Msaada: Mtoto kupoteza uwezo wa kuongea

Ubongo wa mtoto ni karatasi nyeupe, kila unachomlisha kinajaa kwenye akili yake, lakini kumbuka unatumia penseli hivyo basi usisahau kurudia vile unavyomwambia itamsaidia kukariri ama kukumbuka
 
Wangu alitimiza miaka mitatu hatoi neno hata moja!! Nilipeleka kwa wataalam wakasema mzima na alinishtua zaidi alianza kuongea kama bubu!!

Kuna mama mmoja mtaalam wa saikolojia ya watoto nilikutana nae Mbeya nilienda kikazi huko!! Alinipa ushauri nimchanganye na watoto rika lake wanaoongea vyema.

Nikampeleka kwenye kishule hivi, haikupita miezi sita siku hiyo nabadilisha chanel (natoa cartoon) nasikia ananiambia "baba unazingua". Nikajua hapa tayari lugha ishachanganya!!!
 
Hii inaitwa autism
Mpeleke kwa dr.kija mtaalam wa neuro yupo muhimbili
 
Mpeleke kwa dr.kija muhimbili hizo ni dalili za autism
Mtoto huanza kuongea then baadae maneno yanapotea kabisa
 
Aisee!! Mungu akusamehe Mkuu.

Mwenzio anajaribu kutafuta msaada na faraja, Unampa majibu ya hovyo.
Hivi Una mtoto? Unaujua uchungu wa kuwa
Mzazi?

Natamani nikutukane, Ila nimejizuia.
Kuna uhovyo gani kwenye jibu langu? (Nisaidie ili nielewe nsije kurudia)
 
Mkumbuke machimbuko yao mababu na mababu zao mizim ile ya ukoo mkasali makaburini muombe dua watoto wapate baraka za wazee wa zamani, mkiendelea kujifanya wakishua mtatesa watoto
 
Mitatu bado usikate tamaa wangu ndio anatafuta sita ndo kaweza kuongea asilimia 80, kaanza kidogo kidogo akiwa na miaka 5.
 
Mkumbuke machimbuko yao mababu na mababu zao mizim ile ya ukoo mkasali makaburini muombe dua watoto wapate baraka za wazee wa zamani, mkiendelea kujifanya wakishua mtatesa watoto
Si hadi awe na Imani hizo.
Mtoto kuchelewa kuongea Kama vipimo vyote vipo sawa Sio big deal wapo uchelewa hata miaka 7 ndio uongea asilimia 100
 
Ndio maana tunauliza kama kuna lolote wazazi tunaweza fanya kumsaidia mtoto. Kama Mungu ameamua kutupatia bubu, atakuwa amejua tuna nguvu ya kumlea, na wallah tutamlea.
Hakuna ububu hapo.
Japo kwa age hizo pia ni muhimu pia kuchek ishu za kiroho.Pana bro wetu marehemu historical alikuwa Kama na miaka 3 akaacha kuongea maneno kamili kwa kutokuwa na elimu ya kiroho ikachukuliwa kawaida ndio akawa hivyo hivyo ububu.
Ilikuja julikana baada ya miaka 30 ilikua ni ishu za kiswahili ingewahiwa mapema ingesolvika
 
Aisee nimetafuta hii post. Nliona mtu mwingine amepost same thing on insta jana anasema aliambiwa mtoto amekuwa na too much toxins in the body lead ikiwa ndio kwa kiwango kikubwa. Mwingine akacomment akasema wa kwake aliambiwa ana dalili za autism ndio maana. Sasa sijui which is which labda ujaribu kufanya a little research. Nakutakia mafanikio na namwombea mwanetu awe sawa
 
Ina maana mwanao hawajakueleza ana usonji?
 
Usihofu sana, jaribu pia kwenda kumuona speech therapist. Ninajua watoto ambao wameongea na miaka mitatu na zaidi. Kinachotokea inawezekana anachanganyikiwa ni lugha gani ajifunze hasa kama mnatumia lugha zaidi ya moja kuwasiliana hapo nyumbani.
 
Mkuu nenda hospital watakusaidia zaidi inaweza kuwa ana autism !! Mpeleke kwa madaktari wa akili wako vizuri watakudadavulia kwa usahihi !
 
Miaka 2/3 ni kawaida sana. Usitishike ataongea. Nimelea watoto naelewa. Wanatofautiana sana. Akifika 4 haongei kabisa hapo una haki ya kuwa na wasiwasi. Kama ukimwita anasikia na huwa unamsikia akiongea baadhi ya maneno hata kama si kwa usahihi usihofu.
 
Watoto hawafanani ktk ukuaji as long as haumwi. Na hiyo ya kubadilika ni Transformation tu anaenda kuongea vizuri baada ya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…