Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Ni kweli Mkuu, lakini kama Mwanamke ameamua kulazimisha kubaki na Mtoto/Watoto basi huna budi Mwanaume kutenga fedha kwaajili ya kumhudumia damu yako ili mtoto asipate tabu.

Sio vizuri Watoto wapate shida na Wazazi mpo hai, ukiona hutaki kuongea na mtalaka wako fungua Akaunti uwe unatumbukiza hela ya matumizi pamoja labda na ada kila mwisho wa mwezi kwaajili ya Mtoto wako.
Kama hawezi kuwalea kwanini alazimishe kubaki nao?
Kama nitahitaji wanangu alafu ukawazuia bila sababu ya msingi, hakika utalea mwenyewe.
Siyo kutuletea "vitisho ooh fainali uzeeni" kama vile nyie ndiyo Mungu

Tunasubiri tu hiyo fainali uzeeni ije vyovyote🤣
 
Umeongea ujinga
Ujinga wangu ndio hekima yako, na hekima yangu ndio ujinga wako. Kubali kutofautiana. Kutokukubali kutofautiana ndio kunakufanya uonekane mpumbavu zaidi.
 
umalaya wako na kuzaaa bila ndoa vimekufikisha hapo..tamaaa mbaya sana!!!I ona sasa wanataabika watoto Kwa upumbavu wako.

Mpe mtoto wake uyo mwanaume aleee mwenyewe..usigeuze mtoto kama mtaji...ww inaonekana ulimtegea mimba sabb ya huo mshahara...imekula kwako😂😂😂😂
Duh
 
Ujinga ni upi hapo?Mueleze mtu ukweli na ajitambue.Mnakaa mnawadanganya hovyo,kuwasomea vijisheria vya kipuuzi bila kuwafundisha kujisimamia na kuyakabili majukumu.Mnawarembea mwandiko habari za huzuni?Mnawazubaisha na kuwafanya wasiwe responsibles kwa mambo yaliyowakuta,wanayoyaishi na hamuwapi positive options!
Nimemshangaa yaani. Sio Kila haki ni ya kugombaniwa. Huyo baba mtoto angefariki mtoto angeishije?

Ndio maana tunazalisha wanawake wengi wanaoamini hawawezi kujisimamia wala kujihudumia.
 
Ulizaa mtoto Kwa kuhitaji uwe na mtoto au kumridhisha huyo mwanaume?

Lea mwanao! Angekufa ungeenda kulishtaki kaburi?

Fanya kama hayupo, Lea bila huzuni, ona mwanao ni baraka kuu.

Sali na mtegemee Mungu, atakupa riziki ya mtoto wako.

Ukianza habari za ustawi wa jamii, utapauka Kwa stress, huo muda angalia shughuli ya kufanya.

Mwanaume wa kweli na mtu mzima, hakumbushwi kulea damu yake.
Ifanyiwe lamination hii
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Nimemshangaa yaani. Sio Kila haki ni ya kugombaniwa. Huyo baba mtoto angefariki mtoto angeishije?

Ndio maana tunazalisha wanawake wengi wanaoamini hawawezi kujisimamia wala kujihudumia.
Kwaiyo watoto waishi kama yatima na wakati baba Yuko hai??umeshawahi pitia au kuona ugumu wa uyatima Kwa watu wa karibu?mifano km hii sio mizuri
 
Na wamebaki kuiishi slogan ya kipuuzi sana eti..."Mwanamke akiwezeshwa anaweza"...!Wasisubiri kuwezeshwa.Wajifunze kuyaishi maisha kwa uhalisi wake.
 
siwezi mchukulia mwanaume kama Mungu na huku nmeomba jinsi ya kufanya asa kejeli matusi ya nini?? nikaomba basi na ajira mnisaidie nilee hawa watoto ni sabbau hujui behind ya haya mambo....kamwe siwez mfananaisha Mungu wangu na kitu chochote afu sahivi ndoa sio priority yangu kaka so usinikejeli kwa kuona nataka mume sijui kulalamika hapana
Angalia unaweza kufanya Nini Anza nacho, maisha hayajawahi kuwa rahisi, ila ni magumu zaidi ukikaa kufikiria na kimuhuzunika Kwa jambo ambalo huwezi kulibadilisha. Yaliyopita yamepita anzia ulipo.

Watoto wafanye njia yako ya mafanikio. Amka usiku Sali, omba toba, jikabidhi Kwa Mungu na wakabidhi watoto wako Kwa Mungu. Ongea na Mungu kama alivyokupa huo mtihani basi akuoneshe na njia ya kuuvuka. Omba Mungu akupe riziki ya wanao.

Omba Mungu akufunue upate biashara au kazi.

Kuwa na tabia ya kusali usiku mwingi, kwanza utaipata amani ambayo hujaipata muda mrefu, pili utaweza kutafakari uanzie wapi.

Anza na Chochote, utafanikiwa. Huyu aliyeacha kuhudumia ni mtu mzima anajua kama ana watoto na wewe. Achana nae.
 
Kwaiyo watoto waishi kama yatima na wakati baba Yuko hai??umeshawahi pitia au kuona ugumu wa uyatima Kwa watu wa karibu?mifano km hii sio mizuri
Ninasomesha mtoto sekondari, na baba yake yupo hai. Naongea nachokiishi. Nimeona faida ya kulia lia na faida ya kutulia na kupokea mtoto kama baraka na baraka zinamiminika kweli kweli
 
Wewe mama ukiwa wapi?Unelaelewa maana ya mtoto yatima?
Inawezekana sielew lakini Haina mantiki kusema et baba angefariki ingekuwaje Bora kumshauri atafute kazi alee wanae hakuna nafas ya kureplace malez ya watoto km ikiwa mmoja hajawajibika haijalishi Yuko hai au amekufa tayar ni doa Kwa watoto na hata kwenye malez hawawez kuwa sawa
 
Angalia unaweza kufanya Nini Anza nacho, maisha hayajawahi kuwa rahisi, ila ni magumu zaidi ukikaa kufikiria na kimuhuzunika Kwa jambo ambalo huwezi kulibadilisha. Yaliyopita yamepita anzia ulipo.

Watoto wafanye njia yako ya mafanikio. Amka usiku Sali, omba toba, jikabidhi Kwa Mungu na wakabidhi watoto wako Kwa Mungu. Ongea na Mungu kama alivyokupa huo mtihani basi akuoneshe na njia ya kuuvuka. Omba Mungu akupe riziki ya wanao.

Omba Mungu akufunue upate biashara au kazi.

Kuwa na tabia ya kusali usiku mwingi, kwanza utaipata amani ambayo hujaipata muda mrefu, pili utaweza kutafakari uanzie wapi.

Anza na Chochote, utafanikiwa. Huyu aliyeacha kuhudumia ni mtu mzima anajua kama ana watoto na wewe. Achana nae.
asante sana kiukwel umenipa ushauri mzuri sana Mungu akubariki
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Ninasomesha mtoto sekondari, na baba yake yupo hai. Naongea nachokiishi. Nimeona faida ya kulia lia na faida ya kutulia na kupokea mtoto kama baraka na baraka zinamiminika kweli kweli
Wewe uliweza lakini sio kilamtu ana weza kuwa wewe hebu elezea baada ya kupitia hali hiyo Ulijisikiaje moyoni japo uliweza kufanya hivo?Naamini ulianzia huku anakopita mtoa mada na ilivhukua muda kusimama
 
Angalia unaweza kufanya Nini Anza nacho, maisha hayajawahi kuwa rahisi, ila ni magumu zaidi ukikaa kufikiria na kimuhuzunika Kwa jambo ambalo huwezi kulibadilisha. Yaliyopita yamepita anzia ulipo.

Watoto wafanye njia yako ya mafanikio. Amka usiku Sali, omba toba, jikabidhi Kwa Mungu na wakabidhi watoto wako Kwa Mungu. Ongea na Mungu kama alivyokupa huo mtihani basi akuoneshe na njia ya kuuvuka. Omba Mungu akupe riziki ya wanao.

Omba Mungu akufunue upate biashara au kazi.

Kuwa na tabia ya kusali usiku mwingi, kwanza utaipata amani ambayo hujaipata muda mrefu, pili utaweza kutafakari uanzie wapi.

Anza na Chochote, utafanikiwa. Huyu aliyeacha kuhudumia ni mtu mzima anajua kama ana watoto na wewe. Achana nae.
Huu ndo ushauri wa maana dear
 
Naona wakuu wengi wanaonyesha hisia kwamba mwanaume atakuwa na tatizo.
Mimi ninashaka na uandishi huu wa harakaharaka,nahisi kuna tatizo mahali kwa huyu mama mtoto.
Maana katika uandishi wake ameonyesha hisia kwenye pesa tuu na wala sio maridhiano kwa ajili ya malezi bora ya mtoto.
Unajua ukiwa kiburi mwanaume hutomuona hata huko ustawi.
Waulize hao ustawi watakwambia.
Ushazaa nae,epuka kutangaza migogoro yenu kwa watu,muite taratibu kwa hisia ataitika.
Wanaume tunapenda mwanamke mpole na mnyeyekevu,huwa tunapoa kabisaa kama mfupa kwa fisi.
Hakuna mwanaume anayekubali kutawaliwa na ke hayupoo
 
Wewe uliweza lakini sio kilamtu ana weza kuwa wewe hebu elezea baada ya kupitia hali hiyo Ulijisikiaje moyoni japo uliweza kufanya hivo?
Nikikueleza itakusaidia Nini? Kama hujaelewa nilichoandika hapo huwezi kuelewa Tena.

Unadhani huko ustawi atapata anachotaka? Anaweza kwenda na mwanaume akasema uwezo wake ni elfu kumi tu Kwa mwezi. Hawalazimishi.

Tujifunze kuupokea na kuukubali ukweli. Mtoto ni wa baba na mama.

Angekufa angeenda kaburini kudai mahitaji?
 
Usisikilize ushauri wa ndugu,marafiki na majirani. Wewe isikilize sauti ya mtoto wako.
Jamii huwa wanampump mtu halafu wao wanakaa pembeni na hawakusaidii kulea.
Mtafte taratibu mzazi mwenzio,akiona umeonyesha heshima atashuka na mtazungumza
 
Nikikueleza itakusaidia Nini? Kama hujaelewa nilichoandika hapo huwezi kuelewa Tena.

Unadhani huko ustawi atapata anachotaka? Anaweza kwenda na mwanaume akasema uwezo wake ni elfu kumi tu Kwa mwezi. Hawalazimishi.

Tujifunze kuupokea na kuukubali ukweli. Mtoto ni wa baba na mama.

Angekufa angeenda kaburini kudai mahitaji?
Ngoja tuishie hapa
 
asante sana kiukwel umenipa ushauri mzuri sana Mungu akubariki
Karibu mumy...amka Sali, oga pendeza, wapende sana wanao. Mafanikio sio rahisi ila pia sio magumu na lazima upitie changamoto ili uyafikie.
 
Inawezekana sielew lakini Haina mantiki kusema et baba angefariki ingekuwaje Bora kumshauri atafute kazi alee wanae hakuna nafas ya kureplace malez ya watoto km ikiwa mmoja hajawajibika haijalishi Yuko hai au amekufa tayar ni doa Kwa watoto na hata kwenye malez hawawez kuwa sawa
Wanawake bado mna changanoto sana na kuishi mazoea.Wengi wenu hata mkiwa na uwezo wa kutunza mtoto/watoto bado hamridhiki.Mtatafuta namna ya kuendeleza uchokozi,kero,madai na usumbufu wa kila aina hata kama mwanaume/baba wa mtoto hana hela.Sijui ndivyo mlivyoumbwa au ni kujiendekeza tu?
 
Back
Top Bottom