Msaada: Naomba kupewa gharama za hatua hizi za ujenzi


Mkuu, hizi bei ni za kitaa, ukitaka kuumia tumia mafundi wa masaki huko, utaumia sana. Blundering kwa vile umesema haina madoido makubwa sebleni, possibility ya 2x2 za 700,000-800,000 kutosha ni kubwa, then ukikutana na fundi wa kitaa akikupiga 400,000-500,000 kazi inaisha, tena hadi blundering ya nje.

Kwa uzoefu wangu, kwenye plaster nyumba hiyo ufundi tu inaweza kufika 1,200,000(nje -ndani) au zaidi kutegemeana na maelewano. Weka 40-50bags za cement, gari mbili za mchanga(fuso) coz moja hatotosha. Hivyo 50x14,000/-=700,000+240,000+1,200,000= ....hapo bado maji, mbao za kench ili fundi afikie juu.
 
Makisio yako yanaendana na uhalisia, hivi ukitumia tofali za block mbona bado inakula sana cements pamoja na kuta zimenyoshwa vizuri naomba kujua hii ipoje kuna fundi mmoja aliniambia mifuko 54 ya saruji yani kila chumba ni 3bags pamoja na nyumba yangu kiwa kubwa ukirejea kwenye vipimo hapo juu post za mwanzo, halafu fundi mwingine aliniambia mifuko 33bags za saruji zinatosha hapo ndipo ninapo shangaa.... So far plumbing na wiringi kazi imeanza naona gharama zina akisi hazijazidi zipo minimum..
 
Acha kuropoka wewe. Ana madirisha 11 grill moja kaambiwa 150,000 jumla ni 1,650,000.
Nyinyi ndio huwa mnajisifu nimejenga nyumba ya 100m mtu akiangalia haoni cha 100m kumbe umepigwa tu.
Mkuu ushauri wako huwa upo makini na una uzoefu, pia unaletaga makadirio yenye uhalisia, ingawa kuna watu humu wanakatisha tamaa sana, ni heri kuchuja ushauri wa kila mtu, mtu ukifikia mpaka kwenye kuezeka ni 80% halafu mtu anakuambia hapo ni kama 40%,mzee nimeanza naona nasogea mkuu, wiring plus plumbing kazi zilianza... Vifaa vya plumbing phase A tayari na maji tayari yapo ndani nasubiri phase B finishing, vivyo hivyo wiringi phase A tayari wamechimbia conduct pipe na switch box nimeweka njia mpaka za solar so far mambo yanaenda, madirisha week ijayo mkuu, achana na waumiza vichwa.
 
Naongea kutokana na experience, so we hujajenga bora ukae kimya. Kuna vioo umeweka gharama zake?, kuna fundi hujamlipa
Yupo right... Kuna mchango wake hapo juu umenisaidia sana, kila mtu ana changia kutokana na uzoefu kumbuka jinsi tulivyo geographically hatuwezi fanana gharama za ujenzi
 
Humu pia kuna michango imenipa akili ya kujiongeza, inategemeana na umakini wa mtu mimi local fundi ndiyo wamenijengea nyumba yangu mpaka kufika hapa, so unachosema ni kweli ila pia nahitaji other source of information
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatutoi sadaka
Hahahahaha leteni na zile za kwenye jumuiya ndogo ndogo
 
Safi mkuu sikuwepo hewani muda kifogo ilanimekutana na huu ushauri Eli79 kaka wa sakayo nimekuelewa sana, maji yapo ya bomba na tayari mpaka ndani nimeshaingiza, wiringi phase A tayari, hapo kwenye plasta haupo mbali sana hata makadirio yapo sawa ya material cements fundi alisema 54bags kwa maana kila chumba ni 3bags so naona it is proportional.........thanks..msalimie dada ako sakayo
 
Hahaha, hongera sana kiongozi kwa hatua kubwa hiyo. Salamu zimemfikia "dada Sakayo"!!!
 
Tiles inategemea unataka Spanish au Mchina.
Mchina grade 1 sitting room 50*50 ndio zinapendeza box moja 30,000-35,000/- box moja sqm 1.5. Sitting room yako 20sqm utahitaji 14boxes ambayo ni 490,000/-.
Fundi anachaji sqm moja 5,000/-
Safi lkn Umesahau cement ama Gundi ya kushikiza hizo tiles!
 
Siomafundi wote wenye njaa Mkuu.
Na ukimpeleka kwa mafundi njaa ataleta mrejesho wa yaliyojiri. Tafuta mafuundi wa gharama kwa faida yako.
 
Hivi gharama za kumlipa fundi kwa kazi ya plasta huwa ni mpaka kufitisha grill pia, au kufitisha grill ni gharama separate na plasta?
 
Hivi gharama za kumlipa fundi kwa kazi ya plasta huwa ni mpaka kufitisha grill pia, au kufitisha grill ni gharama separate na plasta?
Kufitisha grills na frames ni gharama nyingine mkuu. Mara nyingi wanafanya 10,000 kwa grill/frame moja, kama madirisha na milango ni mingi unaomba discount hata kwa 7,000.
 
Kufitisha grills na frames ni gharama nyingine mkuu. Mara nyingi wanafanya 10,000 kwa grill/frame moja, kama madirisha na milango ni mingi unaomba discount hata kwa 7,000.
Ndiyo mkuu nashukuru kwa muongozo.
 
Hahaha, hongera sana kiongozi kwa hatua kubwa hiyo. Salamu zimemfikia "dada Sakayo"!!!
Mkuu mambo vipi, eti mkuu naomba muongozo kwa uwekaji wa tiles je square meter 1 fundi anachaji kiasi gani?
 
Kuna tofauti gani kati ya gypsum bod ya Tanzania vs Thailand naona tu zimepishana bei tu, ila sijui ubora upoje, waliotumia za Thailand wanipe tofauti zake tafadhali
 
Kuna tofauti gani kati ya gypsum bod ya Tanzania vs Thailand naona tu zimepishana bei tu, ila sijui ubora upoje, waliotumia za Thailand wanipe tofauti zake tafadhali
Hili swali la mafundi,maanake mimi nikiangalia naona zote sawa. Fundi aliniambia ninunue za Thailand ndio nzuri,nilifuata maelekezo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…