Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Yule sio mzee ni muhuni aliyeishiwa nguvu za mwili. Wewe umeona wale wadogo zake diamond walivyo wengi. Baba yake diamond ana watoto zaidi 15. Kila mtoto na mama yake.
 
Unakaambia leta. Unainywa halafu unapiga kimya.
 



Una elimu gani?
 
Hahahaha................Sisi Wanaume bila kutishiwa tishiwa huwa tunajisahau kuwajibika.

Tujifunze kuwajibika na kubeba majukumu ya familia kama Baba
 
kaka iko hivi huyu baba anamtaka mtoto mmoja ambaye ana miaka miwili aishi naye nikamwambia mtoto bado mdogo ataishi na nani akasema atamleta mdogo wake na mfanyakaz bas akamchukua mtoto ila issue inakuja mm kumwona mtoto ikawa shida siruhusiwi kumuona mwanangu mwishowe mdog wake akanambia wifi njoo mfwate mtoto sababu kaka anaonyesha picha sio nzuri kwa mtoto anabadilisha wanawake mbele ya mtoto mpaka dada wa kazi nikaonaga uongo siku nikaenda mchukua mtoto msichana wa kazi akanieleza yote mpaka ushahid wa picha anavyiingia wanawake ndan tofaut naona kiuwkel sikupendezwa nikapotezea nikamchukua mwanangu ndo jamaa kususa huduma ya watoto isitoshe jana nmepigiwa simu wamepelekana polisi alikuwa anambaka dada wa kazi asa unaweza jua mtot anakuwa kwenye mazingira gani akikaa na babaake
 
Yule sio mzee ni muhuni aliyeishiwa nguvu za mwili. Wewe umeona wale wadogo zake diamond walivyo wengi. Baba yake diamond ana watoto zaidi 15. Kila mtoto na mama yake.
Ila ni aibu kwa Mzee wa umri ule kwenda kulia lia shida kwa Mtoto ambaye alimtelekeza bila huduma.


Nasisi pia, tunatakiwa kukumbushana umuhimu na wajibu wetu wa kuwajibika Kama Vichwa vya Familia
 
mi sihitaji pesa yake naomba alete mahitaji ya watoto kila mwezi tu maan kuhusu pesa naonekana huku sijui nataka pesa no nataka mahitahi niweze msaidia mama majukumu apa maaan nimeletea familia na mamaangu hajaajiriwa anabangaiza tu



Hata kwenye mahitaji napo huwa mnawaandikia kwa kuwakomoa sababu ya kukosa kuwa na uchungu wa pesa.

Ni kama wanawake wengine akikaribishwa kula na Mwanaume anaagiza chakula cha gharama na kinywaji cha gharama wakati ingekuwa hela yake asingefanya hivyo.
Ndiyo maana wanaume wengine wakigundua hivyo mkifika quest house hamlali anakuwa na uchungu na hela yake kwa hiyo anakutia ili hela yake iende kwa haki.
 
Dah me nikajua utasema aamke, asali, aoge, awapende sana wanae , awaogeshe pia halafu ahamie kwako umsaidie kupambana na haya maisha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
It's true
 
Miaka 15 nyuma nilimpenda binti nikamchumbia, wazazi wake wakanikataa kuwa mimi ni masikini, Kwa umri wetu na mahaba tukapanga nimbebeshe mimba ili wamfukuze kwao niyumie njia hiyo kumuoa, mtego ukabuma licha ya mimba wazazi wakakaza maisha yalikuwa mboga 7, nikakomaa kulea mimba hadi mtoto akazaliwa nikajitahidi kadri ya nilivyoweza kumhudumia mwanangu akiwa na Mama yake kwao.

Baada kama miaka3 upepo ukabadili mwelekeo baada ya Baba wa familia kufariki, na mama hakuwa na uzoefu wa Biashara. Biashara zikafa zilikuwa za usafirishaji(magari ya biashara) zikabaki nyumba tu 2 za wapangaji na familia ni kubwa.

Nikashangaa gharama za matumizi ya mtoto ikawa kubwa sana, nilikuwa natoa Tsh 50,000 kila mwezi. Mshahara wangu ulikuwa 200,000 sekta binafsi.. nikashangaa mtoto haishi kuugua kumbuka mtoto yuko wilayani huko siwezi mara zote kwenda kumuona, unga wa lishe uliokuwa unatumika week2 ukawa unatumika siku3, haipiti week mtoto anaumwa, amelazwa tuma pesa natuma ikafika kwa mwezi najikuta natumia zaidi 100,000 kwa mtoto, kumbe mtoto aligeuzwa kitega uchumi, nilikuja kugundua siku dada yangu nilipomtuma kimya kimya kwenda kumuona mtoto hospital baada ya kuambiwa kalazwa. Akamkuta kwa jirani ni mzima wa afya anacheza, ikabidi niende baada ya kupeleleza ndani ya miezi 3 mtoto hakuwahi hata kuugua wakati mimi nimeshatuma pesa mara3 ya matibabu.

Nilipogundua hilo, nikaacha kutoa pesa ya matumizi kwa mtoto, mgogoro ukaanza, wakaenda ustawi, nikaitwa, takribani mara 3 ndo nikaenda, baada ya kukaa na kutafuta ufumbuzi wakagoma kunielewa, tukaingia kwenye kupiga gharama, nikawapa kadi ya Bima, na nikaamuriwa kutoa Tsh 20,000 kwa mwezi na siwatumii anatakiwa akaichukue ustawi, nilitoa pesa kwa mwaka mmoja baadae wao wenyewe wakazira kwenda kuchukua pesa wakaomba tu tuyamalize. Yakaisha nikabaki kutoa matumizi kadri nitakavyopata na kujisikia.. kuna wanawake ni wakorofi sana ila yapowafika shingoni wanakuja kulia lia na kutaka huruma ya Jamii.
 
Unamchukulia poa mzee wako kisa eti laana za limwanamke acha hizo, anayeweza kumlaani ni aliyemzaa tu!

Zalisha pita kushoto na usiwahi kukumbuka hivi ndivyo real mens hufanya



Hata Kwa alomzaa ni mpaka iwepo sababu nzito ndipo laana impate mtu.
Na sio hivi hivi tu.
 
Dah huyo jamaa mbona kapangiwa kitengo kuzuri hivyo?huo utaratibu upo vyuo vyote au DIT pekee?
 
Duh! Pole Sana dadangu kea magumu unayopitia Mungu akufanyie wepesi jamani.

Nenda tu ustawi wa Jamii ukatapiganie haki za wanao
 
Kama ana ndoa na alizaa ndani ya ndoa imekuaje akaachika na asipewe msaada? Unaposema.aende BAKWATA kuna sehemu kasema ye ni MUISLAM.

Stori yake ni fupi haya mengine angeyaweka kwenye uzi (sio comments) pengine angeshauriwa vyema
 
Kama ana ndoa na alizaa ndani ya ndoa imekuaje akaachika na asipewe msaada? Unaposema.aende BAKWATA kuna sehemu kasema ye ni MUISLAM.

Stori yake ni fupi haya mengine angeyaweka kwenye uzi (sio comments) pengine angeshauriwa vyema
ipo yote kweny uzi
 
Kumbe hadi kwenye ndoa mnapangiana!!
😅😅 ingia uyaone!
Japo nilimaanisha kwa mahusiano yasiyo rasmi/ndoa. Ukiniambia tu uko na mimba, kama hatukukubaliana basi nakupeleka mahakamani kwa kuniletea mimba bila ridhaa yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…