Ishu iko hivi, hao viongozi wanapaswa kisheria kutoa ushahidi wa uwajibikaji wa serikali na mlolongo wa kiutawala kuhusu lile shambulio lake la mwaka 2017 kule Dodoma. Lissu amewaita kama mashahidi wa lazima kwa sababu kipindi anapigwa risasi hawa wote walikuwa viongozi wakuu serikalini.
kwa hiyo kisheria wana wajibu wa kuieleza mahakama nini kilitokea. Kimsingi, ushahidi wao lazima utagusa mambo makubwa mawili , kwanza kabisa ni suala la ulinzi kuondolewa. Eneo la Area D Dodoma lilikuwa na ulinzi wa masaa 24, ni kwamba Lissu anataka wakuu wa Majeshi na viongozi hao waiambie mahakama ni nani aliyetoa order ya kuondoa askari mageti na doria siku ile yeye anashambuliwa, kwa sababu haiwezekani ulinzi usiwepo ghafla siku hiyo ya tukio, pili ni swala la faili la upelelezi. Miaka yote hii serikali inasingizia upelelezi bado unaendelea lakini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa, kuwaita hawa wakuu maana yake Lissu anataka kuilazimisha serikali ilete ripoti zote za siri za kiintelijensia na jalada la upelelezi mahakamani ili ukweli ujulikane.
Kwahiyo ikitokea wakafika mahakamani kweli, wakaapa kizimbani, kudanganya itakuwa ni ngumu kwa sababu kwanza ni kosa la jinai, na Lissu kupitia mawakili wake atapata nafasi ya kuwabana vizuri kwa maswali. Kama wakienda mahakamani then watoe majibu kama hawajui au hawakumbuki hayo majibu yatakuwa ushahidi tosha kwa Jaji kuonyesha kuwa serikali ilifanya uzembe wa makusudi kushindwa kulinda maisha yake, na kama wakiamua kusema ukweli na kuleta nyaraka, basi siri zote za nani alituma wauaji zitavuja mchana kweupe. Kwa hiyo, Lissu anawavuta kwenye uwanja wake ili kuweka rekodi sawa na kuumbua mfumo mzima wa ulinzi, na hapo ndipo atakaposhinda mapema tu.