Msaada namna na kuondoa watuamiaji kwenye router ya airtel 5G

Unlimited alafu unakuwa mnoko.

Acha ubahili ndugu, ilo bundle la TZS 110,000 bado wanakupiga alafu unashindwa kuwasaidia watu.

Mimi nina router la kuunga watu 200, uswahilini kwangu nimrwagaia bure password wanafurahia data za bure muda wote.
Pengine anataka internet iwe faster na unajua ukiunga watu wengi speed inapungua
 
Mbona unatumia njia ndefu wakati njia fupi ipo? Suluhisho ni kumchana uyo rafiki yako mwambie aache kushare na wengine. Shida nini unamuogopa?
 
Ahsante sana mkuu, nitafanya hivyo kesho nikifika ofisini
Mkuu ahsante hii njia yako imefanya kazi, ubarikiwe sana
 
Unlimited alafu unakuwa mnoko.

Acha ubahili ndugu, ilo bundle la TZS 110,000 bado wanakupiga alafu unashindwa kuwasaidia watu.

Mimi nina router la kuunga watu 200, uswahilini kwangu nimrwagaia bure password wanafurahia data za bure muda wote.
Wabongo si roho mbaya😂
 
Hiyo uhakika.... Mtu anakuwa yuko connected na wifi ila haupati hata 1kb, hata browser haifunguki...

Hapo soon utasikia milio huko nje, watajileta wenyewe. Utasikia "Mkuu umebonyeza wapi mbona hatupati internet tena?"
😂😂 umetisha mkuu
 
Mbona unatumia njia ndefu wakati njia fupi ipo? Suluhisho ni kumchana uyo rafiki yako mwambie aache kushare na wengine. Shida nini unamuogopa?
Mkuu nimemchana mara kibao ila haelewi na kila akija lazima password kwa sababu kazi zetu zinahitaji internet sana
 
Kila nikiangalia kwenye connect list naona kuna users zaidi ya 10, mimi binafsi natumia simu na laptop pekee, nahisi rafiki yangu ame share kwa watu mwengine.

- Andaa orodha ya MAC address zote ambazo ziko xonnected bila idhini kama hivi

  • Ingia opion ya pili tokea chini| Firewall

  • Ingia hapo| Filtering rules

  • Hakikisha Umechagua | Blacklist

  • Kisha chagua | MAC filtering

  • Chagua | Add Rules

  • Andika MAC Address kama mfano unavo onesha, lisha Confirm,

Hatua ya mwisho click| Save And Apply Rules, ( Hapo utakuwa umeblock flow ya data kwenye kifaa husika ambacho kinatumia Data bila idhini yako.)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…