Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

kati ya 2.8 mil upewe 50k una akili kweli kama unaenda kudai pesa hyo bora uache tu..

Pia angalai na uwiano wa watoto wengine kama ni mmoja tu anaye basi angalau upate 250k kwenda mbele.
Yaani kila mwezi atoe 250k iyo ajira? Ushawahi udhuria ata kikao kimoja cha Ustawi mkuu.? Hesabu haziendi simple hivo. Mtu unakuta ana mshahara wa 2.8M usikute ni Gross. Bado kuna makato unakuta take home 2.1M tu.
Bank? Saccos? Bodi? Etc etc
Bado ana familia nyingine?

Yaani hapo akipata 50k sio mbaya. Ikizidi sana 75k.
 
Kweli kabisa !

Halafu wengine unakuta mimba/mtoto wanapewa wanaume 3 [emoji108]

Kote anatarajia kupata ruzuku ya matunzo ya mimba/mtoto ,

Ndiyo maana hawataki kwenda kupima DNA.

Wengi tu wanawauzia wanaume watoto ambao si wao ili wapate hela za malezi.
Sahihi kabisa, kuna case moja nilisimuliwa ofisi ya ustawi wa jamii, jamaa wanne wamepangwa wanatoa matunzo kwa mtoto kila mmoja anaamini yeye ndo baba wa mtoto, kwa nini uingie kichwa kichwa kwa hawa wanawake wajanja wajanja wa mjini. Unaweza kujikuta unaangua kilio.
 
1.Sheria kuhusu hilo itungwe.
2.Sheria kuhusu abortion ipitishwe

Na ndiposa tutaweza kushtakiana vizuri, kwa hapa hatuna sheria hiyo nadhani. Kwahiyo si kosa kisheria mtu yeyote kumbebea mimba yeyote kwa kupenda/hila/ulaghai etc
Mimi ikija akaniletea bila makubaliano yoyote nitaenda mahakamani, tutajua huko huko.
 
Nyie wanawake nyie! Kwa hiyo ulimpanulia hadi akataja Siri za Mshahara wake ndo ukampa bila kuzingatia siku za hatari?
 
Mi kinachopikwa ndicho wote watakula.

Mtoto wangu hatembei miji ya watu na haruhusiwi kula kwa watu

Ikipikwa ugali atakula, yapikwe makande atakula
Maharagwe anayala kabla hayajatoka jikoni
Na hayo ndio malezi bora mkuu.
 
Wanawake wa hivi hawafai hata kidogo,ujue Mimi nikiachana na mke wangu nachukua na watoto wangu,huhitaji ushauri wewe,nashangaa hata waaokupa ushauri maana kinachokusukuma kwaenda mahakamani ni 2.8/M na sio malezi ya mtoto.

Roho yako iko radhi kuua MTU wewe.
 
-Je ulifunga naye ndoa?
  • ana familia/watoto wengine?
  • je una mpa nafasi ya kuonana na mtoto?
-Atunzi mtoto Kwa sbb ana hasira na wewe? CHANZO Nini?
- je umejaribu kutumia njia ya amani kupata fedha ya matunzo?

ANGALIZO:
Hakuna aliyewahi kufungwa kwa kuto toa matunzo.
Anaweza Kuwa na uwezo na Nia ya kutoa sema wewe njia unayotumia sio nzuri. Pengine unachochewa na marafiki,ndugu kwenda ustawi au mahakamani.Kama ni hivi basi una safari ndefu ya mahangaiko yasiyo na matumaini.

Unaweza Kuwa na hasira, chuki au uchungu na mwenzio, kama ni hivi hata maamuzi yako sehemu kubwa sio mazuri. Vaa uanamke, Kuwa na haiba ya kike. mwanaume atajirudi.
Na mtakuwa vizuri tu.

Hizi mambo zenu za usawa, sijui harakati, zina mjeruhi mtu mmoja mmoja Kwa wakati wake. Kisheria (ya zamani) pesa ya matunzo baba anatakiwa kulipa 1000 Kwa mwezi.Jipange!
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Kwa hiyo unahisi ukienda ustawi wa jamii utamegewa hata Robo tu ya huo mshahara?
 
Pambana lea mwanao, achana nae.

Ushawahi ona jogoo analea vifaranga? Wanaume hawaleagi, its nature....atahudumia mtoto Kama na wewe unamuhudumia, Kama uko tayari kufata matumizi ya mtoto guest endelea kumsumbua, Kama unajali utu wako pambana mwenyewe.....mlezi mkuu ni Mungu, mtoto atakua tu bila yeye.

Angalizo, akileta matumizi usikatae na usimlishe mtoto sumu kumuhusu.
Wewe utakuwa ni mke wa mtu tena unayejielewa.👍
 
Acheni kujitia umwamba, mnakuwa hamuwajengi watoto kwenye maadili mazuri.
Kwahiyo mnataka tuwalilie na kuwabembeleza kutoa matumizi?? Mimi binafsi ukishiriki kulea mwanao nitamweka karibu na wewe na nitakuwa namweleza kabisa baba yako anakulea.
Ila usipotunza na mimi sitahangaika na wewe including kumpa habari zako mtaonanaga akiwa mkubwa. Mwanaume anayejua wajibu wake hawezi acha kulea mwanae hata kama amegombana na mama yake.
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi TANESCO Engineer Grade 1 anapokea 2.8. Sasa naombeni msaada - Je, kwa mshahara huo naweza pata elfu 50 ustawi au wanadanganya?
Hao watoto pambana nao menyewe, ipo siku atawakumbuka na kuwapigia magoti, mifano halisi ipo mingi
 
Back
Top Bottom