Msaada: Ni mara ya pili nataka kujidhuru

Pole sana mkuu

Tatizo linakuja pale unapotarajia watu wawe pamoja na wewe.
Kubali upweke kisha anza upya ukiwa mwenyewe.

kama kuna wanaokutegemea angalia usiwaumize kwa kifo chako utakuwa huna tofauti na ndugu wanaokuchora leo.

Ongeza upendo kwa watu wote, wala usitarajie wakulipe kama ufanyavyo.

Kumbuka hata sisi tunaokushauri inawezekana tunapitia magumu zaidi yako.
 
Mkuu kila mtu maisha magumu.Me mwenyewe nawaza mawazo mabaya tu miezi 2 sasa.

Hali ya maisha ngumu na pesa hamna hali si hali.Hapa yenyewe sielewi nitakula nini? Lakini najipa moyo kuwa hali hii itapita
 
You are too soft my friend, hilo la kukufanya utake kujitoa roho!?,mtu anafiwa wazazi na ndugu zake wote akiwa mdogo anabaki yeye na anateswa na wanaomtunza na bado anapambana, wewe unataka kujitoa roho Kwa hizi sababu za kitoto??., Hii Dunia ni ya kupambana sio lelemama.
 
wacha kudeka maisha hayako ivyo mkuu we kitinda mimba sio
 
Unataka kujirusha ghorofani ufe. Si Bora ufie pale Riverside!
Tuseme nzi kafia kidondani.
 
Mwombe Yesu Kristo akusaidie hata kama humwamini au umefanya dhambi kubwa kiasi gani utaona matokeo.
 
Poleh sana
Usisahau kuwa Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi zaidi ya uwezo wake
Jipe moyo pambana
Wote tuna shida arif, sana tu
Ila tunaona ngoja tukae tuone what next
 
Pole sana kaza moyo mkuu kuombe mungu sana na jichanganye na jamii inayokupa furaha pia
 
Una elimu gan , jinsia?
 
Mkuu pole sana, mwaka 2013 mimi nilikuwa najiskia nitafute kamba nijinyonge na nilipitia hayo unayopitia, nilivuka kwa kumtafuta Mchungaji, akaniombea mara ya kwanza sikukaa sawa mara ya pili ndipo nikakaa sawa.
Umetupiwa pepo kwa sababu una kitu cha thamani umebeba.
 
Kimbilia kanisani kwa wachungaji wakakuombee haraka.umetupiwa jini akutoe roho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…