Msaada: Mwanamke niliyezaa naye alienda kwao baada tu ya kujifungua, hataki nimuone mtoto

Msaada: Mwanamke niliyezaa naye alienda kwao baada tu ya kujifungua, hataki nimuone mtoto

Kw
Nenda kwao..wakakutambue
Kwao wananitambua hata wakati ameenda kujifungua ni mama yake ndio tulikuwa tunawasiliana nae. Mama zake mdogo wameshawahi kukaa kwangu kwa siku kadhaa kwa vipindi tofauti.
 
Mkuu kitu cha kwanza fungua kesi upime DNA kuthibitisha kama mtoto ni wako,
Kisha mambo mengine yafuate,

Mtoto kaandikishwa kwa jina lako? Yaani kwa ubini wako?
Halali hua haipotei,

Pole sana mkuu,
Good luck
 
Vijana wa siku hizi nani kawaloga? Unahitaji kuambiwa nini kwamba mtoto si wako?

Tafuta mtoto wako kwingine. Acha ujinga
Hahaa mkuu kutafuta sio suala kubwa kama kuthibitisha ili badae tusijuane.
 
Mkuu kitu cha kwanza fungua kesi upime DNA kuthibitisha kama mtoto ni wako,
Kisha mambo mengine yafuate,

Mtoto kaandikishwa kwa jina lako? Yaani kwa ubini wako?
Halali hua haipotei,

Pole sana mkuu,
Good luck
Asante sana mkuu.
Mtoto kaandikishwa kwa jina langu ndio sababu mwanzo process zote zilifanyika kwangu from kupima mimba na kuanza clinic alipokaribia kujifungua ndio akaondoka hata jina la mtoto nilimpa mimi.
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri huu lakini nachotaka nimalize kabisa hili suala. Nifunge kurasa kama nina mtoto nae au sina isije badae nikajutia kwamba mtoto ni wangu na nilimwacha kwa muda mrefu.

Hata kama sio wangu nijue tu sitadai gharama wala sita laumu mtu ila niwe free sina kwamba sina mtoto nae. Kwa sasa wakati mwingine roho inaniuma nikikumbuka nina mtoto na sifanyi lolote juu yake.

Nikithibitisha sio wangu nitakuwa free zaidi kwani hata sasa ninaishi na mwanamke mwingine.
Sababu ni hii hapa,inaonyesha hakuna mawasiliano mazuri kati yenu na ndio maana hata sasa unaishi na mwanamke mwingine,
Na kama kwao wameshajua una mke mwingine wakati mtoto wao umemzalisha muda si mrefu wamekuchukia.hawakutaki.
La msingi ni kama unavyosema hapo juu wakupe msimamo kama mtoto ni wako uwajibike huduma,na kama si wako upite hivi...
Hapo kuna mambo mengi kati yako na huyo " mzazi" mwenzàko.
 
Hahaa mkuu kutafuta sio suala kubwa kama kuthibitisha ili badae tusijuane.
Unapoteza muda bure. Dada wa watu kajitahidi kukupa ukweli indirectly wewe unashupaa.

Kwani libelous halisimami utafute mtoto wako.

Achana na huyo. Wewe ulikuwa baba mlezi. Baba mzazi kashapewa majukumu yake na kayakubali

Maisha lazima yasonge mbele.
 
Kw
Kwao wananitambua hata wakati ameenda kujifungua ni mama yake ndio tulikuwa tunawasiliana nae. Mama zake mdogo wameshawahi kukaa kwangu kwa siku kadhaa kwa vipindi tofauti.
Kutambua sio kukujua ni kwa kutoa posa na kulipa mahari.bahati mbaya tayari una mtu mwingine unaishi nae
 
Jirani yangu mwanae kampa baba wawili baba og anamuheshimu baba fake anapigwa mizungusho kama wewe na matumizi anatoa
 
Wakuu Salaam,

Moja kwa moja kwenye mada. Mwaka juzi nilipata mtoto na mwanamke mmoja nilikuwa nikiishi naye wakati huo.

Kipindi chote cha ujauzito alikuwa akiishi kwangu mara baada ya kujifungua akaenda nyumbani kwao kupata msaada wa karibu. Alijifungua vizuri mtoto wa kike na baada ya miezi 2 alikuja na mtoto na kukaa siku kadhaa akarudi tena kwao.

To cut story short ni kwamba ilipita muda haji kwangu na kuomba tu matumizi ya mtoto kupitia simu baada ya muda kupita nikamwambia nataka nimuone mtoto mana nimemmiss muda sasa akawa analeta story tu mtoto hamleti.

Nikaamua kukata kutuma hela hadi mtoto aje/aletwe nimuone basi ikawa shida hakumleta mtoto tangu muda huo. Umepita muda sasa mwaka sijamuona mtoto nahitaji kumuona nimeenda kwao lakini nazungushwa kwamba hayupo kasafiri wakati marafiki zake wanasema yupo.

Sasa wakuu naomba tusaidiane nianzie wapi ili kushinikiza kumuona huyu mtoto niende serikali za mtaa au police kabisa? Na kama kuna njia nyingine ya kufanya kumuona tu mtoto mana najua sitaruhusiwa kumchukua kwani bado mdogo.

N:B huyu mwanamke sikumtolea mahari tuliishi pamoja tu tukapata mtoto.
Mtoto so wako
 
Asante sana mkuu.
Mtoto kaandikishwa kwa jina langu ndio sababu mwanzo process zote zilifanyika kwangu from kupima mimba na kuanza clinic alipokaribia kujifungua ndio akaondoka hata jina la mtoto nilimpa mimi.
Uhalali wa kujua ni mwanao au sio mwanao utathibitishwa scientifically kupitia DNA test,

Usikate tamaa wala usiache kutoa matumizi ya mtoto,hata kama itakua sio wako basi fanya utakua kama ulitoa sadaka kwa malaika,

Kua strong bro na ukweli utajulikana,jaribu kuongea na Mama wa mtoto ili kujua sababu hasa inayopelekea wao kutokutaka wewe kumuona mtoto,usipopata majibu ya kuridhisha nenda kisheria,

Sheria zipo ili kutatua matatizo kama haya,usivunjike moyo kwa comments za JF.
 
Kama hataki Umuone anakuzungusha huyo sio mwanao lakini na wewe Uliishi nae miezi yote ya mwanzo ile KUMUANGALI TU MTOTO hukuona kama umepigwa???? Au ndo hujui kufananisha.. ndugu zako nao pia hawajui??? Anyway cha muhimu huyo mwanamke mtafute mkaee usikute kamgawa mwanao kisa kuna mwanaume anatoa pesa zaidi yakoo yani PELEKA KESI POLISI Kama sio ustawi wa jamiii ili jambo liishe kisheria sio kwa maneno mkuu..! Pole sana ila Simamia hili jambo mapema bora upoteze muda na hela hata kwa kupima DNA ili nafsi yako iwe Huru pole sana.
DNA kwa tanzania ukipima lazima upigwe tu labda aende kenya bongo miyeyusho sana kwenye inshu za DNA
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri huu lakini nachotaka nimalize kabisa hili suala. Nifunge kurasa kama nina mtoto nae au sina isije badae nikajutia kwamba mtoto ni wangu na nilimwacha kwa muda mrefu.

Hata kama sio wangu nijue tu sitadai gharama wala sita laumu mtu ila niwe free sina kwamba sina mtoto nae. Kwa sasa wakati mwingine roho inaniuma nikikumbuka nina mtoto na sifanyi lolote juu yake.

Nikithibitisha sio wangu nitakuwa free zaidi kwani hata sasa ninaishi na mwanamke mwingine.
Achana nae nature itaamua hapo badae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom