Msaada namna na kuondoa watuamiaji kwenye router ya airtel 5G

Password lazima nimpe hata mimi nikienda ofisini kwake natumia wifi yake, kuna muda tunatumiana large file
Mchane asigawe connection.
Au tengeneza account ya guest na limit user. So unakua na account mbili moja yako nyingine ya guest.
 
Ni simple sana kublock wanaopewa acces bila wewe kuruhusu.

Njia nzuri ni kuwablock kwa kutumia MAC Address.

Fanya kama ifuatavyo:

1. Login kwenye user access yako.

2. Ukishaingia, nenda kwenye DHCP Information.


3. Ukishaclick DHCP Information, click Device List na utaona users wote wanaotumia router yako.


4. Copy MAC Address za Devices ambazo unahitaji kuziblock. Kisha nenda kwenye kipengele cha Firewall.


5. Ukishaclick Firewall, nenda kwenye kipengele cha Filtering Rules. Kisha nenda kwenye MAC Filtering, kisha nenda kwenye Add Rule.


6. Itakuletea popup window ya kujaza MAC Address, ukishaijaza utaconfirm.


7. Mwisho kabisa, uta Save And Apply Rules. Hiyo MAC Address haitakaa ipate internet mpaka utakapoitoa kwenye hiki kifungo.
 
Ahsante sana mkuu, nitafanya hivyo kesho nikifika ofisini
 
Unampa ya nin?
 
naunga mkono hoja mkuu njia hii nzuri sana
 
Unlimited alafu unakuwa mnoko.

Acha ubahili ndugu, ilo bundle la TZS 110,000 bado wanakupiga alafu unashindwa kuwasaidia watu.

Mimi nina router la kuunga watu 200, uswahilini kwangu nimrwagaia bure password wanafurahia data za bure muda wote.
 
Solution yako ipo hapa.
 
Simple sana,badili password,na atakapokuja muunganishe na hotspot kutoka kwenye simu yako,ili iwe rahisi kwako kucontrol
 
Big up mkuu! Safi sana aisee haya madude nlikuwa nayamudu sana kipindi hiko Module Moja ilikua inaitwa NETWORK AND SYSTEM ADMINISTRATION
 
Nahitaji vifaa vya internet, mikrotik router, access points like ubiquity m2. Mwenye navyo njoo PM.
 
Hata baba yangu angeanza kugawa password ningempiga ban, sielewi unamvumilia vipi huyo mtu.

Kumbuka tu MAC ni device specific so hao wakitumia device nyingine watapata pia kwenye compyuta ni rahisi kubadili MAC ila watumiaji wa kawaida hawalijua hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…