Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Hakuna sheria inayosema utapigiwa hesabu ya Mama na mtoto, haipo.. huyo Mama wa mtoto ni mtu mzima na ana wazazi wake na yeye, mkishafika Ustawi. Wanaangalia umri wa mtoto na mahitaji yake ya msingi. Wataangalia kama anakunwa uji kwa mwezi unga na sukari ni sh ngapi, nguo, sabuni, mafuta, nauli ya kwenda clinic mara moja, kama Jamaa ni mtumishi mtoto ana bima tayari hapo kwenye matibabu halambi hata 100 mbovu.. ikipigwa hesabu haiwezi kufika Tsh 100,000 kwa mwezi, hata kama ana mshahara wa milioni 10 haihusiani.. ndo maana wenye Akili huwa wanajishusha tu na kuwa wapole kuna wakati Baba anaweza kutoa pesa kuliko hiyo.. ila ukimpeleka ustawi ndo umemtibua kabisa.. ingekuwa ulaya huko sawa lakini kibongo bongo sijui hata kama ipo sheria ya kumfunga jela mwanamme aliyekataa kuhudumia mtoto..

Na ndicho nilichokuwa nasema,
Na hakuna Mtoto anayeweza kumaliza hiyo 100,000/= Kwa mwezi Kwa matumizi ya kawaida. Wengi huishi 50k - 70k
Alafu sasa igawanywe Kwa Watu Wawili yaani Baba na Mama wote wachangie hiyo Pesa.
 
Ulizaa mtoto Kwa kuhitaji uwe na mtoto au kumridhisha huyo mwanaume?

Lea mwanao! Angekufa ungeenda kulishtaki kaburi?

Fanya kama hayupo, Lea bila huzuni, ona mwanao ni baraka kuu.

Sali na mtegemee Mungu, atakupa riziki ya mtoto wako.

Ukianza habari za ustawi wa jamii, utapauka Kwa stress, huo muda angalia shughuli ya kufanya.

Mwanaume wa kweli na mtu mzima, hakumbushwi kulea damu yake.
Nimekuelewa vyema sana [emoji4]
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Calm down, you shall overcome someday
mnanikejeli sana mimi kuomba msaada basi naombeni mnisamehe nina roho ndogo sana naumia kwa kunidhihaki nisameheni pengine sikupaswa kuomba ushauri samahanini ilanjueni sijazaa bila ndoa nmezaa kwa ndoa kabisa
 
Naona wakuu wengi wanaonyesha hisia kwamba mwanaume atakuwa na tatizo.
Mimi ninashaka na uandishi huu wa harakaharaka,nahisi kuna tatizo mahali kwa huyu mama mtoto.
Maana katika uandishi wake ameonyesha hisia kwenye pesa tuu na wala sio maridhiano kwa ajili ya malezi bora ya mtoto.
Unajua ukiwa kiburi mwanaume hutomuona hata huko ustawi.
Waulize hao ustawi watakwambia.
Ushazaa nae,epuka kutangaza migogoro yenu kwa watu,muite taratibu kwa hisia ataitika.
Wanaume tunapenda mwanamke mpole na mnyeyekevu,huwa tunapoa kabisaa kama mfupa kwa fisi.
Hakuna mwanaume anayekubali kutawaliwa na ke hayupoo
mkuu umemweleza ukwel shida uyu single maza anataka aambiwe anachopenda kusikia yy..hataki ukwel na ukimweleza ukwel anakuchukulia tofauti..

Nishaona masingle Maza flani na ma feminist wanamfariji as if yy Hana shida..kiukwel wanazidi mpoteza na atapotea jumla..hataki maridhiano analilia tu kupewa fungu Kila mwisho mwenz...mke anaejitambua angekua anafight how arudi Kwa mme wake na sio kulilia pesa!!!
 
Wewe sasa ndio wale wapotoshaji tunaowaongelea hapa kila siku. Hapo akisemwa baba mtoto wa huyo mwanamke ndicho unachotaka kukisikia. Ila anapohojiwa mwanamke basi sisi ni roho mbaya, wakorofi, hatujielewi, tunatukana.

Hii mentality ya kuamini mwanamke always yupo right ilijengwa na kizazi cha wanaume waliokuwa wanakumbatiwa sana na mabibi na mama zao maisha yao ya utotoni muda mwingi. Wanaume hawa wakabeba vinasaba vya kike wakiona mwanamke anasemwa kwa mabaya na uzembe wake na wao wanajikuta automatically wanajiskia kama wanashambuliwa na kutukanwa yote hii ni matokeo ya kubeba akili ya kike.

Sasa wanaume wa miaka hii wamekuzwa kitofuti na wanaweza kutambua mipaka ya haki ndio maana unaona hata mtu aje na story kuwa mwanaume alimkatakata mapanga watataka kujua huyo mwanaume ulimfanya nini hadi afikie hatua hiyo kabla hawajaanza kukuonea huruma na kuleta hisia za kutetea mwanamke kwasababu ya kutambulishwa kama kiumbe dhaifu kwenye jamii ile hali kuwa si kweli.

Nadhani ifike wakati tuanze kujua na kutambua haki yako inapoishia ndipo ya mwenzako inaanzia so its very important kujua mipaka. Wanawake hamna mipaka na haki zenu ndio maana mnajikuta mara nyingi sana mpo katika eneo la mwanaume na hapo mwanaume akiwasha moto mnasema ni mkorofi sababu unahaki ya kuingia katika haki za mwanaume na kuchukua unachotaka.

Nitakupa mfano, wewe unaweza kutana na mwanaume ana muonekano mzuri na ana uwezo wa kifedha. Ikatokea ukaanza kujijengea fikra kuwa ukiweza kumrubuni kimahaba akakukubalia wewe kuingia himaya yake na kutumia mali zake kujinufaisha wewe binafsi then hapo unakuwa umeshaanza kuvuka mipaka ya haki. Kwann uanzishe mahusiano kwa misingi ya tamaa za mali?

Ukijastukia ni baadae umejitegesha ujauzito, mnapata mtoto unaanza sasa kuwa direct kudai kwa kulazimisha kutumia mali za mwanaume kulea mtoto ambaye wewe kwa tamaa zako ndie ulisababisha kutengenezwa na mwanaume kakushitukia sasa ndio maana unaona balaa linakuwakia.

Mabinti/wanawake wa sasa tamaa zenu ndio mtaji wa maisha na hiki ndicho kinawaliza kila siku sio wanaume. Someni vitabu vya MUNGU kila wasaa mnaopata sio kusoma post za kidangaji huko mitandaoni ili akili zenu ziwe safi muweze kuamua kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU sio kwa uwezo wa UROHO MTAKATIFU.
Hao ni Pipa na mfuniko, ye naye kazalishwa tu yupo yupo
 
AMRI KUMI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana MUNGU wako usiabudu miungu wengine
2. Usitaje bure jina la MUNGU wako
3. Shika kitakatifu siku ya MUNGU
4. Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani
5. Usiue
6. Usizini
7. Usiibe
8. Usiseme uongo
9. Usitamaman mwanamke/mwanaume asie mke/mme wako
10. Usitamani mali za watu
Hizo sio Amri za Mungu na hazijawahi kuwa.
We umeenda kuzitoa kwenye kidaftari cha RC
 
Usisikilize ushauri wa ndugu,marafiki na majirani. Wewe isikilize sauti ya mtoto wako.
Jamii huwa wanampump mtu halafu wao wanakaa pembeni na hawakusaidii kulea.
Mtafte taratibu mzazi mwenzio,akiona umeonyesha heshima atashuka na mtazungumza
Ashasema ndoa sio priority yake,,asa nazani unaelewa ni mwanamke wa aina gani uyu...
 
asante member barikiwa

Usitumie mihemko kukabiliana na ishu hiyo.
Ukiweza ku-dili naye Kwa Akili na upendo utakula zaidi ya Nusu ya Mshahara wake.
Elewa kuwa Serikali haina uwezo wa kumpangia MTU matumizi ya Mshahara wake.
Hivyo hata angelipwa milioni 10 bado anaweza kumhudumia mtoto Kwa kiwango kidogo cha Pesa.
Hapo ni kucheza na Akili yake tuu. Ambapo. Hapo ndio pagumu Kwa sababu wewe(Wanawake) mnaona ni wajibu wake kumtunza mtoto wake Jambo ambalo ni kweli lakini akitoa hiyo 50k pia itahesabika anatimiza wajibu wake tuu licha ya kuwa anatoa Pesa ambayo utaona ni ndogo.

Ni ishu ya upendo, kama hampendi huyo mtoto au umemuwekea mazingira ya kutompenda mtoto lazima haya yajitokeze
 
Hizo sio Amri za Mungu na hazijawahi kuwa.
We umeenda kuzitoa kwenye kidaftari cha RC
Ziweke hizo ambazo hazipo kwenye kidaftari cha RC..!! Yaani mimi Mu-RC unataka nikachukue kwenye kidaftari cha dhehebu gani? Weka basi zako
 
Hapana,
Kwani kalenda ya uzazi Mungu kaiweka kwa nani kati ya Mwanaume na mwanamke?
Hivyo anayetakiwa kuchukua tahadhari Kwa kujijua zaidi ni nani ?

Ikitokea vinginevyo mhanga atakuwa nani?

Je huwa wanakubaliana kuzaa?
Suala la uzazi wa mpango ni shirikishi, ukimwachia Mwanamke peke yake linaweza kuwa zito mwisho mkajikuta mnapata watoto ambao hamkupanga kuwapata.

Na ukishapata watoto ni wajibu wako Mume kumlea huyo mtoto kwa kuhakikisha anapata huduma zote muhimu.
 
Naombeni msaada nataka kwenda ustawi, baba wa watoto huduma ananisumbua maana ni mfanyakazi serikalini iko hivi

iko hivi mimi nmeolewa na tuna miaka 4 na nusu ya ndoa now nina miaka 24 ex husband ako na 31 ...ye ni engneer tanesco kipindi tunaowana sikukaa sana naona ni saba ile nikabeba mimba nikajifungua mtoto wa kwanza ..nikaja beba mimba nikajifungua wa pili siwezi sema mimi ndo nina matatizo au yeye maan nitakuwa nakosea pengine mimi nilikosea au yeye pia alinikosea maan nikisema alinifanya hivi sijui vile ntakuwa pengine namponda yeye kumbe shida ninayo mm ila mimi ndiye nikawa naumia kila nikijitahid kurekebisha ilishindikana basi tukawa tunaishi ndan kama watu hawajuani chuki yule baba kwangu ndo ilizidi maan nahis alinichoka zaidi kutokana na kuwa kinyume nae baadhi ya mambo yake ambayo sikuona sahihi au kutokana na tofaut zetu ukimwambia hiki tunaishia kulumbana kutokana na pengine tuliyopitia tulichokana ila mimi kama mm nilivumilia sababu ya mtoto apo nina mimba miez 7 ikafikia hatua mbaya mpaka napigiwa simu na manzi za nje zinanitukana nilipata pressure ya mimba nikajifungua siku ambazo sio makadirio nilijifungua week 29 mtoto njiti na siku najifungua hakuwa nyumban alilala kwa manzi zake alipigiwa simu na nesi alete vifaa hosptal kwa maan kabla ya kuingia theatre niliandika namba za wadhamin wawili na sikwenda kwa nia ya kujifungua ila nilikwenda kama clinic ndo pressure ikanishika ikabidi nikimbizwe op fasta basi nilipozinduka nilimuona hosp na mama yang na baadhu ya ndug zake apo mtoto alikuwa yupo kwenye incubeta ile ya kupumulia tulikaa sana hosp bas baada ya kuruhusiwa nilikaa week mbili alinipa talaka kwamba hanitaki ye anataka kuoa niende kwetu nikawasiliana na kwao tulikaa kikao ila alionekana mkorofi sana bas mpaka hivi navoongea mamaangu kajitoa kabisa kwenye maswala ya kesi yetu nipo napambana mwenyew ila kinachonifanya nipambane naye kwa sasa hali yangu haijaimarika sana kutokana na op nilifanyiwa mbili ya mtoto na ya hernia ya kitovu ambapo huko nyuma nilipata op ya nje ya kizazi na ya mtoto wa kwanza jumla ninayo mishono 4 kwa muda mfupi kwahiy sikukava sana hivo mamaangu analalamika anaelemewa sababu mamaangu ni kibarua tu hana biashara ya ajira ila yeye tulivyoachana alinitamkia sitapata chochote sikuhangaika maan tulijenga tukifanya maendeleo tukiwa wote sikutak kusumbuana nae kwenye mali maan niliamini ipo siku ningepata mali zangu na mimi je (nyie mnaosema nimefwata mali je ningeshindwa enda bakwata kudai mali zang?? msipende mtukan mtu hamjui nachopitia maan cheti ninacho na kuhus msharah alikuwa ananambia mpk siku anapandishwa cheo alinionyesha karatas kabisa ya ofisi mmenitukana san



cha mwisho nilitak kupambania haki za watoto tu
kabila gani hizo zinakataa watoto aisee
Wanawake msiforce wanaume kufuata mipango yenu
 
Hakuna sheria inayosema utapigiwa hesabu ya Mama na mtoto, haipo.. huyo Mama wa mtoto ni mtu mzima na ana wazazi wake na yeye, mkishafika Ustawi. Wanaangalia umri wa mtoto na mahitaji yake ya msingi. Wataangalia kama anakunwa uji kwa mwezi unga na sukari ni sh ngapi, nguo, sabuni, mafuta, nauli ya kwenda clinic mara moja, kama Jamaa ni mtumishi mtoto ana bima tayari hapo kwenye matibabu halambi hata 100 mbovu.. ikipigwa hesabu haiwezi kufika Tsh 100,000 kwa mwezi, hata kama ana mshahara wa milioni 10 haihusiani.. ndo maana wenye Akili huwa wanajishusha tu na kuwa wapole kuna wakati Baba anaweza kutoa pesa kuliko hiyo.. ila ukimpeleka ustawi ndo umemtibua kabisa.. ingekuwa ulaya huko sawa lakini kibongo bongo sijui hata kama ipo sheria ya kumfunga jela mwanamme aliyekataa kuhudumia mtoto..

Nilikuwa namaanisha, kama gharama ni 100,000/= basi mwanaume atachangia Nusu na Mwanamke Nusu. Full stop,
Mtoto ni wawote
 
Ashasema ndoa sio priority yake,,asa nazani unaelewa ni mwanamke wa aina gani uyu...
tatiz unajibu bila kuelewa unajua uyo alisemaje nikamjibu ivo inshort kwa sasa sihitaji kuolewa priority ni kuwalewa watoto wangu period..

maan uyo kaongelea sijui kama utaolewa mara sijui hamna wa kukuoa thus y nikasema ivo kama sikuandikiwa kuolewa hata nifanyaje siwez pata io ndoa basi
 
Naona wakuu wengi wanaonyesha hisia kwamba mwanaume atakuwa na tatizo.
Mimi ninashaka na uandishi huu wa harakaharaka,nahisi kuna tatizo mahali kwa huyu mama mtoto.
Maana katika uandishi wake ameonyesha hisia kwenye pesa tuu na wala sio maridhiano kwa ajili ya malezi bora ya mtoto.
Unajua ukiwa kiburi mwanaume hutomuona hata huko ustawi.
Waulize hao ustawi watakwambia.
Ushazaa nae,epuka kutangaza migogoro yenu kwa watu,muite taratibu kwa hisia ataitika.
Wanaume tunapenda mwanamke mpole na mnyeyekevu,huwa tunapoa kabisaa kama mfupa kwa fisi.
Hakuna mwanaume anayekubali kutawaliwa na ke hayupoo
Mimi aliposema sina shida ya Ndoa ndipo nikastuka na waza tofauti zaidi. Mwanamke ambaye haheshimu na kuitambua ndoa kama taasisi nyetu na priority yake katika Maisha mtazame mara mbili mbili akiwa anazungumzia mahusiano.

Ndoa ndio taasisi namba moja ya mwanamke. Vyote anavyovitafuta hapa Duniank vipo humo. Inastaajabisha sana wanawake wa kisasa kwa wingi wanaidharau sana Ndoa na kuiona kama sehemu ya kupita au kuipuuza ile hali wanataka faida zake.

Watoto huzaliwa ndani ya ndoa sio nje ya ndoa. Matumizi na matunzo ya mwanamke hupatikana ndani ya ndoa sio nje ya ndoa. Kabla hajaolewa atatunzwa katika ndoa ya baba yake na mama yake akiolewa atatunzwa na mumewe katika ndoa yake.

Mwanamke anapata mapenzi ya kitandani ndani ya ndoa akiwa na mumewe si kinyume chake.

Mwanamke anapata faraja, kuliwazwa na kubembelezwa ndani ya ndoa sio nje ya ndoa.

Mwanamke atapata nyumba kwa mume wake ndani ya ndoa sio kwenda kupanga au kujenga huo itakuwa ni maskani sio nyumbani.

Mwanamke anapata baraka za MUNGU akiwa chini ya mumewe akitumikia ndoa yake. Haya maisha ya kidunia sio baraka ni mafanikio ambayo yanaweza kuwa na baraka ama yasiwe nayo.

Maisha ya kidunia hayana faida kwa mwanamke asiye na Ndoa ni mahangaiko, hofu, wasi wasi, huzuni kila saa na matatizo ya kiakili.

Maisha hayataki tamaa yanataka utu.
 
Waliotelekezwa na kufanikiwa ni wangapi?
Tunaweza kukosa takwimu sahihi kwa sasa lakini wapo waliotelekezwa na wakafanikiwa.

Ila kwenda kumuomba msaada mtoto uliyemtelekeza huwa ni aibu na hubaki funzo kwa Wazazi wengine wenye nia hiyo
 
Karibu mumy...amka Sali, oga pendeza, wapende sana wanao. Mafanikio sio rahisi ila pia sio magumu na lazima upitie changamoto ili uyafikie.
Dah me nikajua utasema aamke, asali, aoge, awapende sana wanae , awaogeshe pia halafu ahamie kwako umsaidie kupambana na haya maisha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Una uhakika wote tumelelewa na Baba zetu.. vingine ni kama kurithi.. mwanamme aliyekulia mazingira ya kutelekekezwa na Baba na akakua kwa malezi ya Mama kuna uwezekano mkubwa naye akikua akawa katili na kutelekeza watoto.. haoni shida.
Ni sahihi Mkuu, wengi tumeshuhudia wapo hivyo.

Ni kama wanatembea na Kisasi
 
Back
Top Bottom