa directives kwamba huu ugonjwa nendeni tu kwa watu wa Imani
 
Nilisikia watoto wa kiume huwa wanachelewa kuongea. Naamini ataweza kuongea.
 
Poleni sana kwa changamoto mnazopitia ndugu zetu
 
Reactions: Mit
Pole sana mkuu
 
Mie nikutie moyo Mkuu, watoto hawafanani naamini ataongea kwani alishawahi kuongea hapo nyuma, vuta subra na maombi yaendelee kwa imani yako wakati unaendelea kutafuta solution na kwa wataalam pia kama baadhi walivyoshauri hapo juu. Mwenyezi Mungu ni muaminifu atatenda.
 
Anamawili mapepo au kuna mtu anamtishia so kaharibika kisaikolojia au bado muda wake dada angu alikaa hadi latatu ndio akanza kusoma kuandika vyema so hawa watoto niwazito kuongea ila wanaakili kinyama sana so ataongea tu
 
Miaka miwili bado mdogo, hata hivyo unajaribu kumuongelesha...?

Kijana wangu nilikua namwita naanza kumwambia moja, mbili anafuatisha hiyo inasaidia kulainisha ulimi

Bado naamini kwenye njia za asili kumpeleka hospital iwe hatua ya badae
 
Pole sana mkuu kamchunguze hospital na masikio pia kama anasikia vizuri, hii inatokeaga nimeshawahi kuona visa vya namna hii lakin mwishowe ataongea Tu, pia penda Mwenywe kumuongelesha utabaini vingi
 
Aisee, haya maneno sio mazuri hata kidogo, hujafa hujaumbika ndugu. Kama hatuwezi kuwa faraja kwa wengine basi tusiwavunje moyo wanaohitaji hiyo faraja.
Mtoa mada hajahitaji faraja. Kaja kuomba ushauri
 
Pole sana mkuu kamchunguze hospital na masikio pia kama anasikia vizuri, hii inatokeaga nimeshawahi kuona visa vya namna hii lakin mwishowe ataongea Tu, pia penda Mwenywe kumuongelesha utabaini vingi
Asante sana. Hospitali tumeshampeleka mara 2. Wamemchunguza, wanasema tuendelee kum-monitor. Hana tatizo la ukiziwi, ingawa mara nyingi akiitwa itamchukua relatively muda mrefu kurespond.
 

Habari!

Pole kwa yote mnayopitia kifamilia.

Ili kujua kama mtoto au mtu fulani hajaweza kufikia uwezo wake wa kuongea, ni vyema kuwa unafahamu kwa umri wake anatakiwa kuwa ana uwezo upi wa kutengeneza maneno. Wakati mwingine mtoto anaweza kuanza kwa spidi kubwa na kurejea kwenye hali yake tarajiwa au kinyume chake.

Tunazaliwa na uwezo tofauti, lakini mazingira pia huweza kuongezea au kupunguza uwezo husika.

Matatizo ya kutokuweza kutoa maneno kwa kiasi tarajiwa yakibeba maana au bila maana kulingana na umri, kunaweza kusababishwa na mambo haya:

1: Kutokuwa na uwezo wa kusikia
2: matatizo ya misuli ya ulimi
3: maendeleo dumavu ya ubongo
4: tatizo maalumu kwenye cerebral cortex.
5: matatizo ya kisaikolojia
6: mchango hasi au chanya wa mazingira yanayomzunguka mhusika.
7: madhira yaliyoanza tangu wakati wa ujauzito

Ili kuweza kujua kwa uhakika ni nini chanzo, tatizo halisi, kwa kiasi gani na nini kifanyike ni vyema zaidi kuhusisha SPEECH THERAPIST/mtaalamu maalumu wa tiba ya kuongea.

Hospitali kubwa hasa za rufaa vs Taifa (MNH) huwa na vitengo hivi. Nina uhakika pia kwa hospitali kama Agha Khan/Dar-es-salaam wana kitengo husika. Jaribu kufatilia kwa hospitali za ngazi hiyo hapo unaweza kuwapata wahusika na ukasaidika kupitia wataalamu hawa.

NB: Ufuatiliaji utaanza tangu ujauzito mpaka hapo alipofikia, pia jamii ya wahusika/wazazi ni vyema kupata taarifa zao.
 
Asante sana mkuu. Umeeleweka. Kwa sasa familia iko mkoani. Tumeshampeleka kwa madaktari wa watoto, wanasema waendelee kumuangalia hadi atimize miaka 3, ili dalili zijitokeze. We'll also try the speech therapists. Dhumuni kubwa tusijeambiwa huko mbele kwamba hali ya mtoto ingetengemaa kama tungewahi matibabu.
 
Sio ana usonji (autism) mpeleke kwa wataalamu
 
Sio ana usonji (autism) mpeleke kwa wataalamu
Hatujui. Ndio tunajaribu kupata experience na misaada ya mawazo ya wadau.
Miaka miwili bado mdogo, hata hivyo unajaribu kumuongelesha...?

Kijana wangu nilikua namwita naanza kumwambia moja, mbili anafuatisha hiyo inasaidia kulainisha ulimi

Bado naamini kwenye njia za asili kumpeleka hospital iwe hatua ya badae
Ni kweli bado mdogo kumkatia tamaa. Lakini alishaanza kusema mom, dad, one, two... akiwa na mwaka na nusu. Ghafla vikapotea. Ndo tunajaribu kuangalia njia za kurejesha kauli mdomoni mwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…