Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Uzee unatisha Mkuu, si uliona Baba yake Diamond alivyokuwa anaomba huruma ya Watanzania kuwa ametelekezwa na Mwanaye.

Na mbaya zaidi mtoto ambaye ulimtekeleza unakuta anafanikiwa maisha na wewe ndiyo unakuta hata ugali wa siku unashindwa kumudu kuupata.[emoji28]
Yule sio mzee ni muhuni aliyeishiwa nguvu za mwili. Wewe umeona wale wadogo zake diamond walivyo wengi. Baba yake diamond ana watoto zaidi 15. Kila mtoto na mama yake.
 
Yaàni ni maboss kwelikweli,mtu anapanga masharti Utasema yeye ndio mwenye hiyo nyumba,ukipika maharage anasema sitaki nataka nyama,ukipika nyama anasema nataka Chipsi,ukipika Chipsi anasema nataka samaki aaaaaah hakika hutu tuviumbe ni tusumbufu Sana....Nina kamoja hako kananimbiaga "mama,hii juice sijaipenda"yaàni hapo mie nimejipinda najua katafurahi ,naishia kuchokaa[emoji16][emoji16][emoji16]
Unakaambia leta. Unainywa halafu unapiga kimya.
 
siwezi mchukulia mwanaume kama Mungu na huku nmeomba jinsi ya kufanya asa kejeli matusi ya nini?? nikaomba basi na ajira mnisaidie nilee hawa watoto ni sabbau hujui behind ya haya mambo....kamwe siwez mfananaisha Mungu wangu na kitu chochote afu sahivi ndoa sio priority yangu kaka so usinikejeli kwa kuona nataka mume sijui kulalamika hapana



Una elimu gani?
 
Umeshauri vizuri lakini Huko Chini umeharibu.
Hakuna mambo ya laana na Dhambi kwenye uhalisia wa Maisha.
Wapo Watu wanatenda wajibu na Majukumu Yao na bado uzeeni wanapasuka, na wapo Watu wanatelekeza Watoto na kufanya Matendo ya hovyo na uzeeni wanaishi vizuri au Watoto waliowatelekeza wanawakumbuka na kuwatunza.
Ulichofanya ni kutishia Watu ili waogope.

Muhimu ni kusema, Watu wabebe majukumu yao, ukizaa tunza wanaokuhusu, lakini hiyo sio Guarantee ya kutopasuka uzeeni. Kuna wazee wamelea Watoto Kwa Hali na Mali na bado wametelekezwa na Wake na watoto wao.
Hahahaha................Sisi Wanaume bila kutishiwa tishiwa huwa tunajisahau kuwajibika.

Tujifunze kuwajibika na kubeba majukumu ya familia kama Baba
 
Usitumie mihemko kukabiliana na ishu hiyo.
Ukiweza ku-dili naye Kwa Akili na upendo utakula zaidi ya Nusu ya Mshahara wake.
Elewa kuwa Serikali haina uwezo wa kumpangia MTU matumizi ya Mshahara wake.
Hivyo hata angelipwa milioni 10 bado anaweza kumhudumia mtoto Kwa kiwango kidogo cha Pesa.
Hapo ni kucheza na Akili yake tuu. Ambapo. Hapo ndio pagumu Kwa sababu wewe(Wanawake) mnaona ni wajibu wake kumtunza mtoto wake Jambo ambalo ni kweli lakini akitoa hiyo 50k pia itahesabika anatimiza wajibu wake tuu licha ya kuwa anatoa Pesa ambayo utaona ni ndogo.

Ni ishu ya upendo, kama hampendi huyo mtoto au umemuwekea mazingira ya kutompenda mtoto lazima haya yajitokeze
kaka iko hivi huyu baba anamtaka mtoto mmoja ambaye ana miaka miwili aishi naye nikamwambia mtoto bado mdogo ataishi na nani akasema atamleta mdogo wake na mfanyakaz bas akamchukua mtoto ila issue inakuja mm kumwona mtoto ikawa shida siruhusiwi kumuona mwanangu mwishowe mdog wake akanambia wifi njoo mfwate mtoto sababu kaka anaonyesha picha sio nzuri kwa mtoto anabadilisha wanawake mbele ya mtoto mpaka dada wa kazi nikaonaga uongo siku nikaenda mchukua mtoto msichana wa kazi akanieleza yote mpaka ushahid wa picha anavyiingia wanawake ndan tofaut naona kiuwkel sikupendezwa nikapotezea nikamchukua mwanangu ndo jamaa kususa huduma ya watoto isitoshe jana nmepigiwa simu wamepelekana polisi alikuwa anambaka dada wa kazi asa unaweza jua mtot anakuwa kwenye mazingira gani akikaa na babaake
 
Yule sio mzee ni muhuni aliyeishiwa nguvu za mwili. Wewe umeona wale wadogo zake diamond walivyo wengi. Baba yake diamond ana watoto zaidi 15. Kila mtoto na mama yake.
Ila ni aibu kwa Mzee wa umri ule kwenda kulia lia shida kwa Mtoto ambaye alimtelekeza bila huduma.


Nasisi pia, tunatakiwa kukumbushana umuhimu na wajibu wetu wa kuwajibika Kama Vichwa vya Familia
 
mi sihitaji pesa yake naomba alete mahitaji ya watoto kila mwezi tu maan kuhusu pesa naonekana huku sijui nataka pesa no nataka mahitahi niweze msaidia mama majukumu apa maaan nimeletea familia na mamaangu hajaajiriwa anabangaiza tu



Hata kwenye mahitaji napo huwa mnawaandikia kwa kuwakomoa sababu ya kukosa kuwa na uchungu wa pesa.

Ni kama wanawake wengine akikaribishwa kula na Mwanaume anaagiza chakula cha gharama na kinywaji cha gharama wakati ingekuwa hela yake asingefanya hivyo.
Ndiyo maana wanaume wengine wakigundua hivyo mkifika quest house hamlali anakuwa na uchungu na hela yake kwa hiyo anakutia ili hela yake iende kwa haki.
 
Dah me nikajua utasema aamke, asali, aoge, awapende sana wanae , awaogeshe pia halafu ahamie kwako umsaidie kupambana na haya maisha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
inaleta tatizo kubwa sana hii kitu.. watoto wengi tuliozaliwa kwa michanganyo iliyochochewa na tabia chafu za wazazi wetu kutoboa kwenye maisha inakuwaga ni shughuli pevu sana kuna baraka fulani zinavurugwa japo zipo ila kuzifikia mpaka upambane sanaa
It's true
 
Miaka 15 nyuma nilimpenda binti nikamchumbia, wazazi wake wakanikataa kuwa mimi ni masikini, Kwa umri wetu na mahaba tukapanga nimbebeshe mimba ili wamfukuze kwao niyumie njia hiyo kumuoa, mtego ukabuma licha ya mimba wazazi wakakaza maisha yalikuwa mboga 7, nikakomaa kulea mimba hadi mtoto akazaliwa nikajitahidi kadri ya nilivyoweza kumhudumia mwanangu akiwa na Mama yake kwao.

Baada kama miaka3 upepo ukabadili mwelekeo baada ya Baba wa familia kufariki, na mama hakuwa na uzoefu wa Biashara. Biashara zikafa zilikuwa za usafirishaji(magari ya biashara) zikabaki nyumba tu 2 za wapangaji na familia ni kubwa.

Nikashangaa gharama za matumizi ya mtoto ikawa kubwa sana, nilikuwa natoa Tsh 50,000 kila mwezi. Mshahara wangu ulikuwa 200,000 sekta binafsi.. nikashangaa mtoto haishi kuugua kumbuka mtoto yuko wilayani huko siwezi mara zote kwenda kumuona, unga wa lishe uliokuwa unatumika week2 ukawa unatumika siku3, haipiti week mtoto anaumwa, amelazwa tuma pesa natuma ikafika kwa mwezi najikuta natumia zaidi 100,000 kwa mtoto, kumbe mtoto aligeuzwa kitega uchumi, nilikuja kugundua siku dada yangu nilipomtuma kimya kimya kwenda kumuona mtoto hospital baada ya kuambiwa kalazwa. Akamkuta kwa jirani ni mzima wa afya anacheza, ikabidi niende baada ya kupeleleza ndani ya miezi 3 mtoto hakuwahi hata kuugua wakati mimi nimeshatuma pesa mara3 ya matibabu.

Nilipogundua hilo, nikaacha kutoa pesa ya matumizi kwa mtoto, mgogoro ukaanza, wakaenda ustawi, nikaitwa, takribani mara 3 ndo nikaenda, baada ya kukaa na kutafuta ufumbuzi wakagoma kunielewa, tukaingia kwenye kupiga gharama, nikawapa kadi ya Bima, na nikaamuriwa kutoa Tsh 20,000 kwa mwezi na siwatumii anatakiwa akaichukue ustawi, nilitoa pesa kwa mwaka mmoja baadae wao wenyewe wakazira kwenda kuchukua pesa wakaomba tu tuyamalize. Yakaisha nikabaki kutoa matumizi kadri nitakavyopata na kujisikia.. kuna wanawake ni wakorofi sana ila yapowafika shingoni wanakuja kulia lia na kutaka huruma ya Jamii.
 
Unamchukulia poa mzee wako kisa eti laana za limwanamke acha hizo, anayeweza kumlaani ni aliyemzaa tu!

Zalisha pita kushoto na usiwahi kukumbuka hivi ndivyo real mens hufanya



Hata Kwa alomzaa ni mpaka iwepo sababu nzito ndipo laana impate mtu.
Na sio hivi hivi tu.
 
Watoto wapo real sana na wanakuaga na honest opinion. Anasema kitu kwa ukweli na si kwa lengo la kumfurahisha au kumkera mtu.

Hapo kwenye kutokupenda juisi amenikumbusha chuo DIT kunakuaga na mwanafunzi ambaye kazi yake ni kukagua vyakula vya cafeteria na canteen zote, akisema viko poa ndio vinauzwa kwa wanafunzi, akisema haviko poa, haviuzwi. Jamaa utasikia ameonja supu halafu anasema, hiki kiwango cha chumvi sijakipenda, ipo mbali sana ongeza😀😀
Dah huyo jamaa mbona kapangiwa kitengo kuzuri hivyo?huo utaratibu upo vyuo vyote au DIT pekee?
 
Duh! Pole Sana dadangu kea magumu unayopitia Mungu akufanyie wepesi jamani.

Nenda tu ustawi wa Jamii ukatapiganie haki za wanao
 
Masikini umeandika kwa huruma hadi nimejisikia vibaya. Pole sana kama una roho ndogo Jf sio sehemu ya kuomba ushauri mpenzi.
Siku hizi JF imekuwa ya ovyo sio sehemu serious kabisa. Wanaume wa Jamii forum 90% ni wa ovyo wana roho mbaya na chuki kwa kila mwanamke. Wanapenda kuwatukana na kujudge wanawake bila hata kujua uhalisia.
Wanaume wa JF wao ishu za ndoa na watoto wanaona wanawake ndio wakosaji kiasi cha kuwatukana ni malaya na wafwata mali/hela kwa wanaume au umejibebesha mimba.

mama cutest nilichotaka kukwambia ni usiumie na comment za wapumbavu hawa na wala zisikupe shida na usijibizane nao wengi wana stress za maisha na tatizo la afya ya akili. Watatukana ila ndio ukweli huo.

Wewe kama ni mke wa ndoa na una cheti swala lako kaanzie bakwata huko utapata msaada na mwisho ugua pole ukishapona jishighulishe ulee wanao kwamwe usikubali kuambiwa uache kazi eti kaa nyumbani unaona madhara yake ndio hayo.
Kama ana ndoa na alizaa ndani ya ndoa imekuaje akaachika na asipewe msaada? Unaposema.aende BAKWATA kuna sehemu kasema ye ni MUISLAM.

Stori yake ni fupi haya mengine angeyaweka kwenye uzi (sio comments) pengine angeshauriwa vyema
 
Kama ana ndoa na alizaa ndani ya ndoa imekuaje akaachika na asipewe msaada? Unaposema.aende BAKWATA kuna sehemu kasema ye ni MUISLAM.

Stori yake ni fupi haya mengine angeyaweka kwenye uzi (sio comments) pengine angeshauriwa vyema
ipo yote kweny uzi
 
Kumbe hadi kwenye ndoa mnapangiana!!
😅😅 ingia uyaone!
Japo nilimaanisha kwa mahusiano yasiyo rasmi/ndoa. Ukiniambia tu uko na mimba, kama hatukukubaliana basi nakupeleka mahakamani kwa kuniletea mimba bila ridhaa yangu
 
Back
Top Bottom