Masikini umeandika kwa huruma hadi nimejisikia vibaya. Pole sana kama una roho ndogo Jf sio sehemu ya kuomba ushauri mpenzi.
Siku hizi JF imekuwa ya ovyo sio sehemu serious kabisa. Wanaume wa Jamii forum 90% ni wa ovyo wana roho mbaya na chuki kwa kila mwanamke. Wanapenda kuwatukana na kujudge wanawake bila hata kujua uhalisia.
Wanaume wa JF wao ishu za ndoa na watoto wanaona wanawake ndio wakosaji kiasi cha kuwatukana ni malaya na wafwata mali/hela kwa wanaume au umejibebesha mimba.
mama cutest nilichotaka kukwambia ni usiumie na comment za wapumbavu hawa na wala zisikupe shida na usijibizane nao wengi wana stress za maisha na tatizo la afya ya akili. Watatukana ila ndio ukweli huo.
Wewe kama ni mke wa ndoa na una cheti swala lako kaanzie bakwata huko utapata msaada na mwisho ugua pole ukishapona jishighulishe ulee wanao kwamwe usikubali kuambiwa uache kazi eti kaa nyumbani unaona madhara yake ndio hayo.