Msaada: Nawezaje kuacha tabia ya kuongea peke yangu?

Pole man. Haina side effects sana zaidi ya kupoteza muda na kuchoka kutokua productive.

Ila inasaidia kutoa hasira, mawazo, stress na kupass time.

Soma soma kuhusu Maladaptive Day Dreaming.
Shukrani sana mkuu [emoji1545][emoji1545] ..
 
Hakuna mtu ambae haongei peke yake inategemea unaongea vp kimya kmya (kwenye nafsi yako) au kwa sauti kabisa!! Kama unaongea kwa sauti kapima shida ya akili
 
Hiyo ni dalili ya IQ kubwa,nilisoma mahali kuwa kuongea peke yako ni sifa kubwa ya watu wenye uwezo wa hali ya juu kiakili
 
Watu wanaweza wasikuelewe. Ila Mi naelewa.

Yaani mimi naweza jipa safari ya kutembea ili nifanye hiyo kitu, especially nikivaa earphones.

Yangu inaitwa Maladaptive Day Dreaming. Sema haina madhara so naitumia ku-cope na maisha.
Chizi kwenye ubora wake
 
Unakuwa upo kwenye personal meeting, endelea tu mkuu
 
Nashukuru kuona tupo wengi, mwanzoni niliona kama tatizo ..
Hapa duniani hakuna cha peke yako ukiexperience jambo jua kuna watu wengine pia wenye jambo kama hilo.

Mimi mazungumzo yangu huwa ni ya ndani kwa ndani sitoi sauti ila huwa nina vikao vingi mno ndani ya halmashauri ya kichwa changu.
Huwa siboreki kukaa peke yangu maana vikao ni vingi mnoπŸ˜€.
 
First born wangu yupo hivyo ila ni kichwa hatari...walimu wake wanasema mtihani hata uwe ngumu vipi huwa hazidi saa moja amemaliza paper ..mwanzo ilibidi wamuwekee mtego wakidhani ameingia na majibu!
Mimi huwa ninaongea peke yangu mambo mengi ila sitoi sauti wala gestures ila dogo ni sauti hadi vitendo
 
Mkuuu haraka sana iyo ring ya dhahabu itupe mapema kabla mabadiliko ya maumbo hayajaanza.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Funga mdomo na rubber band, kama bado, tumia solar tape kabisa ubane mdomo wote, funga zungushia na koo yote banaa banaa. Kama bado, chukua bubble gum uwe unatafuna tafuna kila siku. Kama bado nenda haraka Mirembe hosp upate matibabu haraka, huo ni ukichaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…