Miaka 15 nyuma nilimpenda binti nikamchumbia, wazazi wake wakanikataa kuwa mimi ni masikini, Kwa umri wetu na mahaba tukapanga nimbebeshe mimba ili wamfukuze kwao niyumie njia hiyo kumuoa, mtego ukabuma licha ya mimba wazazi wakakaza maisha yalikuwa mboga 7, nikakomaa kulea mimba hadi mtoto akazaliwa nikajitahidi kadri ya nilivyoweza kumhudumia mwanangu akiwa na Mama yake kwao.
Baada kama miaka3 upepo ukabadili mwelekeo baada ya Baba wa familia kufariki, na mama hakuwa na uzoefu wa Biashara. Biashara zikafa zilikuwa za usafirishaji(magari ya biashara) zikabaki nyumba tu 2 za wapangaji na familia ni kubwa.
Nikashangaa gharama za matumizi ya mtoto ikawa kubwa sana, nilikuwa natoa Tsh 50,000 kila mwezi. Mshahara wangu ulikuwa 200,000 sekta binafsi.. nikashangaa mtoto haishi kuugua kumbuka mtoto yuko wilayani huko siwezi mara zote kwenda kumuona, unga wa lishe uliokuwa unatumika week2 ukawa unatumika siku3, haipiti week mtoto anaumwa, amelazwa tuma pesa natuma ikafika kwa mwezi najikuta natumia zaidi 100,000 kwa mtoto, kumbe mtoto aligeuzwa kitega uchumi, nilikuja kugundua siku dada yangu nilipomtuma kimya kimya kwenda kumuona mtoto hospital baada ya kuambiwa kalazwa. Akamkuta kwa jirani ni mzima wa afya anacheza, ikabidi niende baada ya kupeleleza ndani ya miezi 3 mtoto hakuwahi hata kuugua wakati mimi nimeshatuma pesa mara3 ya matibabu.
Nilipogundua hilo, nikaacha kutoa pesa ya matumizi kwa mtoto, mgogoro ukaanza, wakaenda ustawi, nikaitwa, takribani mara 3 ndo nikaenda, baada ya kukaa na kutafuta ufumbuzi wakagoma kunielewa, tukaingia kwenye kupiga gharama, nikawapa kadi ya Bima, na nikaamuriwa kutoa Tsh 20,000 kwa mwezi na siwatumii anatakiwa akaichukue ustawi, nilitoa pesa kwa mwaka mmoja baadae wao wenyewe wakazira kwenda kuchukua pesa wakaomba tu tuyamalize. Yakaisha nikabaki kutoa matumizi kadri nitakavyopata na kujisikia.. kuna wanawake ni wakorofi sana ila yapowafika shingoni wanakuja kulia lia na kutaka huruma ya Jamii.