Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

Inaonyesha watz wako na tabia flani ambayo inazingua, sema kwa upande wa wenzetu wa kenya wao wako na changamoto nyingi zakimaisha kuliko hata huku tz kwaiyo wakiskia kuna job mahali hawalazi damu

Nmetembea Dubai, aise wakenya, waganda, waNigeria wengi sana...wabongo hawaonekani 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wanakuwaga wagumu sana maana wa bongo wengi wazinguaji, unakuta mtu hana hata passport halafu anaenda agent wa Kenya ..kwa hiyo wanawakataa..halafu pia wanaweka bei juu sana kwa watz, unakuta hadi USD 1000 uko wakati kwa mkenya mwenzake ni 100 tu.

Hapa ndipo huwa wananishangaza hawa viumbe wenye tamaa na money...mtu amekuja kwako ana shida kwa maana hana pesa, alafu wewe unamuomba tena pesa ili umpatie kazi...kama ana pesa atakuja kuhangaika kukutafuta kote huko! Hawana msaada aise!
 
Mtalalamika sana, ukweli ni kwamba Mbongo ukimsaidia lazima akulize!! Yaan waliosema "ukiona mahali pana chuki jua wema ulitangulia" hawakukosea hata kidogo.

Unamsaidia Mbongo na kazi unamtafutia, unampa connections zote!! Atachoanza ni fitna, zile connections ziwe zake wewe upoteze urudi Bongo mikono mitupu!! Ndiyo raha ya waswahili hiyo!!

Kuna mahali Asia huko tulishawishi timu ya kubebana wabongo!! Kilichotokea, si unajua mkishakaa wabongo wengi mahali!! Mnauwana wenyewe kwa wenyewe, huo mpango ukafeli
 
Wewe upo wapi mkuu?
 

Mzungu na Mwarabu watakusaidia unapopatwa na shida ila mbongo sasa may be wachache! Tena apate nafasi nzuri kama ofisini na awe bosi wako aisee utakimbia na utaiona kazi chungu.


Mbongo akiwa ofisini dunia yote yake, au anajiona kama yuko paradise vile....Mwafrika na mhindi ni kama baba mmoja ivi, wengi wao tabia zinaendana.
 
Daah mkuu sijui nianzie wapi ila sisi watanzania ni watu wa kuuana sisi kwa sisi na hii ni ajabu, leo hii alhamis kuna mwanangu school mate kabisa yupo uarabuni na ana certificate tu ya biashara nimemuuliza alicho nijibu nikachoka hapo hapo
KUNA SEHEMU tunakosea lazima tujifunze kubadilika kwakweli
 
nilichokuja kugundua ni kuwa hao ulio wataja wameathiriwa sana na umasiki....umasikini ni mbaya sana ndugu yangu aswa ukiuendekeza...kenya ni masikini lakini ni masikini wasomi ambao wanachanganya umasikini na jeuri....wamejikubari na wapo teyari kupambana na umasikini wao...tz ni masikini lakini umasikini wetu umeambatana ana adui mkubwa nae ni UJINGA...
 
KUNA SEHEMU tunakosea lazima tujifunze kubadilika kwakweli
Japo sio saana ila Ukweli ni roho mbaya, ina tutesa sana roho ya kumuona mwenzako ana teseka alafu wewe una furahi ndio hio, hatuoni fahari tukifanikiwa watanzania wote
 
Daah mkuu sijui nianzie wapi ila sisi watanzania ni watu wa kuuana sisi kwa sisi na hii ni ajabu, leo hii alhamis kuna mwanangu school mate kabisa yupo uarabuni na ana certificate tu ya biashara nimemuuliza alicho nijibu nikachoka hapo hapo
Kasemaje huyo ndorobo?
 
kazi ipo kama upo serious nitafute jamaa atawafanyia interview ijumatatu means 12/7/2021

kazi ni ya udereva tax wa kampuni ambayo utakuwa unafanya kwa masaa 12 tu kwa siku.

mahitaji ni passport na leseni ya udereva class C.

Wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini.

mshahara ni 800$ ambayo utakuwa unalipwa kila mwisho wa mwezi.

Note:
kinachohitajika ni passport na driver licens tu,viza na vitu vingine vyote utalipiwa isipokuwa utakatwa 800$ kama gharama ya agent ambae atakuwa responsible kwa lolote utapokuwa huko dubai.

makato hayo ya agent yatafanyika kama ifuatavyo.

Baada ya kupewa viza na kupatiwa ticket yako ya ndege na kusaini mkataba ukiwa air port utatakiwa kumpa agent 200$ kama malipo yake ya kwanza na hizo 600$ utatakiwa kulipa kwa kukatwa 100$ kila mwisho wa mwezi kwa miezi 6.

na safari mnatakiwa mpaka tarehe 25 muwe mlishasafiri.

Note 2:
kuhusu usalama wa mwajiriwa ni kwamba mkataba wenu utakuwa signed chini ya wizara ya kazi na ajira na kutakuwa na sehemu ya ubalozi wa Tanzania na mnakoenda kusign.
pia mwishoni kutakuwa na wadhamini wa hiyo kampuni(mwajiri) ambao wanaishi masaki ambao watakuwa responsible kwa lolote litalowapata mkiwa kwenye ajira yenu dubai.

Nafasi zilikuwa 10 now bdo wawili so kama utakuwa na vigezo au interested
karibu pm ila hakikisha unavigezo husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…